Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Samuel 13
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. 2 Samuel 3.2-3.3 1 Chroniques 3.9 1 Chroniques 3.2 2 Samuel 14.27 1 Rois 11.1
2 Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote. 2 Corinthiens 7.10 1 Rois 21.4 Cantique 5.8
3 Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. 1 Samuel 16.9 Genèse 38.1 2 Samuel 14.2 Genèse 38.20 2 Samuel 13.32
4 Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, umbu la ndugu yangu, Absalomu. Michée 7.3 Lévitique 18.9 Luc 12.32 Lévitique 20.17 Jérémie 8.12
5 Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake. 2 Samuel 16.21-17.4 Marc 6.24-6.25 Actes 23.15 Psaumes 50.18-50.19 Proverbes 19.27
6 Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula mkononi mwake. Genèse 18.6 Matthieu 13.33
7 Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari, akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie chakula. 8 Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake, akaioka mikate. 9 Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Wakatoka kila mtu kwake. Genèse 45.1 Juges 3.19 Jean 3.20
10 Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. 11 Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Genèse 39.11-39.12
12 Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Juges 20.6 Lévitique 20.17 Juges 19.23 Genèse 34.7 Lévitique 18.9
13 Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. Genèse 19.8 Juges 19.24 Genèse 20.12
14 Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. 2 Samuel 12.11 Esther 7.8 Deutéronome 22.25-22.27 Juges 20.5
15 Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Ezéchiel 23.17
16 Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. 17 Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. 18 Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake. Genèse 37.3 Juges 5.30 Psaumes 45.13-45.14 Genèse 37.32 Genèse 37.23
19 Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti. Jérémie 2.37 Josué 7.6 2 Samuel 1.2 Job 2.12 1 Samuel 4.12
20 Huyo Absalomu nduguye akamwambia, je! Amekuwa nawe Amnoni nduguyo? Ila sasa tulia, dada; ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili. Basi Tamari akakaa hali ya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu. Genèse 34.2 Romains 12.19 Proverbes 26.24 Genèse 46.15
21 Na mfalme Daudi alipoyasikia maneno hayo yote, alikasirika sana. Genèse 34.7 2 Samuel 3.28-3.29 1 Samuel 2.29 1 Samuel 2.22-2.25 2 Samuel 12.5
22 Ila Absalomu hakusema na Amnoni wala kwa heri wala kwa shari; kwa maana Absalomu alimchukia Amnoni kwa kumtenza nguvu umbu lake Tamari. Lévitique 19.17-19.18 Genèse 31.24 1 Jean 3.15 Genèse 24.50 Matthieu 18.15
23 Ikawa baada ya miaka miwili mizima, Absalomu alikuwa na wenye kukata manyoya ya kondoo huko Baal-hasori uliopo upande wa Efraimu; naye Absalomu akawaalika wana wote wa mfalme. 1 Samuel 25.4 Genèse 38.12-38.13 1 Rois 1.9 2 Chroniques 26.10 1 Samuel 25.7
24 Absalomu akamjia mfalme, akasema, Tazama sasa, mimi mtumwa wako ninao wakata manyoya ya kondoo; basi mfalme na aende, nakusihi, na watumishi wake pamoja nami mtumwa wako. 2 Samuel 11.8-11.15 Psaumes 55.21 Psaumes 12.2 Jérémie 41.6-41.7
25 Mfalme akamwambia Absalomu, Sivyo, mwanangu, tusiende sote, tusije tukakulemea. Akamsihi sana; asikubali kwenda, ila akambariki. Luc 14.23 Actes 16.15 Genèse 19.2-19.3 Ruth 2.4 2 Samuel 14.22
26 Ndipo akasema Absalomu, Kwamba huji, nakusihi, mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi. 2 Samuel 3.27 2 Samuel 11.13-11.15 Psaumes 55.21 2 Samuel 20.9
27 Mfalme akamwambia, Kwa nini aende nawe? Lakini Absalomu akamsihi sana, naye akamwacha Amnoni na wana wote wa mfalme waende naye. Proverbes 26.24-26.26
28 Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, iweni na ujasiri. Juges 19.6 Juges 19.22 Juges 19.9 Ruth 3.7 1 Samuel 25.36-25.38
29 Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila mtu nyumbu wake, wakakimbia. 2 Samuel 18.9 1 Rois 1.33 Proverbes 29.12 Michée 7.3 1 Samuel 22.18-22.19
30 Ikawa, walipokuwa njiani, habari zikamwasilia Daudi, kusema, Absalomu amewaua wana wote wa mfalme, wala hata mmoja wao hakusalia. 31 Ndipo mfalme akainuka, akararua nguo zake, akalala chini; nao watumishi wake wote wakasimama karibu naye, wenye nguo zao zimeraruliwa. 2 Samuel 1.11 2 Samuel 12.16 2 Samuel 3.31 Genèse 37.34 Josué 7.6
32 Akajibu Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akasema, Asidhani bwana wangu ya kwamba wamewaua vijana wote, wana wa mfalme; maana ndiye Amnoni peke yake aliyekufa; yakini haya yamekusudiwa kwa kinywa chake Absalomu tangu siku ile alipotenzwa nguvu umbu lake, Tamari. Genèse 27.41 1 Samuel 16.9 Psaumes 7.14 Proverbes 24.11-24.12 2 Samuel 13.3
33 Basi sasa bwana wangu mfalme asilitie neno hili moyoni, kudhani ya kwamba wana wote wa mfalme wamekufa maana ni Amnoni peke yake aliyekufa. 2 Samuel 19.19
34 Lakini Absalomu akakimbia. Na kijana yule aliyekuwa mlinzi akainua macho yake, akaona, na tazama, kuna watu wengi wanakuja kwa njia ya upande wa kilima nyuma yake. Genèse 4.8-4.14 Amos 5.19 Proverbes 28.17 2 Samuel 13.37-13.38
35 Ndipo Yonadabu akamwambia mfalme, Tazama, wana wa mfalme wamekuja; kama mimi mtumwa wako nilivyosema, ndivyo ilivyo. 36 Ikawa alipokwisha kusema, tazama, wana wa mfalme walikuja, nao wakapaza sauti zao wakalia; mfalme naye akalia, na watumishi wake wote, kilio kikubwa mno. 2 Samuel 12.21 2 Samuel 13.15 2 Samuel 18.33
37 Lakini Absalomu akakimbia, akamwendea Talmai, mwana wa Amihuri, mfalme wa Geshuri. Naye Daudi akamlilia mwanawe kila siku. 2 Samuel 3.3 2 Samuel 14.23 2 Samuel 13.34 2 Samuel 14.32 1 Chroniques 3.2
38 Basi Absalomu akakimbia, akaenda Geshuri, akakaa huko muda wa miaka mitatu. 2 Samuel 14.23 2 Samuel 14.32 2 Samuel 15.8
39 Mfalme Daudi akatamani kutoka kumwendea Absalomu kwa kuwa ametulizwa kwa habari ya Amnoni, kwa maana amekufa. Genèse 38.12 Genèse 24.67 Genèse 37.35 Psaumes 84.2 Psaumes 119.20

Cette Bible est dans le domaine public.