Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
2 Samuel 13.7 Bible en Swahili de l’est
Viol de Tamar par Amnon
1 Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. 1 Chroniques 3.9 2 Samuel 3.2-3.3 1 Chroniques 3.2 2 Samuel 14.27 Genèse 6.2 2 Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote. 2 Corinthiens 7.10 1 Rois 21.4 Cantique 5.8 3 Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. 1 Samuel 16.9 1 Corinthiens 3.19 Jérémie 4.22 Esther 5.10 Genèse 3.1 4 Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, umbu la ndugu yangu, Absalomu. Lévitique 18.9 Luc 12.32 Lévitique 20.17 Jérémie 8.12 Esaïe 3.9 5 Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake. 2 Samuel 16.21-17.4 Marc 6.24-6.25 Actes 23.15 Psaumes 50.18-50.19 Proverbes 19.27 6 Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula mkononi mwake. Genèse 18.6 Matthieu 13.33 7 Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari, akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie chakula. 8 Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake, akaioka mikate. 9 Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Wakatoka kila mtu kwake. Genèse 45.1 Juges 3.19 Jean 3.20 10 Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. 11 Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Genèse 39.11-39.12 12 Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Juges 19.23 Juges 20.6 Lévitique 20.17 Genèse 34.7 Lévitique 18.9 13 Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. Genèse 19.8 Juges 19.24 Genèse 20.12 14 Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. 2 Samuel 12.11 Esther 7.8 Deutéronome 22.25-22.27 Juges 20.5 15 Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Ezéchiel 23.17 16 Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. 17 Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. 18 Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake. Genèse 37.3 Juges 5.30 Psaumes 45.13-45.14 Genèse 37.32 Genèse 37.23 19 Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti. Josué 7.6 Jérémie 2.37 2 Samuel 1.2 Job 2.12 1 Samuel 4.12 20 Huyo Absalomu nduguye akamwambia, je! Amekuwa nawe Amnoni nduguyo? Ila sasa tulia, dada; ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili. Basi Tamari akakaa hali ya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu. Genèse 34.2 Romains 12.19 Proverbes 26.24 Genèse 46.15 21 Na mfalme Daudi alipoyasikia maneno hayo yote, alikasirika sana. Genèse 34.7 2 Samuel 3.28-3.29 1 Samuel 2.29 1 Samuel 2.22-2.25 2 Samuel 12.5 22 Ila Absalomu hakusema na Amnoni wala kwa heri wala kwa shari; kwa maana Absalomu alimchukia Amnoni kwa kumtenza nguvu umbu lake Tamari. Lévitique 19.17-19.18 Genèse 31.24 1 Jean 3.15 Genèse 24.50 Proverbes 25.9