Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 5.10
Bible en Swahili de l’est


1 Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu? Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?Job 15.15 Hébreux 12.1 Psaumes 16.3 Deutéronome 33.2-33.3 Psaumes 106.16
2 Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.Job 18.4 Proverbes 8.5 Psaumes 92.6 Proverbes 1.22-1.23 Psaumes 107.17
3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara niliyalaani maskani yake.Psaumes 73.18-73.20 Psaumes 37.35-37.36 Actes 1.20 Deutéronome 27.15-27.26 Psaumes 73.3-73.9
4 Watoto wake wako mbali na wokovu, Nao wamesongwa langoni, Wala hapana atakayewaponya.Psaumes 127.5 Psaumes 119.155 Job 10.7 Job 1.19 Psaumes 109.9-109.15
5 Mavuno yake wale wenye njaa huyala, Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani, Nao wenye kiu huzitwetea mali zao.Lamentations 2.16 Jérémie 51.44 Job 18.8-18.10 Osée 8.7 Lamentations 2.5
6 Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi;1 Samuel 6.9 Osée 10.4 Amos 3.6 Deutéronome 32.27 Lamentations 3.38
7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka, Kama cheche za moto zirukavyo juu.Job 14.1 Genèse 3.17-3.19 1 Corinthiens 10.13 Ecclésiaste 5.15-5.17 Ecclésiaste 2.22
8 Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu daawa yangu;Psaumes 50.15 Psaumes 37.5 1 Pierre 4.19 1 Pierre 2.23 Psaumes 77.1-77.2
9 Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;Psaumes 40.5 Job 9.10 Psaumes 72.18 Romains 11.33 Esaïe 40.28
10 Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani;Jérémie 14.22 Actes 14.17 Psaumes 147.8 Jérémie 5.24 Job 36.28
11 Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama.1 Samuel 2.7-2.8 Luc 1.52-1.53 Psaumes 91.14 Jacques 1.9 Psaumes 107.41
12 Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.Esaïe 8.10 Néhémie 4.15 Psaumes 33.10-33.11 Psaumes 21.11 Proverbes 21.30
13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.Psaumes 9.15-9.16 1 Corinthiens 1.19-1.20 Luc 1.51 1 Corinthiens 3.19 Esther 9.25
14 Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku.Job 12.25 Esaïe 59.10 Deutéronome 28.29 Proverbes 4.19 Amos 8.9
15 Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.Psaumes 35.10 Psaumes 109.31 Psaumes 140.12 Job 4.10 Psaumes 72.4
16 Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake.Psaumes 107.42 Psaumes 63.11 1 Samuel 2.8-2.9 Esaïe 14.32 Romains 3.19
17 Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.Psaumes 94.12 Jacques 1.12 Hébreux 12.5-12.11 Jérémie 31.18 Apocalypse 3.19
18 Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.Osée 6.1 Esaïe 30.26 Deutéronome 32.39 1 Samuel 2.6 Psaumes 147.3
19 Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.Psaumes 34.19 1 Corinthiens 10.13 Proverbes 24.16 Psaumes 91.3-91.10 2 Corinthiens 1.8
20 Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.Psaumes 33.19 Genèse 45.7 1 Rois 17.6 Matthieu 24.6 Osée 13.14
21 Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.Psaumes 31.20 Jacques 3.5-3.8 Proverbes 12.18 Psaumes 55.21 Esaïe 54.17
22 Wewe utayacheka maangamizo na njaa; Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.Ezéchiel 34.25 Esaïe 35.9 Esaïe 65.25 2 Rois 19.21 Osée 2.18
23 Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara; Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako.Ezéchiel 14.15-14.16 Romains 8.38-8.39 Daniel 6.22 Esaïe 11.6-11.9 Osée 2.18
24 Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama; Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu.Psaumes 91.10 Psaumes 121.7-121.8 Job 18.6 Psaumes 107.4 Deutéronome 28.6
25 Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi, Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi.Psaumes 112.2 Psaumes 72.16 Genèse 15.5 Psaumes 128.3-128.6 Job 42.13-42.16
26 Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.Genèse 15.15 Proverbes 9.11 Proverbes 10.27 Genèse 25.8 Psaumes 91.16
27 Tazama, haya tumeyapeleleza, ndivyo yalivyo; Yasikie, uyajue, ili upate mema.Psaumes 111.2 Job 15.17 Job 12.2 Deutéronome 10.13 Job 15.9-15.10

Cette Bible est dans le domaine public.