Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 18
Bible en Swahili de l’est


1 Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. Actes 19.1 2 Timothée 4.20 2 Corinthiens 1.23 2 Corinthiens 1.1 1 Corinthiens 1.2
2 Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao; 1 Corinthiens 16.19 2 Timothée 4.19 Actes 11.28 Actes 18.26 Romains 16.3-16.4
3 na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema. 1 Corinthiens 4.12 1 Thessaloniciens 2.9 2 Corinthiens 11.7 2 Corinthiens 11.9 2 Corinthiens 12.13
4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani. Actes 17.17 2 Chroniques 32.11 Actes 19.8 Actes 19.26 2 Corinthiens 5.11
5 Hata Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na lile neno, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo. Actes 18.28 Actes 17.3 Actes 20.21 Jérémie 6.11 2 Corinthiens 5.14
6 Walipopingamana naye na kumtukana Mungu, akakung’uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa. Ezéchiel 33.4 2 Samuel 1.16 Ezéchiel 18.13 Actes 13.51 Néhémie 5.13
7 Akaondoka huko akaingia katika nyumba ya mtu mmoja jina lake Tito Yusto, mcha Mungu, ambaye nyumba yake ilikuwa mpaka mmoja na sinagogi. Actes 16.14 Colossiens 4.11 Actes 17.4 Actes 10.22 Actes 13.42
8 Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa. Actes 8.12 Actes 11.14 Romains 10.14-10.17 Genèse 17.27 Actes 8.35-8.38
9 Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, Actes 27.23-27.25 Ezéchiel 2.6-2.8 Actes 23.11 2 Corinthiens 12.1-12.3 1 Thessaloniciens 2.2
10 kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. Matthieu 28.20 Exode 4.12 2 Corinthiens 12.9 Romains 10.20-10.21 Jean 10.16
11 Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu. Actes 19.10 Actes 14.3 Actes 20.31
12 Hata Galio alipokuwa liwali wa Akaya, Wayahudi wakamwinukia Paulo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu, Actes 13.7 Actes 18.27 2 Corinthiens 1.1 Actes 13.50 1 Corinthiens 16.15
13 wakisema Mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria. Actes 24.5-24.6 Actes 21.28 Actes 18.4 Actes 6.13 Actes 18.15
14 Na Paulo alipotaka kufunua kinywa chake, Galio akawaambia Wayahudi, Kama lingekuwa jambo la dhuluma au la hila mbaya, enyi Wayahudi, ingekuwa haki mimi kuchukuliana nanyi; Hébreux 5.2 1 Pierre 3.14-3.15 Actes 13.18 Actes 21.39-22.2 Actes 25.18-25.20
15 bali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sheria yenu, liangalieni ninyi wenyewe, maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo. Actes 23.29 Actes 25.19 Actes 25.11 1 Timothée 6.4 Tite 3.9
16 Akawafukuza waondoke mbele ya kiti cha hukumu. Romains 13.3-13.4 Psaumes 76.10 Apocalypse 12.16
17 Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu. 1 Corinthiens 1.1 1 Corinthiens 1.23 Actes 17.32 Amos 6.6
18 Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. Romains 16.1 Actes 21.24 Nombres 6.18 Actes 18.2 1 Corinthiens 9.20
19 Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi. Actes 19.1 1 Corinthiens 16.8 Actes 18.24 1 Timothée 1.3 Ephésiens 1.1
20 Walipomtaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali; Actes 21.13-21.14 Actes 20.16 Marc 1.37-1.38 1 Corinthiens 16.12
21 bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso, Jacques 4.15 1 Corinthiens 4.19 Actes 20.16 Romains 1.10 Hébreux 6.3
22 na alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu kanisa, kisha akatelemkia Antiokia. Actes 8.40 Actes 21.17-21.19 Actes 25.1 Actes 25.9 Actes 23.23
23 Hata akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwathibitisha wanafunzi. Actes 14.22 Actes 16.6 Actes 15.32 Actes 15.41 1 Thessaloniciens 5.14
24 Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. 1 Corinthiens 4.6 Tite 3.13 1 Corinthiens 1.12 1 Corinthiens 16.12 1 Corinthiens 3.5-3.6
25 Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohana tu. Actes 19.3 Romains 12.11 Genèse 18.19 Actes 19.23 Marc 12.14
26 Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi. Proverbes 25.12 1 Corinthiens 8.2 Luc 24.27 Marc 10.15 Actes 28.23
27 Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe, naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Philippiens 1.29 Actes 18.12 2 Corinthiens 1.24 Philippiens 1.25 Actes 19.1
28 Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo. Actes 18.5 Actes 9.22 Luc 24.44 Luc 24.27 1 Corinthiens 15.3-15.4

Cette Bible est dans le domaine public.