Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Corinthiens 11.26
Bible en Swahili de l’est


1 Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami.2 Corinthiens 11.4 2 Corinthiens 11.19 2 Corinthiens 5.13 2 Corinthiens 11.21 2 Corinthiens 11.16-11.17
2 Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.Osée 2.19-2.20 Esaïe 54.5 Ephésiens 5.26-5.27 Jean 3.29 Lévitique 21.13-21.15
3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.1 Timothée 2.14 Apocalypse 12.9 Colossiens 2.4 Galates 1.6 Colossiens 2.8
4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!Galates 1.6-1.8 1 Corinthiens 3.11 Romains 8.15 Ephésiens 4.4-4.5 Actes 4.12
5 Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu.2 Corinthiens 12.11-12.12 Galates 2.6-2.9 1 Corinthiens 15.10
6 Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu.Ephésiens 3.4 1 Corinthiens 1.17 2 Corinthiens 4.2 2 Corinthiens 5.11 2 Corinthiens 12.12
7 Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?2 Corinthiens 12.13 1 Thessaloniciens 2.9 2 Corinthiens 10.1 1 Corinthiens 9.6 Actes 20.34
8 Naliwanyang’anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi.2 Corinthiens 11.9 Philippiens 4.14-4.16 Philippiens 4.18
9 Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda.1 Thessaloniciens 2.6 1 Thessaloniciens 2.9 2 Corinthiens 12.13-12.16 2 Thessaloniciens 3.8-3.9 Philippiens 4.10-4.16
10 Kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya.Romains 9.1 Actes 18.12 Romains 1.9 2 Corinthiens 1.23 Actes 18.27
11 Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.2 Corinthiens 12.15 2 Corinthiens 6.11-6.12 2 Corinthiens 7.3 Jean 2.24-2.25 2 Corinthiens 12.2-12.3
12 Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi.1 Corinthiens 9.12 Galates 6.13-6.14 Galates 1.7 1 Corinthiens 5.6 2 Corinthiens 11.18
13 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.Apocalypse 2.2 Galates 2.4 Galates 1.7 Philippiens 3.2 1 Jean 4.1
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.Galates 1.8 Apocalypse 12.9 2 Corinthiens 2.11 2 Corinthiens 11.3 Matthieu 4.1-4.10
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.Philippiens 3.19 Jérémie 23.14-23.15 Jude 1.4 2 Corinthiens 3.9 Ephésiens 6.12
16 Nasema tena, mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; ili mimi nami nipate kujisifu ngaa kidogo.2 Corinthiens 11.1 2 Corinthiens 12.6 2 Corinthiens 11.21-11.23 2 Corinthiens 11.19 2 Corinthiens 12.11
17 Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.1 Corinthiens 7.12 2 Corinthiens 9.4 1 Corinthiens 7.6 1 Corinthiens 7.25 2 Corinthiens 11.18-11.27
18 Kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu.Philippiens 3.3-3.4 2 Corinthiens 12.11 1 Pierre 1.24 2 Corinthiens 12.5-12.6 2 Corinthiens 11.12
19 Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha.1 Corinthiens 4.10 1 Corinthiens 8.1 1 Corinthiens 10.15 Apocalypse 3.17
20 Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.Galates 2.4 Galates 5.1 Galates 4.3 Galates 4.9 2 Corinthiens 1.24
21 Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri.2 Corinthiens 10.10 2 Corinthiens 10.1-10.2 2 Corinthiens 11.22-11.27 2 Corinthiens 11.17 Philippiens 3.3-3.6
22 Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia.Philippiens 3.5 Romains 11.1 Romains 9.4 Jean 8.33-8.39 Exode 3.18
23 Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.2 Corinthiens 6.4-6.5 1 Corinthiens 15.10 Actes 9.16 2 Corinthiens 3.6 1 Corinthiens 3.5
24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.Deutéronome 25.2-25.3 Marc 13.9 Matthieu 10.17
25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;Actes 14.19 Actes 14.5 Hébreux 11.37 Actes 16.22-16.23 Actes 16.37
26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;Actes 14.5 Actes 20.19 Actes 17.5 Actes 13.50 Actes 25.3
27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.2 Corinthiens 6.5 Philippiens 4.12 2 Thessaloniciens 3.8 1 Thessaloniciens 2.9 1 Corinthiens 4.11-4.12
28 Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.Actes 20.18-20.35 Romains 1.14 Romains 16.4 Actes 18.23 Romains 15.16
29 Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe?1 Corinthiens 8.13 1 Corinthiens 9.22 Néhémie 5.6-5.13 Apocalypse 2.20 Galates 6.2
30 Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu.1 Corinthiens 2.3 2 Corinthiens 12.5-12.11 Colossiens 1.24 2 Corinthiens 11.16-11.18 Jérémie 9.23-9.24
31 Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo.Romains 9.5 Romains 1.25 Jean 10.30 Ephésiens 1.3 2 Corinthiens 11.11
32 Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata;Actes 9.24-9.25 2 Corinthiens 11.26
33 nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake.Actes 9.25 1 Samuel 19.12 Josué 2.18

Cette Bible est dans le domaine public.