Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Rois 15.5
Bible en Swahili de l’est


1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli Uzia mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala.2 Rois 15.13 2 Chroniques 26.3-26.4 2 Rois 14.21 2 Chroniques 26.1 2 Rois 14.16-14.17
2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na miwili huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu.2 Chroniques 26.3-26.4
3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama yote aliyoyafanya babaye Amazia.2 Rois 14.3-14.4 2 Chroniques 26.4 2 Rois 12.2-12.3
4 Ila mahali pa juu hapakuondolewa, nao watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.2 Rois 14.4 1 Rois 22.43 1 Rois 15.14 2 Chroniques 17.6 2 Chroniques 34.3
5 Bwana akampiga mfalme, akawa na ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee. Na Yothamu mwana wa mfalme alikuwa juu ya nyumba, akiwahukumu watu wa nchi.Lévitique 13.46 Nombres 12.14 1 Rois 3.9 2 Rois 5.27 2 Samuel 8.15
6 Basi mambo yote ya Uzia yaliyosalia, nayo yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?2 Chroniques 26.5-26.15 2 Rois 14.18
7 Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi; na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.2 Chroniques 26.23 Esaïe 6.1
8 Katika mwaka wa thelathini na nane wa Uzia mfalme wa Yuda Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria miezi sita.2 Rois 14.29-15.1 2 Rois 14.16-14.17 2 Rois 14.21
9 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana kama walivyofanya babaze; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.2 Rois 10.29 2 Rois 14.24 2 Rois 13.2 2 Rois 13.11 2 Rois 10.31
10 Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake.2 Rois 15.14 1 Rois 16.9-16.10 2 Rois 9.24 1 Rois 15.28 2 Rois 15.25
11 Basi mambo yote ya Zekaria yaliyosalia, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.2 Rois 14.28
12 Hilo ndilo neno la Bwana alilomwambia Yehu, akisema, Wana wako watakaa kitini mwa Israeli hata kizazi cha nne. Ikawa vivyo hivyo.2 Rois 10.30 2 Rois 14.29 2 Rois 10.10 2 Rois 13.1 Jean 19.36-19.37
13 Huyo Shalumu mwana wa Yabeshi alianza kutawala katika mwaka wa thelathini na kenda wa Uzia mfalme wa Yuda; akatawala muda wa mwezi mmoja katika Samaria.2 Rois 15.1 1 Rois 16.15 2 Rois 15.8 Proverbes 28.17 1 Rois 16.24
14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza, akaja Samaria, akampiga Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamwua, akatawala mahali pake.1 Rois 14.17 1 Rois 15.33 1 Rois 16.15 1 Rois 16.17 1 Rois 16.8-16.9
15 Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na fitina aliyoifanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli.2 Rois 15.11 1 Rois 14.19 1 Rois 22.39 1 Rois 14.29
16 Ndipo Menahemu akapiga Tifsa, na wote waliokuwamo, na mipaka yake, toka Tirza; kwa sababu hawakumfungulia, kwa hiyo akaupiga; nao wanawake wote waliokuwamo wenye mimba akawapasua.2 Rois 8.12 Osée 13.16 1 Rois 4.24 Amos 1.13
17 Katika mwaka wa thelathini na kenda wa Uzia mfalme wa Yuda Menahemu mwana wa Gadi alianza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka kumi katika Samaria. 18 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha siku zake zote makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli. 19 Akaja Pulu mfalme wa Ashuru juu ya nchi; naye Menahemu akampa Pulu talanta elfu za fedha, ili kwamba mkono wake uwe pamoja naye, na ufalme uwe imara mkononi mwake.2 Rois 14.5 1 Chroniques 5.25-5.26 Jérémie 17.5 2 Rois 16.8 Osée 10.6
20 Na Menahemu akawatoza Israeli fedha hiyo, yaani, wakuu wote wenye mali, kila mtu shekeli hamsini za fedha, ili ampe huyo mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akarejea, wala hakukaa huko katika nchi.2 Rois 17.3-17.4 2 Rois 23.35 Job 1.3 2 Samuel 19.32 Ruth 2.1
21 Basi mambo yote ya Menahemu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 22 Menahemu akalala na babaze; na Pekahia mwanawe akatawala mahali pake. 23 Katika mwaka wa hamsini wa Uzia mfalme wa Yuda Pekahia mwana wa Menahemu alianza kutawala juu ya Israeli hatika Samaria; akatawala miaka miwili.1 Rois 15.25 1 Rois 16.8 1 Rois 22.51 Job 20.5 2 Rois 21.19
24 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.2 Rois 15.9 2 Rois 15.18
25 Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia fitina, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.2 Chroniques 28.6 2 Rois 15.27 2 Rois 15.10 2 Rois 9.5 1 Rois 16.9
26 Basi mambo yote ya Pekahia yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini.Esaïe 7.1 Esaïe 7.4 2 Rois 15.23 2 Rois 15.8 2 Rois 15.2
28 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.2 Rois 15.18 2 Rois 21.2 2 Rois 13.2 2 Rois 15.9 2 Rois 13.6
29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.1 Chroniques 5.26 2 Rois 16.7 2 Rois 17.6 1 Rois 15.20 Josué 20.7
30 Na Hoshea mwana wa Ela akafanya fitina juu ya Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.2 Rois 17.1 2 Rois 16.1 2 Chroniques 28.4-28.6 Esaïe 8.6 2 Rois 15.10
31 Basi mambo yote ya Peka yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 32 Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala.2 Rois 15.7 1 Chroniques 3.12 2 Rois 14.21 Matthieu 1.9 2 Rois 15.27
33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki.2 Chroniques 27.1
34 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana; akafanya kama yote aliyoyafanya Uzia baba yake.2 Chroniques 26.4-26.5 2 Rois 15.3-15.4 2 Chroniques 27.2
35 Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu walikuwa wakitoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya Bwana.2 Rois 12.3 2 Chroniques 23.20 2 Chroniques 32.12 2 Rois 18.4 2 Rois 15.4
36 Basi mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?2 Rois 15.6-15.7 2 Chroniques 27.4-27.9
37 Zamani hizo akaanza Bwana kumtuma juu ya Yuda Resini mfalme wa Shamu, na Peka mwana wa Remalia.Esaïe 7.1 2 Rois 16.5 2 Chroniques 28.6 Luc 21.28 Jérémie 43.10
38 Yothamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi baba yake. Na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.2 Chroniques 28.1 1 Rois 1.2 2 Samuel 7.12 1 Rois 14.31 Matthieu 1.9

Cette Bible est dans le domaine public.