Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Samuel 2
Bible en Swahili de l’est


1 Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako; Esaïe 12.2-12.3 Psaumes 92.10 Psaumes 13.5 Psaumes 9.14 Psaumes 89.17
2 Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. 2 Samuel 22.32 Exode 15.11 Psaumes 89.8 Psaumes 86.8 Deutéronome 32.30-32.31
3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. 1 Rois 8.39 Proverbes 8.13 Daniel 4.30-4.31 Job 31.6 Daniel 4.37
4 Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. Psaumes 37.15 Psaumes 46.9 Psaumes 76.3 Hébreux 11.34 2 Corinthiens 12.9
5 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. Jérémie 15.9 Psaumes 113.9 Esaïe 54.1 Galates 4.27 1 Samuel 1.6
6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. Deutéronome 32.39 Esaïe 26.19 2 Rois 5.7 Osée 6.1-6.2 Apocalypse 1.18
7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Psaumes 75.7 Job 5.11 Deutéronome 8.17-8.18 Jacques 4.10 Job 1.21
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Psaumes 113.7-113.8 Psaumes 104.5 Job 38.4-38.6 2 Samuel 7.8 Psaumes 102.25
9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Psaumes 33.16-33.17 Psaumes 91.11-91.12 Psaumes 121.3 Matthieu 8.12 1 Pierre 1.5
10 Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake. Psaumes 2.9 Psaumes 89.24 Psaumes 96.13 Psaumes 98.9 Psaumes 21.1
11 Kisha Elkana akaenda Rama nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia Bwana mbele yake Eli, kuhani. 1 Samuel 2.18 1 Samuel 3.1 1 Samuel 1.28 1 Samuel 1.19 1 Samuel 3.15
12 Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali Bwana, Jérémie 2.8 Romains 1.21 Romains 1.28-1.30 2 Corinthiens 6.15 Juges 2.10
13 wala haki ya makuhani ilivyokuwa kwa watu. Wakati huo mtu ye yote alipotoa dhabihu wakati wo wote, ndipo huja mtumishi wa kuhani, nyama ilipokuwa katika kutokota, naye akawa na uma wa meno matatu mkononi mwake; Lévitique 7.29-7.34
14 naye huutia kwa nguvu humo chunguni, au birikani, au sufuriani, au chomboni; nyama yote iliyoinuliwa kwa huo uma kuhani huichukua mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokuja huko. 2 Pierre 2.13-2.15 Lévitique 7.34 1 Samuel 2.29 Malachie 1.10 Exode 29.27-29.28
15 Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, huja mtumishi wa kuhani, akamwambia yule mwenye kuitoa dhabihu, Mtolee kuhani nyama ya kuoka; kwa kuwa hataki kupewa nyama iliyotokoswa, bali nyama mbichi. Lévitique 3.16 Romains 16.18 Lévitique 3.3-3.5 Philippiens 3.19 Jude 1.12
16 Tena, ikiwa mtu yule amwambia, Hawakosi wataichoma moto hayo mafuta kwanza, kisha utwae kadiri roho yako itakavyopenda; ndipo husema, Sivyo, lakini sharti unipe sasa hivi; la, hunipi, basi nitaitwaa kwa nguvu. Lévitique 7.23-7.25 1 Pierre 5.2-5.3 Lévitique 3.16 Michée 2.1-2.2 Néhémie 5.15
17 Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa Bwana; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya Bwana. Genèse 6.11 Malachie 2.13 Psaumes 51.4 2 Rois 21.6 Malachie 2.7-2.9
18 Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za Bwana, naye alikuwa kijana, mwenye kuvaa naivera ya kitani. 1 Samuel 3.1 1 Samuel 2.11 Exode 28.4 2 Samuel 6.14 1 Samuel 22.18
19 Tena mamaye humfanyizia kanzu ndogo, na kumletea mwaka kwa mwaka, hapo alipokwea pamoja na mumewe ili kutoa dhabihu kila mwaka. 1 Samuel 1.3 1 Samuel 1.21 Exode 23.14
20 Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, Bwana na akupe uzao kwa mwanamke huyu, badala ya azimo aliloazimiwa Bwana. Kisha wakaenda nyumbani kwao. 1 Samuel 1.27-1.28 Genèse 14.19 Nombres 6.23-6.27 Luc 2.34 Ruth 4.11
21 Naye Bwana akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za Bwana. Genèse 21.1 Juges 13.24 1 Samuel 2.26 Luc 2.40 1 Samuel 3.19
22 Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. Exode 38.8 1 Samuel 2.13-2.17 1 Samuel 8.1 Osée 4.9-4.11 Jérémie 7.9-7.10
23 Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote. Esaïe 3.9 Philippiens 3.19 Actes 9.4 1 Rois 1.6 Jérémie 3.3
24 Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana. Apocalypse 2.20 2 Rois 10.31 1 Samuel 2.22 1 Rois 13.18-13.21 1 Rois 15.30
25 Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua. Nombres 15.30 Josué 11.20 1 Samuel 3.14 Hébreux 10.26 Hébreux 7.25
26 Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa Bwana, na kwa watu pia. Luc 2.52 Romains 14.18 Proverbes 3.3 Luc 1.80 Luc 2.40
27 Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli, akamwambia, Bwana asema hivi, Je! Mimi sikujidhihirisha nafsi yangu kwa nyumba ya baba yako, walipokuwa katika Misri, wakiitumikia nyumba ya Farao? Exode 4.27 Juges 13.6 1 Rois 13.1 Exode 4.14-4.16 Deutéronome 33.1
28 Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto? Exode 28.1 Lévitique 8.7-8.8 Lévitique 7.7-7.8 Nombres 18.19 Nombres 5.9-5.10
29 Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema? Matthieu 10.37 1 Samuel 2.13-2.17 Deutéronome 12.5-12.6 Deutéronome 32.15 Ezéchiel 13.19
30 Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu. Exode 29.9 Jérémie 18.9-18.10 Proverbes 3.9-3.10 Jean 12.26 Esaïe 29.13
31 Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee. 1 Samuel 22.17-22.20 Job 22.9 1 Rois 2.35 1 Samuel 14.3 Ezéchiel 30.21-30.24
32 Nawe utalitazama teso la maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele. Zacharie 8.4 Psaumes 78.59-78.64 1 Samuel 4.11 1 Samuel 4.4 1 Samuel 4.22
33 Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa wapatapo kuwa watu wazima. 1 Rois 2.26-2.27 1 Rois 1.7 1 Samuel 22.21-22.23 1 Rois 1.19 Matthieu 2.16-2.18
34 Na hii ndiyo ishara itakayokuwa kwako, itakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; watakufa wote wawili katika siku moja. 1 Rois 13.3 1 Samuel 4.11 1 Samuel 4.17 1 Rois 14.12 1 Samuel 3.12
35 Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele. 1 Rois 11.38 2 Samuel 7.27 2 Samuel 7.11 1 Samuel 25.28 Psaumes 18.50
36 Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali unitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate. 1 Rois 2.27 Malachie 1.13 Ezéchiel 44.10-44.12 1 Samuel 2.29-2.30

Cette Bible est dans le domaine public.