1 Njaa ikawa nzito katika nchi.
Genèse 42.5 Genèse 18.13 Lamentations 5.10 Genèse 41.54-41.57 Ecclésiaste 9.1-9.2
2 Ikawa walipokwisha kula nafaka waliyoileta kutoka Misri, baba yao akawaambia, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo.
Genèse 42.1-42.2 Proverbes 16.18 1 Timothée 5.8 1 Timothée 6.6-6.8 Proverbes 31.16
3 Yuda akamwambia akisema, Yule mtu alituagizia sana akisema, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi.
Genèse 44.23 Genèse 43.5 Genèse 42.15-42.20 Genèse 42.33-42.34 Actes 20.25
4 Ukimpeleka ndugu yetu pamoja nasi, tutashuka na kukununulia chakula.
5 Ila usipompeleka, hatushuki, maana mtu yule alituambia, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi.
Genèse 44.26 Genèse 42.38 Exode 20.12
6 Israeli akasema, Mbona mmenitendea vibaya hata mkamwarifu mtu yule ya kwamba mna ndugu mwingine?
7 Wakasema, Mtu yule alituhoji sana habari zetu na za jamaa yetu, akisema, Baba yenu angali hai? Mnaye ndugu mwingine? Nasi tukamjibu sawasawa na maswali hayo. Je! Tuliweza kujua ya kwamba atasema, Shukeni pamoja na ndugu yenu?
Genèse 43.3 Genèse 42.13 Genèse 43.27
8 Yuda akamwambia Israeli babaye, Mpeleke kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu.
Genèse 42.2 Genèse 45.19 Psaumes 118.17 Esdras 8.21 Nombres 14.31
9 Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima;
Genèse 42.37 Philémon 1.18-1.19 Hébreux 7.22 Genèse 44.32-44.33 1 Rois 1.21
10 maana kama hatungalikawia, hakika tungaliisha kurudi mara ya pili.
Genèse 19.16
11 Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.
Genèse 37.25 Jérémie 8.22 Ezéchiel 27.17 Proverbes 18.16 1 Rois 10.15
12 Mkatwae fedha maradufu mikononi mwenu, na fedha zile zilizorudishwa kinywani mwa magunia yenu zirudisheni mikononi mwenu; labda zilisahauliwa.
Genèse 42.25 Genèse 42.35 Romains 13.8 Philippiens 4.8 2 Corinthiens 8.21
13 Mtwaeni na ndugu yenu, mwondoke na kurudi kwa mtu yule.
Genèse 42.38
14 Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa.
Esther 4.16 Genèse 17.1 Psaumes 100.5 Proverbes 16.7 Psaumes 119.41
15 Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu.
16 Naye Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, Uwalete watu hawa nyumbani, ukachinje na kuandalia, maana watu hawa watakula pamoja nami adhuhuri.
Genèse 44.1 Genèse 43.19 1 Samuel 25.11 Genèse 39.4-39.5 Genèse 26.30
17 Yule mtu akafanya kama Yusufu alivyomwambia Naye akawaleta watu hao nyumbani mwa Yusufu.
18 Lakini watu hao wakaogopa kwa sababu wameletwa nyumbani mwa Yusufu, wakasema, Kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humu; apate kutushitaki, na kutuangukia, atutwae sisi kuwa watumwa, na punda zetu.
Genèse 42.35 Psaumes 53.5 Juges 14.4 Genèse 42.21 Job 15.21
19 Wakamkaribia yule msimamizi wa nyumba ya Yusufu, wakasema naye mlangoni pa nyumba.
20 Wakamwambia, Tazama, bwana, kweli tulishuka mara ya kwanza ili tununue chakula.
Genèse 42.3 Genèse 42.10 Genèse 42.35 Genèse 43.3 Genèse 42.27
21 Ikawa, tulipofika nyumba ya wageni, tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake, fedha zetu kwa uzani wake kamili; nasi tumezileta tena mikononi mwetu.
Genèse 43.12 1 Pierre 3.16 Romains 12.17 Genèse 42.27-42.35 1 Pierre 2.12
22 Nasi tumeleta fedha nyingine mikononi mwetu ili tununue chakula; hatujui ni nani aliyezitia fedha zetu katika magunia yetu.
23 Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia. Kisha akawatolea Simeoni.
Genèse 42.24 Jean 20.19 Jean 20.21 Luc 24.36 Jean 20.26
24 Mtu yule akawaleta wale watu nyumbani mwa Yusufu, akawapa maji, wakatawadha miguu, akawapa punda zao chakula.
Genèse 18.4 Genèse 24.32 Genèse 19.2 Luc 7.44 Jean 13.4-13.17
25 Wakaiweka tayari ile zawadi hata atakapokuja Yusufu adhuhuri, maana wamesikia ya kwamba watakula chakula huko.
Genèse 43.11 Genèse 43.16
26 Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka nchi.
Genèse 37.7-37.10 Genèse 42.6 Philippiens 2.10-2.11 Psaumes 72.9 Genèse 37.19-37.20
27 Akawaulizia hali yao, akasema, Je! Baba yenu, yule mzee mliyemnena, hajambo? Angali hai?
Genèse 42.11 Genèse 42.13 Exode 18.7 1 Samuel 17.22 Juges 18.15
28 Wakasema, Mtumwa wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.
Genèse 37.7 Genèse 43.26 2 Chroniques 24.17 2 Samuel 1.2 Exode 18.7
29 Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mamake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu.
Nombres 6.25 Genèse 42.13 Psaumes 67.1 1 Timothée 1.2 Genèse 30.22-30.24
30 Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo.
Genèse 42.24 1 Rois 3.26 Jérémie 31.20 Actes 20.31 Genèse 45.2
31 Akanawa uso, akatoka, akajizuia, akasema, Leteni chakula.
Genèse 45.1 Esaïe 42.14 Jérémie 31.16 1 Pierre 3.10
32 Wakamwandalia yeye peke yake, na wao peke yao, na wale Wamisri waliokula pamoja naye peke yao; maana Wamisri hawawezi kula pamoja na Waebrania, kwa kuwa ni chukizo kwa Wamisri.
Exode 8.26 Genèse 46.34 Genèse 31.54 Genèse 43.16
33 Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao.
34 Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye.
Genèse 45.22 2 Samuel 11.8 Habakuk 1.6 Proverbes 31.6 1 Samuel 9.22-9.24