Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 33
Bible en Swahili de l’est


1 Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Job 13.6 Psaumes 49.1-49.3 Job 34.2 Marc 4.9
2 Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Job 3.1 Matthieu 5.2 Job 31.30 Psaumes 78.2
3 Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu. Job 27.4 Proverbes 20.15 Job 36.3-36.4 Job 38.2 Proverbes 8.7-8.8
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Genèse 2.7 Job 32.8 Job 27.3 Job 10.12 Psaumes 33.6
5 Kwamba waweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame. Job 33.32-33.33 Job 32.12 Job 32.1 Psaumes 50.21 Job 23.4-23.5
6 Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo. Job 4.19 Genèse 3.19 Job 13.3 Job 20.22 Exode 4.16
7 Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito. Job 13.21 Job 9.34 Psaumes 88.16 Psaumes 32.4
8 Hakika umenena masikioni mwangu, Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema, Deutéronome 13.14 Jérémie 29.23
9 Mimi ni safi, sina makosa; Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu; Job 10.7 Job 16.17 Job 11.4 Job 9.21 Job 29.14
10 Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami, Hunihesabu kuwa ni adui yake; Job 13.24-13.25 Job 19.11 Job 14.16 Job 34.5 Job 10.15-10.17
11 Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza. Job 13.27 Job 31.4 Psaumes 105.18 Actes 16.24 Daniel 4.35
12 Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki; Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. Job 32.17 Job 34.23 Romains 9.19-9.21 Jérémie 18.6 Job 35.4
13 Nawe kwani kumnung’unikia, Kwa vile asivyotoa hesabu ya mambo yake yote? Job 40.2 Esaïe 45.9 Daniel 4.35 Ezéchiel 22.14 1 Corinthiens 10.22
14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Psaumes 62.11 Job 40.5 Marc 8.17-8.18 Proverbes 1.29 Luc 24.25
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Job 4.13 Nombres 12.6 Genèse 20.3 Daniel 8.18 Jérémie 23.28
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Job 36.15 Job 36.10 Esaïe 50.5 Psaumes 40.6 Romains 15.28
17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Jacques 4.10 Osée 2.6 Esaïe 2.11 Matthieu 27.19 2 Corinthiens 12.7
18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. 2 Pierre 3.9 Job 33.24 2 Pierre 3.15 Job 33.30 Job 33.22
19 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; Job 30.17 Job 5.17-5.18 1 Corinthiens 11.32 Psaumes 119.71 Psaumes 38.1-38.8
20 Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. Psaumes 107.17-107.18 Amos 5.11 Genèse 3.6 Job 3.24 Jérémie 3.19
21 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje. Job 19.20 Proverbes 5.11 Psaumes 32.3-32.4 Psaumes 22.15-22.17 Job 13.28
22 Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi. 2 Samuel 24.16 1 Samuel 2.6 Actes 12.23 Psaumes 30.3 Apocalypse 9.11
23 Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo; Malachie 3.1 Ecclésiaste 7.28 Job 34.10 Aggée 1.13 1 Corinthiens 11.30-11.32
24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi. Psaumes 49.7-49.8 Job 33.18 Exode 34.6-34.7 Esaïe 38.17-38.19 Psaumes 71.3
25 Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake; 2 Rois 5.14 Psaumes 103.5 Job 42.16 Josué 14.10-14.11 Osée 2.15
26 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake. Psaumes 50.15 Esaïe 30.19 Psaumes 30.5 Psaumes 116.1-116.6 Actes 9.11
27 Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo; Romains 6.21 2 Samuel 12.13 Psaumes 14.2 Romains 7.16 Jérémie 3.13
28 Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga. Job 33.22 Job 3.9 Job 33.24 Psaumes 49.19 Esaïe 38.17-38.18
29 Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu, Philippiens 2.13 Ephésiens 1.11 1 Corinthiens 12.6 2 Corinthiens 12.8 Job 33.14-33.17
30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai. Psaumes 56.13 Esaïe 38.17 Psaumes 118.17-118.18 Psaumes 40.1-40.2 Job 33.28
31 Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize; Nyamaza, mimi nitasema. Job 32.11 Job 21.2 Job 13.6 Job 18.2
32 Kama una neno la kusema, nijibu; Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki. Job 15.4-15.5 Job 22.5-22.9 Job 21.27 Job 27.5
33 Kama sivyo, unisikilize mimi; Nyamaza, nami nitakufunza hekima. Psaumes 34.11 Proverbes 8.5 Proverbes 4.1-4.2 Proverbes 5.1-5.2 Psaumes 49.3

Cette Bible est dans le domaine public.