31 Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho; 1 Rois 7.49 Zacharie 4.2 Exode 37.17-37.24 Apocalypse 1.12 Hébreux 9.2 32 nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake; matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili 33 vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja; tovu na ua; na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua; vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara; Jérémie 1.11-1.12 Nombres 17.4-17.8 Exode 37.19-37.20 Zacharie 4.3 34 na katika hicho kinara vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake; 35 na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara. 36 Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho; kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi. Nombres 8.4 1 Rois 10.16-10.17 2 Chroniques 9.15 Exode 25.18 37 Nawe zifanye taa zake saba; nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake. Nombres 8.2 2 Chroniques 13.11 Exode 27.21 Lévitique 24.2-24.4 Exode 37.23 38 Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi. Esaïe 6.6 Nombres 4.9 Jérémie 52.18 1 Rois 7.50 Exode 37.23 39 Kitafanywa cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote. 40 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, ulioonyeshwa mlimani. Exode 26.30 Hébreux 8.5 Nombres 8.4 Actes 7.44 1 Chroniques 28.11