Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 26.59
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa baada ya hilo pigo, Bwana akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia,Nombres 25.9
2 Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani.Exode 38.25-38.26 Nombres 1.2-1.3 Exode 30.11-30.16
3 Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia,Nombres 22.1 Nombres 33.48 Nombres 35.1 Nombres 26.63 Deutéronome 34.8
4 Fanyeni jumla ya watu, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama Bwana alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri.Nombres 1.1 1 Chroniques 21.1
5 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu;1 Chroniques 5.3 Genèse 46.8-46.9 Exode 6.14 1 Chroniques 5.1 Genèse 29.32
6 na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. 7 Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini.Nombres 1.21 Nombres 26.1 Nombres 2.11 Nombres 26.21 Genèse 46.9
8 Na wana wa Palu; Eliabu. 9 Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na Bwana;Nombres 1.16 Psaumes 106.17 Jude 1.11 Nombres 16.1-16.35
10 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.Nombres 16.38 Nombres 16.31-16.35 2 Pierre 2.6 Nombres 27.3 Jude 1.7
11 Pamoja na hayo, hao wana wa Kora hawakufa.Exode 6.24 Psaumes 48.1 Psaumes 45.1 Psaumes 47.1 Nombres 16.5
12 Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini;1 Chroniques 4.24 Exode 6.15 Genèse 46.10 1 Rois 7.21
13 wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli.Genèse 46.10
14 Hizi ndizo jamaa za Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili.Nombres 2.12-2.13 Nombres 1.22-1.23
15 Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni;Genèse 46.16 Nombres 2.14
16 wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri;Genèse 46.16
17 wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli.Genèse 46.16
18 Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano.Nombres 2.14-2.15 Nombres 1.24-1.25
19 Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani.Genèse 46.12 Genèse 38.1-38.10 1 Chroniques 2.3-2.8
20 Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.Genèse 46.12 Néhémie 11.24 1 Chroniques 4.21 Matthieu 1.3 1 Chroniques 2.3-2.8
21 Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. 22 Hizi ndizo jamaa za Yuda kama waliohesabiwa kwao, sabini na sita elfu na mia tano.Nombres 1.26-1.27 Nombres 2.3-2.4 1 Chroniques 5.2 Psaumes 115.14 Hébreux 7.14
23 Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva;Genèse 46.13 1 Chroniques 7.1 Nombres 2.5 Genèse 30.17-30.18
24 wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni.Genèse 46.13
25 Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu.Nombres 2.5-2.6 Nombres 1.28-1.29
26 Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli.Genèse 46.14 Genèse 30.19-30.20
27 Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano.Nombres 1.30-1.31 Nombres 2.7-2.8
28 Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu.Genèse 46.20 Genèse 48.13-48.20 Genèse 48.5 Genèse 41.51-41.52
29 Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi.Josué 17.1 Nombres 36.1 1 Chroniques 7.14-7.19 Genèse 48.14 Juges 5.14
30 Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki;Juges 6.11 Josué 17.2 Juges 6.34 Juges 6.24 Juges 8.2
31 na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; 32 na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. 33 Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na wana waume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa.Nombres 27.1 Nombres 36.10-36.12
34 Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba.Nombres 2.20-2.21 Nombres 1.34-1.35
35 Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi.1 Chroniques 7.20-7.21
36 Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. 37 Hizi ndizo jamaa za wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, thelathini na mbili elfu na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao.Nombres 1.32-1.33 Nombres 2.18-2.19
38 Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu;1 Chroniques 8.1 1 Chroniques 7.6-7.12 Genèse 46.2 Genèse 46.21
39 wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu.Genèse 46.21
40 Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani.1 Chroniques 8.3
41 Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita.Nombres 1.36-1.37 Nombres 2.22-2.23 Genèse 46.21
42 Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao.Genèse 46.23
43 Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na nne elfu na mia nne.Nombres 1.38-1.39 Nombres 2.25-2.26
44 Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia.1 Chroniques 7.30 Genèse 46.17
45 Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. 46 Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera.Genèse 46.17
47 Hizi ndizo jamaa za wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, hamsini na tatu elfu na mia nne.Nombres 1.40-1.41 Nombres 2.27-2.28
48 Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni;1 Chroniques 7.13 Genèse 46.24
49 wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu.1 Chroniques 7.13
50 Hizi ndizo jamaa za Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia nne.Nombres 1.42-1.43 Nombres 2.29-2.30
51 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, mia sita na moja elfu, na mia saba na thelathini (601,730).Nombres 1.46 Néhémie 9.23 Job 12.9-12.10 Exode 12.37 Nombres 2.32
52 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 53 Watu hawa watagawanyiwa nchi hiyo iwe urithi wao, vile vile kama hesabu ya majina yao ilivyo.Josué 14.1 Josué 11.23 Psaumes 105.44 Genèse 12.7 Apocalypse 21.27
54 Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake.Nombres 33.54 Nombres 32.5 Nombres 32.3 Josué 17.14
55 Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya kabila za baba zao, ndivyo watakavyopata urithi.Nombres 34.13 Nombres 33.54 Josué 11.23 Josué 14.2 Apocalypse 7.4-7.8
56 Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache.Romains 11.7 1 Corinthiens 12.4
57 Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari.Genèse 46.11 Exode 6.16-6.19 1 Chroniques 6.1 1 Chroniques 6.16-6.30 Nombres 35.2-35.3
58 Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu.Nombres 3.17-3.21 Exode 6.20 Nombres 16.1
59 Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.Exode 6.20 Exode 2.1-2.2 Lévitique 18.12
60 Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.Nombres 3.2 Nombres 3.8
61 Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za Bwana.Lévitique 10.1-10.2 Nombres 3.4 1 Chroniques 24.1-24.2
62 Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa ishirini na tatu elfu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.Deutéronome 10.9 Nombres 35.2-35.8 Nombres 1.49 Nombres 3.39 Josué 13.14
63 Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.Nombres 26.3
64 Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai.Deutéronome 2.14-2.15 Hébreux 3.17 Nombres 14.29 1 Corinthiens 10.5 Deutéronome 4.3-4.4
65 Kwa kuwa Bwana alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.Nombres 14.38 Nombres 14.28-14.30 Nombres 14.35 Psaumes 90.3-90.7 Deutéronome 32.49-32.50

Cette Bible est dans le domaine public.