Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 21
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema. Genèse 18.10 Genèse 18.14 Galates 4.23 1 Samuel 2.21 Genèse 17.19
2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Hébreux 11.11 Galates 4.22 Genèse 17.21 Genèse 18.10 Genèse 18.14
3 Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia. Genèse 17.19 Matthieu 1.2 Romains 9.7 Josué 24.3 Hébreux 11.18
4 Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru. Actes 7.8 Lévitique 12.3 Deutéronome 12.32 Exode 12.48 Jean 7.22-7.23
5 Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka. Genèse 17.17 Romains 4.19 Genèse 17.1
6 Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. Esaïe 54.1 Genèse 18.12-18.15 Psaumes 126.2 Genèse 17.17 Luc 1.14
7 Akasema, N’nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake. Genèse 18.11-18.12 Ephésiens 3.10 Psaumes 86.10 Psaumes 86.8 Deutéronome 4.32-4.34
8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. Genèse 29.22 Genèse 40.20 1 Rois 3.15 1 Samuel 1.22 Juges 14.12
9 Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Genèse 16.15 Galates 4.29 Genèse 16.1 Psaumes 44.13-44.14 2 Rois 2.23-2.24
10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Jean 8.35 1 Jean 2.19 Genèse 36.6-36.7 Genèse 17.21 Matthieu 22.13
11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Genèse 17.18 Hébreux 12.11 2 Samuel 18.33 Genèse 22.1-22.2 Matthieu 10.37
12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Hébreux 11.18 Genèse 17.19 1 Samuel 8.7 Genèse 17.21 1 Samuel 8.9
13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. Genèse 21.18 Genèse 16.10 Genèse 17.20 Genèse 25.12-25.18
14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Genèse 26.33 Ecclésiaste 9.10 Esaïe 16.8 Genèse 22.19 Genèse 37.15
15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. 2 Rois 3.9 Psaumes 63.1 Exode 15.22-15.25 Jérémie 14.3 Exode 17.1-17.3
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. 1 Samuel 30.4 Genèse 27.38 Zacharie 12.10 1 Rois 3.26 Juges 2.4
17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Genèse 16.11 Exode 3.7 Genèse 16.9 Exode 22.23 Genèse 15.1
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. Genèse 21.13 Genèse 16.10 Genèse 17.20 Genèse 25.12-25.18 1 Chroniques 1.29-1.31
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Nombres 22.31 Esaïe 35.5-35.6 2 Rois 6.17-6.20 Luc 24.16-24.31
20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde. Genèse 39.21 Genèse 28.15 Genèse 39.2-39.3 Genèse 16.12 Juges 13.24-13.25
21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri. 1 Samuel 25.1 Nombres 13.26 Nombres 13.3 Genèse 26.34-26.35 Genèse 24.3-24.4
22 Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Ibrahimu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda. Genèse 26.28 Genèse 26.26 Genèse 20.2 Esaïe 8.10 Hébreux 13.5
23 Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake. Josué 2.12 Genèse 20.14 1 Samuel 20.13 Deutéronome 6.13 1 Samuel 30.15
24 Ibrahimu akasema, Nitaapa. Romains 12.18 Genèse 14.13 Hébreux 6.16
25 Kisha Ibrahimu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumwa wa Abimeleki wamekinyang’anya. Genèse 26.15-26.22 Genèse 29.8 Genèse 13.7 Juges 1.15 Exode 2.15-2.17
26 Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu. Genèse 13.7 2 Rois 5.20-5.24
27 Ibrahimu akatwaa kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano. Proverbes 21.14 Proverbes 18.24 Genèse 26.28-26.31 1 Samuel 18.3 Esaïe 32.8
28 Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao. 29 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini? 1 Samuel 15.14 Genèse 33.8 Exode 12.26
30 Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki. Genèse 31.52 Josué 22.27-22.28 Genèse 31.44-31.48 Josué 24.27
31 Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili. Genèse 26.33 Genèse 21.14 Juges 20.1 Genèse 26.23 Josué 15.28
32 Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti. Exode 13.17 Juges 13.1 Genèse 14.13 Genèse 26.14 Genèse 31.53
33 Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele. Psaumes 90.2 Esaïe 40.28 Genèse 4.26 Genèse 12.8 Deutéronome 33.27
34 Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi. Hébreux 11.13 Psaumes 39.12 1 Chroniques 29.15 Hébreux 11.9 1 Pierre 2.11

Cette Bible est dans le domaine public.