Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 69
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Psaumes 69.14-69.15 Psaumes 42.7 Psaumes 45.1 Esaïe 43.2 Apocalypse 17.15
2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. Psaumes 40.2 Psaumes 88.6-88.7 Genèse 7.17-7.23 Jérémie 38.6 Matthieu 26.37-26.38
3 Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu. Psaumes 6.6 Esaïe 38.14 Psaumes 119.82 Psaumes 119.123 Deutéronome 28.32
4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. Psaumes 35.19 Jean 15.25 Psaumes 40.12 Esaïe 53.4-53.7 Psaumes 59.3
5 Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu. Jérémie 16.17 Psaumes 17.3 Psaumes 38.5 Psaumes 44.20-44.21 Psaumes 38.9
6 Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Psaumes 72.18 Psaumes 7.7 Psaumes 25.3 Actes 13.23 Actes 13.17
7 Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Jérémie 15.15 Psaumes 44.22 Esaïe 50.6 Matthieu 26.67-26.68 Matthieu 27.29-27.30
8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu. Psaumes 31.11 Psaumes 38.11 Jean 1.11 Matthieu 10.35-10.36 Matthieu 26.48-26.50
9 Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. Romains 15.3 Psaumes 119.139 Jean 2.14-2.17 Psaumes 89.50-89.51 1 Chroniques 15.27-15.29
10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. Psaumes 35.13 Luc 7.33-7.34 Psaumes 102.8-102.9 Psaumes 109.24-109.25
11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. Jérémie 24.9 1 Rois 9.7 Job 17.6 Deutéronome 28.37 Joël 1.8
12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. Matthieu 27.20 Actes 4.26-4.27 Genèse 19.1 Matthieu 27.12-27.13 Deutéronome 16.18
13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Esaïe 49.8 2 Corinthiens 6.2 Luc 22.44 1 Samuel 25.8 Psaumes 32.6
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji. Psaumes 144.7 Psaumes 69.1-69.2 Psaumes 109.21 Psaumes 42.7 Luc 19.14
15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu. Jonas 2.2-2.7 Nombres 16.33-16.34 Esaïe 43.1-43.2 Apocalypse 12.15-12.16 Matthieu 12.40
16 Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee. Psaumes 63.3 Psaumes 25.16 Psaumes 109.21 Psaumes 51.1 Esaïe 63.7
17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi. Psaumes 27.9 Psaumes 102.2 Psaumes 44.24 Psaumes 40.13 Job 7.21
18 Uikaribie nafsi yangu, uikomboe, Kwa sababu ya adui zangu unifidie. Psaumes 31.5 Psaumes 22.19 Josué 7.9 Psaumes 10.1 Psaumes 22.1
19 Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. Hébreux 12.2 Jean 8.49 Psaumes 69.7-69.9 Psaumes 22.6-22.7 Psaumes 38.9
20 Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu. Job 16.2 Esaïe 63.5 Psaumes 142.4 Marc 14.50 Jean 16.32
21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki. Marc 15.23 Matthieu 27.34 Luc 23.36 Matthieu 27.48 Marc 15.36
22 Meza yao mbele yao na iwe mtego; Naam, wakiwa salama na iwe tanzi. Romains 11.8-11.10 Proverbes 1.32 Esaïe 8.14-8.15 1 Pierre 2.8 1 Thessaloniciens 5.3
23 Macho yao yatiwe giza wasione, Na viuno vyao uvitetemeshe daima. Daniel 5.6 Jérémie 30.6 Romains 11.10 Esaïe 6.9-6.10 Deutéronome 28.65-28.67
24 Uimwage ghadhabu yako juu yao, Na ukali wa hasira yako uwapate. Psaumes 79.6 Osée 5.10 Deutéronome 31.17 Esaïe 13.8 Luc 21.22
25 Matuo yao na yawe ukiwa, Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao. Matthieu 23.38 Actes 1.20 Matthieu 24.1-24.2 1 Rois 9.8 Esaïe 5.1
26 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe, Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha. Esaïe 53.4 Zacharie 1.15 Esaïe 53.10 2 Chroniques 28.9 Zacharie 13.7
27 Uwaongezee uovu juu ya uovu, Wala wasiingie katika haki yako. Esaïe 26.10 Néhémie 4.5 Romains 1.28 Matthieu 23.31-23.32 Romains 9.31
28 Na wafutwe katika chuo cha uhai, Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe. Luc 10.20 Philippiens 4.3 Apocalypse 3.5 Hébreux 12.23 Exode 32.32-32.33
29 Nami niliye maskini na mtu wa huzuni, Mungu, wokovu wako utaniinua. Psaumes 40.17 Matthieu 8.20 Psaumes 22.27-22.31 Ephésiens 1.21-1.22 Psaumes 59.1
30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani. Psaumes 28.7 Psaumes 34.3 Psaumes 40.1-40.3 Psaumes 118.28-118.29 Psaumes 50.14
31 Nayo yatampendeza Bwana kuliko ng’ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato. Psaumes 50.13-50.14 Psaumes 50.23 1 Pierre 2.5 Osée 14.2 Ephésiens 5.19-5.20
32 Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe. Psaumes 34.2 Psaumes 22.26 Psaumes 25.9 Esaïe 55.6-55.7 Jean 20.20
33 Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake. Psaumes 68.6 Ephésiens 3.1 Luc 4.18 Apocalypse 2.10 Psaumes 10.17
34 Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake. Esaïe 49.13 Psaumes 96.11 Esaïe 55.12 Psaumes 150.6 Psaumes 98.7-98.8
35 Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki. Psaumes 51.18 Esaïe 44.26 Esaïe 46.13 Psaumes 147.12-147.13 Psaumes 48.11-48.13
36 Wazao wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo. Psaumes 102.28 Psaumes 37.29 Psaumes 91.14 Jean 14.23 Actes 2.39

Cette Bible est dans le domaine public.