Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 4.20
Bible en Swahili de l’est


1 Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema Bwana, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa;Joël 2.12 Jérémie 3.22 Jérémie 3.1 Genèse 35.2 Ephésiens 4.22-4.31
2 nawe utaapa hivi, Kama Bwana aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watajibariki katika yeye, nao watajitukuza katika yeye.Esaïe 65.16 Jérémie 9.24 Deutéronome 10.20 1 Corinthiens 1.31 Galates 3.8
3 Maana Bwana awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba.Osée 10.12 Luc 8.14 Matthieu 13.7 Marc 4.7 Matthieu 13.22
4 Jitahirini kwa Bwana, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.Deutéronome 10.16 Romains 2.28-2.29 Jérémie 9.26 Deutéronome 30.6 Colossiens 2.11
5 Tangazeni katika Yuda, hubirini katika Yerusalemu, na kusema, Pigeni baragumu katika nchi, pigeni kelele sana, na kusema, Jikusanyeni pamoja, tukaingie katika miji yenye boma.Jérémie 8.14 Josué 10.20 Jérémie 6.1 Osée 8.1 Ezéchiel 33.2-33.6
6 Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamivu makuu.Jérémie 50.2 Jérémie 1.13-1.15 Jérémie 51.27 Jérémie 6.22 Jérémie 6.1
7 Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa; ameanza kushika njia, ametoka katika mahali pake; ili aifanye nchi yako kuwa ukiwa, miji yako ifanywe maganjo, asibaki mwenyeji ndani yake.Jérémie 5.6 Jérémie 2.15 Esaïe 1.7 Jérémie 25.9 Esaïe 6.11
8 Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha.Jérémie 6.26 Esaïe 22.12 Esaïe 10.4 Esaïe 32.11 Esaïe 5.25
9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema Bwana, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.Esaïe 22.3-22.5 Ezéchiel 13.9-13.16 Esaïe 29.9-29.10 Esaïe 19.16 Psaumes 102.4
10 Nami nikasema, Aa, Bwana MUNGU! Hakika umewadanganya sana watu hawa na Yerusalemu, ukisema, Mtakuwa na amani lakini upanga umeingia katika nafsi za watu.Jérémie 5.12 Esaïe 63.17 Jérémie 23.17 2 Thessaloniciens 2.9-2.12 1 Rois 22.20-22.23
11 Wakati ule watu hawa na Yerusalemu wataambiwa neno hili, Upepo wa moto utokao katika vilele vya nyikani visivyo na miti, ukimwelekea binti ya watu wangu, hauwi upepo wa kupepeta, wala upepo wa kutakasa;Ezéchiel 17.10 Osée 13.15 Jérémie 30.23-30.24 Osée 13.3 Lamentations 2.11
12 ni upepo wa nguvu kuliko hizo utakaokuja kwa ajili yangu; sasa mimi nitatoa hukumu juu yao.Jérémie 1.16 Ezéchiel 7.8-7.9 Ezéchiel 6.11-6.13 Ezéchiel 5.8
13 Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi zake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika.Esaïe 5.28 Esaïe 66.15 Lamentations 4.19 Esaïe 19.1 Habakuk 1.8
14 Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?Jacques 4.8 Esaïe 55.7 Proverbes 1.22 Actes 8.22 Jérémie 13.27
15 Maana sauti yatangaza habari toka Dani, yahubiri uovu toka vilima vya Efraimu;Jérémie 8.16 Juges 18.29 Josué 17.15 Jérémie 6.1 Josué 20.7
16 Wapasheni mataifa habari; angalieni, hubirini juu ya Yerusalemu, ya kwamba walinzi wanatoka katika nchi ya mbali, wanatoa sauti yao juu ya miji ya Yuda.Ezéchiel 21.22 Jérémie 5.15 Esaïe 39.3 Jérémie 2.15 Jérémie 6.18
17 Kama watu walindao shamba, wameuzunguka wauhusuru; kwa sababu ameniasi mimi, asema Bwana.Jérémie 5.23 2 Rois 25.1-25.4 Lamentations 1.18 Luc 19.43-19.44 Daniel 9.7-9.19
18 Njia yako na matendo yako yamekupatia haya; huu ndio uovu wako; kwa maana ni uchungu, hakika unafikilia hata moyo wako.Jérémie 2.19 Jérémie 2.17 Esaïe 50.1 Psaumes 107.17 Proverbes 1.31
19 Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.Esaïe 16.11 Esaïe 22.4 Jérémie 9.10 Habakuk 3.16 Jérémie 9.1
20 Uangamivu baada ya uangamivu umetangazwa; kwa maana nchi yote imeharibika; hema zangu zimetekwa nyara ghafula, na mapazia yangu katika dakika moja.Psaumes 42.7 Jérémie 10.19-10.20 Nombres 16.21 Esaïe 54.2 Joël 1.15
21 Niione bendera hata lini, na kuisikia sauti ya tarumbeta?2 Chroniques 36.3 2 Chroniques 35.25 2 Chroniques 36.17 2 Chroniques 36.6-36.7 Jérémie 4.19
22 Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.Romains 16.19 1 Corinthiens 14.20 Jérémie 5.21 Romains 3.11 Osée 4.6
23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.Marc 13.24-13.25 Matthieu 24.29 Genèse 1.2 Luc 21.25-21.26 Esaïe 13.10
24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko.Ezéchiel 38.20 Esaïe 5.25 Jérémie 10.10 Psaumes 114.4-114.7 Habakuk 3.6
25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.Jérémie 9.10 Jérémie 12.4 Sophonie 1.2-1.3 Osée 4.3
26 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali.Psaumes 107.34 Esaïe 7.20-7.25 Esaïe 5.9-5.10 Jérémie 12.4 Michée 3.12
27 Maana Bwana asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini sitaikomesha kabisa.Jérémie 30.11 Jérémie 5.18 Jérémie 46.28 Jérémie 5.10 Romains 9.27-9.29
28 Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache.Osée 4.3 Nombres 23.19 Jérémie 12.4 Esaïe 50.3 Esaïe 5.30
29 Mji mzima unakimbia, kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi na wenye pinde wanaingia vichakani, wanapanda juu ya majabali; kila mji umeachwa, hapana hata mtu mmoja akaaye ndani yake.Jérémie 4.7 Esaïe 2.19-2.21 Apocalypse 6.15-6.17 Jérémie 52.7 Luc 23.30
30 Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.2 Rois 9.30 Lamentations 1.2 Esaïe 10.3 Lamentations 1.19 Esaïe 20.6
31 Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa utungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.Lamentations 1.17 Esaïe 1.15 Jérémie 13.21 Esaïe 13.8 1 Corinthiens 9.16

Cette Bible est dans le domaine public.