Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 10.14
Bible en Swahili de l’est


1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,Actes 8.40 Actes 27.1 Jean 18.3 Actes 25.13 Actes 23.33
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.Actes 10.22 Actes 13.16 Actes 13.26 Actes 10.35 Actes 10.7
3 Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!Actes 3.1 Actes 5.19 Actes 9.4 Job 4.15-4.16 Actes 10.19
4 Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.Hébreux 6.10 Actes 10.31 Luc 1.12-1.13 Actes 9.5-9.6 Malachie 3.16
5 Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro.Actes 15.7 Actes 9.36 Jean 1.42 Actes 10.32 Actes 9.38
6 Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.Actes 9.43 Ephésiens 4.8-4.12 Jean 7.17 Romains 10.14-10.17 Actes 11.13-11.14
7 Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa katika wale waliomhudumia daima;Genèse 24.52 Juges 7.10 Genèse 24.1-24.10 1 Samuel 14.6-14.7 Philémon 1.16
8 na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yafa.Ecclésiaste 9.10 Actes 9.36 Galates 1.16 Actes 26.19 Psaumes 119.59-119.60
9 Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;Psaumes 55.17 Sophonie 1.5 1 Samuel 9.25 Matthieu 20.5 Jérémie 32.29
10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,Actes 22.17 Matthieu 12.1-12.3 Ezéchiel 40.2 Apocalypse 1.10 Nombres 24.16
11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;Jean 1.51 Romains 16.25-16.26 Romains 9.4 Matthieu 8.11 Actes 7.56
12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.1 Corinthiens 6.9-6.11 Jean 7.37 Esaïe 65.25 Genèse 7.8-7.9 Esaïe 11.6-11.9
13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.Actes 10.10 Jérémie 35.2-35.5 Jean 4.31-4.34
14 Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.Ezéchiel 4.14 Lévitique 20.25 Deutéronome 14.1-14.29 Luc 1.60 Matthieu 16.22
15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.Tite 1.15 Matthieu 15.11 1 Corinthiens 10.25 Romains 14.14 1 Timothée 4.3-4.5
16 Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.Genèse 41.32 Jean 21.17 2 Corinthiens 13.1
17 Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,Actes 10.3 Actes 10.7-10.19 Actes 5.24 Actes 25.20 Actes 2.12
18 wakaita; wakauliza kwamba Simoni aitwaye Petro anakaa humo.Actes 11.11 Actes 10.5-10.6
19 Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.Actes 8.29 Actes 21.4 Actes 13.2 1 Timothée 4.1 1 Corinthiens 12.11
20 Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma.Actes 15.7-15.9 Esaïe 48.16 Actes 9.15 Marc 16.15 Zacharie 2.9-2.11
21 Petro akawashukia wale watu, akanena, Mimi ndiye mnayemtafuta. Mmekuja kwa sababu gani?Jean 1.38-1.39 Marc 10.51 Jean 18.4-18.8 Actes 10.29
22 Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno kwako.Actes 11.14 Actes 10.2 3 Jean 1.12 Romains 10.17-10.18 Luc 7.4-7.5
23 Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.Actes 11.12 Actes 10.45 Actes 9.38 Genèse 24.31-24.32 Ecclésiaste 9.10
24 Siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, hali amekusanya jamaa zake na rafiki zake.Zacharie 3.10 Jean 4.28-4.29 Luc 5.29 Jean 1.41-1.49 Zacharie 8.20-8.23
25 Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia.Matthieu 8.2 Apocalypse 19.10 Daniel 2.46 Apocalypse 22.8-22.9 Daniel 2.30
26 Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu.Apocalypse 19.10 Apocalypse 22.8-22.9 Apocalypse 13.8 Esaïe 48.13 Matthieu 4.10
27 Na katika kusema naye akaingia ndani, akaona watu wengi wamekusanyika.2 Corinthiens 2.12 Actes 10.24 Jean 4.35 Actes 14.27 1 Corinthiens 16.9
28 Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.Jean 4.9 Jean 18.28 Galates 2.12-2.14 Actes 10.34-10.35 Jean 4.27
29 Kwa sababu hiyo nalikuja nilipoitwa, nisikatae; basi nawauliza, ni neno gani mliloniitia?1 Pierre 3.15 Actes 10.19-10.20 Psaumes 119.60
30 Kornelio akasema, Siku tatu zilizopita, katika saa ii hii, yaani saa tisa, nilikuwa nikisali nyumbani mwangu; nikamwona mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zing’arazo,Actes 10.3 Actes 10.23-10.24 Actes 1.10 Luc 24.4 Actes 3.1
31 akasema, Kornelio, kuomba kwako kumesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.Actes 10.4 Lévitique 2.2 Hébreux 6.10 Apocalypse 5.8 Lévitique 2.9
32 Basi, tuma watu kwenda Yafa, ukamwite Simoni aitwaye Petro, anakaa katika nyumba ya Simoni, mtengenezaji wa ngozi, karibu na pwani; naye akija atasema nawe. 33 Mara nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Basi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Bwana.Galates 4.14 Actes 28.28 Actes 17.11-17.12 Jacques 1.19 1 Thessaloniciens 2.13
34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;2 Chroniques 19.7 Romains 2.11 Colossiens 3.25 Deutéronome 10.17 1 Pierre 1.17
35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.Actes 10.2 Actes 15.9 1 Jean 2.29 2 Corinthiens 7.1 Hébreux 11.4-11.6
36 Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),Matthieu 28.18 Actes 2.36 Apocalypse 17.14 Apocalypse 19.16 Jérémie 23.5-23.6
37 jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana;Marc 1.14-1.15 Matthieu 3.1-3.3 Actes 2.22 Jean 4.1-4.3 Luc 23.5
38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.Actes 2.22 Jean 3.2 Luc 4.18 Jean 3.34 Esaïe 61.1-61.3
39 Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini.Luc 24.48 Actes 10.41 Actes 1.8 Actes 2.32 Actes 2.23-2.24
40 Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika,Actes 2.24 Romains 6.4-6.11 2 Corinthiens 4.14 Matthieu 28.1-28.2 Romains 14.9
41 si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.Jean 14.22 Actes 10.39 Jean 21.13 Jean 14.17 Jean 15.16
42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu.1 Pierre 4.5 2 Timothée 4.1 Actes 17.31 Romains 14.9-14.10 2 Corinthiens 5.10
43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.Esaïe 53.11 Jean 5.24 Jérémie 31.34 Actes 15.9 Romains 10.11
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.Actes 11.15 Actes 15.8 Actes 19.6 Actes 4.31 Actes 2.2-2.4
45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.Actes 10.23 Actes 2.38 Ephésiens 2.11 Actes 11.15-11.18 Galates 2.15
46 Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,Actes 19.6 Actes 2.4 Marc 16.17 Actes 2.11 1 Corinthiens 14.20-14.25
47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?Actes 8.36 Actes 15.8-15.9 Romains 10.12 Actes 11.15-11.17 Actes 2.4
48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.Actes 2.38 Actes 8.16 1 Corinthiens 1.13-1.17 Galates 3.27 Actes 16.15

Cette Bible est dans le domaine public.