Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 17
Bible en Swahili de l’est


1 Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi. Philippiens 4.16 1 Thessaloniciens 1.1 2 Timothée 4.10 2 Thessaloniciens 1.1 Actes 20.4
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, Actes 9.20 Actes 8.35 Actes 13.5 Luc 4.16 Actes 17.10
3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Actes 9.22 Actes 18.28 Luc 24.46 Luc 24.32 Actes 3.18
4 Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Actes 17.12 Actes 15.22 Actes 14.4 Actes 13.43 Actes 13.50
5 Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; Romains 16.21 Actes 17.13 Juges 9.4 Actes 17.7 Actes 19.40
6 na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, Actes 24.5 Actes 28.22 Luc 23.5 Exode 3.8-3.9 Actes 21.28-21.31
7 na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Luc 23.2 Actes 16.21 Jean 19.12 Actes 25.8-25.11 Daniel 3.12
8 Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. Jean 11.48 Matthieu 2.3
9 Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao. Actes 17.5
10 Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Actes 20.4 Actes 17.13-17.14 Actes 17.2 Actes 9.25 1 Samuel 20.42
11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Jean 5.39 1 Thessaloniciens 2.13 Esaïe 34.16 2 Pierre 1.19-1.21 2 Timothée 3.15-3.17
12 Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache. Actes 13.50 Jacques 1.21 Jacques 1.10 Actes 13.46 Jean 1.45-1.49
13 Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano. Luc 12.51 1 Thessaloniciens 2.14-2.16 Matthieu 23.13 1 Rois 21.25 Actes 6.12
14 Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko. Actes 17.10 Matthieu 10.23 Actes 16.1 Actes 20.3 Actes 19.22
15 Lakini wale waliomsindikiza Paulo wakampeleka mpaka Athene; nao wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kwamba wasikawie kumfuata, wakaenda zao. Actes 18.1 1 Thessaloniciens 3.1 Actes 18.5 Actes 17.21 2 Timothée 4.20-4.21
16 Paulo alipokuwa akiwangojea huko Athene na kuona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake. Actes 17.23 Exode 32.19-32.20 Jean 2.13 Job 32.2-32.3 Psaumes 69.9
17 Basi katika sinagogi akahojiana na Wayahudi na waliomcha Mungu, na wale waliokutana naye sokoni kila siku. Proverbes 1.20-1.22 Marc 16.15 Jérémie 6.11 Proverbes 8.1-8.4 Actes 8.2
18 Na baadhi ya Waepikureo na Wastoiko, wenye ujuzi, wakakutana naye. Wengine wakasema, Mpuzi huyu anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza habari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akihubiri habari za Yesu na ufufuo. Actes 4.2 Actes 6.9 Marc 9.14 Proverbes 26.12 1 Corinthiens 15.3-15.4
19 Wakamshika, wakamchukua Areopago, wakisema, Je! Twaweza kujua maana ya elimu hii mpya unayoinena? Marc 1.27 Actes 17.22 Actes 26.1 1 Jean 2.7-2.8 Actes 17.20
20 Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, basi, maana ya mambo haya. 1 Pierre 4.4 Osée 8.12 Actes 2.12 Actes 10.17 1 Corinthiens 1.23
21 Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya. 2 Timothée 2.16-2.17 Colossiens 4.5 1 Timothée 5.13 Ephésiens 5.16 2 Thessaloniciens 3.11-3.12
22 Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini. Actes 25.19 Actes 17.16 Actes 19.35 Jérémie 10.2-10.3 Jérémie 50.38
23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Jean 4.22 Actes 17.30 1 Jean 5.20 2 Thessaloniciens 2.4 Jean 17.3
24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; 1 Rois 8.27 Deutéronome 10.14 Actes 7.48 Matthieu 11.25 Psaumes 115.16
25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. Job 22.2 Psaumes 50.8-50.13 Job 33.4 Esaïe 42.5 Romains 11.35
26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; 1 Corinthiens 15.47 1 Corinthiens 15.22 Malachie 2.10 Genèse 3.20 Deutéronome 32.7-32.8
27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Actes 14.17 Romains 1.20 Jérémie 23.23-23.24 Deutéronome 4.7 Actes 15.17
28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Job 12.10 Hébreux 1.3 Colossiens 1.17 Jean 5.26 Psaumes 36.9
29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu. Psaumes 106.20 Exode 20.4 Habakuk 2.19-2.20 Romains 1.20-1.23 Psaumes 94.7-94.9
30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Luc 24.47 Actes 14.16 Tite 2.11-2.12 1 Pierre 4.3 Romains 3.25
31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu. 2 Pierre 3.7 Matthieu 25.31-25.46 Psaumes 98.9 Romains 2.16 Psaumes 96.13
32 Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo. Actes 17.18 Actes 2.13 Actes 24.25 Actes 26.8 Hébreux 3.7-3.8
33 Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha. 34 Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao. Actes 17.19 Esaïe 55.10-55.11 Jean 19.38-19.42 Actes 13.48 Romains 11.5-11.6

Cette Bible est dans le domaine public.