Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lévitique 19
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akanena na Musa, akamwambia, 2 Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu. Lévitique 20.26 Lévitique 11.44-11.45 1 Pierre 1.15-1.16 Lévitique 20.7 Matthieu 5.48
3 Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Exode 20.8 Exode 20.12 Exode 21.17 Exode 16.29 Exode 21.15
4 Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Lévitique 26.1 Exode 20.23 Exode 34.17 Exode 20.3-20.5 Deutéronome 27.15
5 Nanyi hapo mtakapomchinjia Bwana sadaka ya amani mtaisongeza ili kwamba mpate kukubaliwa. Lévitique 22.19 Lévitique 7.16 Lévitique 1.3 Lévitique 22.21 2 Chroniques 31.2
6 Italiwa siku iyo hiyo mliyoichinja, na siku ya pili yake; na kama kitu cho chote katika sadaka hiyo kilisalia hata siku ya tatu kitachomwa moto. Lévitique 7.11-7.17
7 Kwamba sadaka hiyo yaliwa hata kidogo siku ya tatu ni machukizo; haitakubaliwa; Lévitique 7.18-7.21 Esaïe 65.4 Jérémie 16.18 Lévitique 22.23 Esaïe 1.13
8 lakini kila mtu atakayekula atauchukua uovu wake mwenyewe, kwa sababu amekinajisi kitu hicho kitakatifu cha Bwana; na nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. Lévitique 5.1 Lévitique 22.15
9 Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako; Lévitique 23.22 Ruth 2.15 Ruth 2.2 Lévitique 23.10 Lévitique 23.29
10 wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako, wala usiyaokote matunda ya mizabibu yako yaliyopukutika; uyaache kwa ajili ya maskini na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Juges 8.2 Michée 7.1 Esaïe 24.13 Abdias 1.5 Jérémie 49.9
11 Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo. Ephésiens 4.25 Colossiens 3.9 Exode 20.15 Psaumes 101.7 Jérémie 9.3-9.5
12 Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. Exode 20.7 Lévitique 18.21 Jacques 5.12 Lévitique 6.3 Matthieu 5.33-5.34
13 Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang’anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi. Jacques 5.4 Deutéronome 24.14-24.15 Malachie 3.5 Proverbes 20.10 Marc 10.19
14 Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. Deutéronome 27.18 Lévitique 19.32 Lévitique 25.17 1 Pierre 2.17 1 Corinthiens 8.8-8.13
15 Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki. Deutéronome 1.17 Exode 23.2-23.3 Deutéronome 16.19 Proverbes 24.23 Deutéronome 25.13-25.16
16 Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; mimi ndimi Bwana. Exode 23.1 Exode 23.7 Psaumes 15.3 Ezéchiel 22.9 Proverbes 20.19
17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. 1 Jean 2.9 Luc 17.3 1 Jean 2.11 Proverbes 27.5-27.6 Galates 6.1
18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana. Romains 12.19 Galates 5.14 Romains 13.9 Jacques 2.8 Matthieu 19.19
19 Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja. Deutéronome 22.9-22.11 Matthieu 9.16-9.17 2 Samuel 13.29 2 Samuel 18.9 2 Corinthiens 6.14-6.17
20 Tena mtu ye yote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mume, wala hakukombolewa kwa lo lote, wala hakupewa uhuru; wataadhibiwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru. Deutéronome 22.23-22.24 Exode 21.20-21.21
21 Na huyo mume ataleta sadaka yake ya hatia aitoe kwa Bwana, hata mlangoni pa hema ya kukutania; kondoo mume kwa hiyo sadaka ya hatia. Lévitique 6.6-6.7 Lévitique 5.1-5.6 Lévitique 5.15
22 Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia mbele za Bwana, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya. Lévitique 4.26 Lévitique 4.20
23 Nanyi hapo mtakapoingia nchi ile, mkiwa mmepanda miti ya namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu matunda yake kama ni kutotahiriwa; muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu kama kutotahiriwa; matunda yake hayataliwa. Lévitique 12.3 Lévitique 22.27 Jérémie 6.10 Exode 22.29-22.30 Lévitique 14.34
24 Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni matakatifu, kwa ajili ya kumpa Bwana shukrani. Proverbes 3.9 Deutéronome 18.4 Deutéronome 12.17-12.18 Nombres 18.12-18.13 Deutéronome 14.28-14.29
25 Na katika mwaka wa tano mtakula katika matunda yake, ili ipate kuwapa maongeo yake; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Aggée 1.9-1.11 Aggée 1.4-1.6 Malachie 3.8-3.10 Aggée 2.18-2.19 Lévitique 26.3-26.4
26 Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. 2 Rois 17.17 Deutéronome 12.23 2 Rois 21.6 Lévitique 3.17 Lévitique 7.26
27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu. Lévitique 21.5 Jérémie 48.37 Esaïe 15.2 Ezéchiel 7.18 Ezéchiel 44.20
28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana. Deutéronome 14.1 1 Rois 18.28 Jérémie 48.37 Jérémie 16.6 Lévitique 21.5
29 Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu. Osée 4.12-4.14 Lévitique 21.7 1 Corinthiens 6.15 Deutéronome 23.17-23.18
30 Zishikeni Sabato zangu, mpaheshimu patakatifu pangu; mimi ndimi Bwana. Lévitique 26.2 Lévitique 19.3 Ecclésiaste 5.1 Psaumes 89.7 Lévitique 16.2
31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Esaïe 8.19 Lévitique 20.27 1 Samuel 28.3 1 Chroniques 10.13 2 Chroniques 33.6
32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana. 1 Timothée 5.1 Lamentations 5.12 Romains 13.7 Job 32.4 1 Rois 2.19
33 Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu. Exode 22.21 Jérémie 7.6 Malachie 3.5 Exode 23.9 Ezéchiel 22.29
34 Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Deutéronome 10.19 Lévitique 19.18 Exode 12.48-12.49 Matthieu 5.43
35 Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. Deutéronome 25.13 Deutéronome 25.15 Proverbes 16.11 Michée 6.1 Lévitique 19.15
36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. Exode 20.2 Proverbes 11.1 Proverbes 20.10 Deutéronome 25.13-25.15
37 Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi Bwana. Lévitique 18.4-18.5 1 Jean 3.22-3.23 Psaumes 119.34 Deutéronome 4.5-4.6 Deutéronome 4.1-4.2

Cette Bible est dans le domaine public.