Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 5.19
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,Matthieu 4.18-4.22 Marc 1.16-1.20 Josué 12.3 Matthieu 14.34 Nombres 34.11
2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.Marc 1.19 Matthieu 4.21
3 Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.Jean 1.41-1.42 Marc 4.1-4.2 Matthieu 4.18 Matthieu 13.1-13.2 Jean 8.2
4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.Jean 21.6
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.Jean 2.5 Jean 15.14 Ezéchiel 37.11-37.12 Luc 8.24 Ezéchiel 37.4-37.7
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;1 Corinthiens 15.58 Actes 4.4 Galates 6.9 Actes 2.41 Ecclésiaste 11.6
7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.Galates 6.2 Philippiens 4.3 Exode 23.5 Romains 16.2-16.4 Actes 11.25
8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.Esaïe 6.5 Job 42.5-42.6 Apocalypse 1.17 Apocalypse 22.8-22.9 1 Corinthiens 13.12
9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;Luc 4.32 Psaumes 8.6 Luc 4.36 Psaumes 8.8 Marc 9.6
10 na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu.Matthieu 4.19 Matthieu 13.47 Marc 1.17 Matthieu 4.21 Luc 6.14
11 Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, wakaacha vyote wakamfuata.Luc 5.28 Matthieu 4.20 Matthieu 19.27 Marc 10.29-10.30 Philippiens 3.7-3.8
12 Ikawa, alipokuwa katika mmojawapo wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejaa ukoma; naye alipomwona Yesu alianguka kifudifudi, akamwomba akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.Matthieu 8.2-8.4 Luc 17.16 Psaumes 50.15 Luc 17.12-17.13 Marc 1.40-1.45
13 Naye akaunyosha mkono wake, akamgusa akisema, Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukamwondoka.2 Rois 5.10 Psaumes 33.9 Matthieu 9.29-9.30 Ezéchiel 36.29 Osée 14.4
14 Akamkataza asimwambie mtu, ila, Nenda ukajionyeshe kwa kuhani; ukatoe kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.Marc 6.11 Lévitique 14.2-14.32 Matthieu 12.16 Luc 17.14 Matthieu 8.4
15 Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.Matthieu 9.26 Matthieu 15.30-15.31 Marc 1.28 Marc 3.7 Matthieu 4.23-4.25
16 Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.Matthieu 14.23 Luc 6.12 Marc 1.35-1.36 Marc 6.46 Jean 6.15
17 Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.Luc 6.19 Luc 8.46 Matthieu 15.1 Marc 7.1 Luc 11.52-11.54
18 Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.Marc 2.3-2.12 Matthieu 9.2-9.8 Jean 5.5-5.6 Actes 9.33
19 Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.Marc 2.4 Deutéronome 22.8 Matthieu 10.27 2 Samuel 11.2 Matthieu 24.17
20 Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.Luc 7.48 Matthieu 9.2 Actes 14.9 Jean 5.14 Jean 2.25
21 Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? N’nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?Esaïe 43.25 Marc 2.6-2.7 Jean 10.33 Luc 7.49 Psaumes 32.5
22 Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnahojiana nini mioyoni mwenu?Hébreux 4.12 Matthieu 12.25 Marc 8.17 Esaïe 66.18 Apocalypse 2.23
23 Lililo jepesi ni lipi? Kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, uende?Matthieu 9.5 Marc 2.9
24 Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.Esaïe 53.11 Jean 20.22-20.23 Matthieu 28.18 Luc 8.54 Actes 9.40
25 Mara hiyo akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu.Psaumes 33.9 Jean 9.24 Psaumes 103.1-103.3 Luc 17.15-17.18 Psaumes 50.23
26 Ushangao ukawashika wote, wakamtukuza Mungu; wakajaa hofu, wakisema, Leo tumeona mambo ya ajabu.Matthieu 9.8 Luc 7.16 Matthieu 12.23 Actes 5.11-5.13 Matthieu 28.8
27 Baada ya hayo akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate.Marc 2.13-2.22 Matthieu 8.22 Matthieu 4.19-4.21 Matthieu 10.3 Jean 1.43
28 Akaacha vyote, akaondoka, akamfuata.Luc 5.11 1 Rois 19.19-19.21 Matthieu 19.22-19.27 Luc 9.59-9.62
29 Na Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake; palikuwa na mkutano mkuu wa watoza ushuru na watu wengineo waliokuwa wameketi chakulani pamoja nao.Luc 15.1 1 Corinthiens 5.9-5.11 Marc 2.15 Jean 12.2 1 Corinthiens 10.27
30 Ikawa Mafarisayo na waandishi wao kuwanung’unikia wanafunzi wake, wakisema, Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?Actes 23.9 Luc 15.1-15.2 Esaïe 65.5 Luc 5.17 Luc 7.39
31 Yesu akajibu akawaambia, Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi.Marc 2.17 Matthieu 9.12-9.13 Jérémie 8.22
32 Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.Luc 15.10 Luc 15.7 Actes 3.19 Actes 5.31 Luc 24.47
33 Nao wakamwambia, Wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa!Luc 18.12 Matthieu 9.14-9.17 Marc 2.18-2.22 Luc 11.1 Jean 1.35
34 Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao?Jean 3.29 Cantique 3.10-3.11 Psaumes 45.10-45.16 Apocalypse 19.7-19.9 Ephésiens 5.25-5.27
35 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile.Luc 17.22 2 Corinthiens 11.27 Actes 3.21 Actes 14.23 Zacharie 13.7
36 Akawaambia na mithali, Hakuna akataye kiraka cha vazi jipya na kukitia katika vazi kuukuu; na kama akitia, amelikata lile jipya, na kile kiraka cha vazi jipya hakilingani na lile vazi kuukuu.2 Corinthiens 6.16 Matthieu 9.16-9.17 Lévitique 19.19 Marc 2.21-2.22 Deutéronome 22.11
37 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama akitia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe itamwagika, na viriba vitaharibika.Josué 9.4 Psaumes 119.83 Josué 9.13
38 Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya.Hébreux 8.8-8.13 Colossiens 2.19-2.23 1 Timothée 4.8 Galates 2.12-2.14 Hébreux 13.9-13.10
39 Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema.Jérémie 6.16 Romains 4.11-4.12 Hébreux 11.39 Hébreux 11.1-11.2 Marc 7.7-7.13

Cette Bible est dans le domaine public.