Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Josué 8.2
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Usiche, wala usifadhaike; wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake;Deutéronome 7.18 Deutéronome 1.21 Josué 1.9 Josué 6.2 Deutéronome 31.8
2 nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma.Deutéronome 20.14 Josué 6.21 Proverbes 13.22 2 Chroniques 20.22 Luc 12.20-12.21
3 Basi Yoshua akainuka, na watu wote wa vita pamoja naye, ili waende Ai; Yoshua akachagua watu thelathini elfu, watu mashujaa wenye uwezo, akawapeleka wakati wa usiku.2 Pierre 3.10 Matthieu 25.6 Matthieu 24.39 1 Thessaloniciens 5.2 Matthieu 24.50
4 Akawaagiza, akasema, Angalieni, mtaotea kuuvizia ule mji, upande wa nyuma wa mji; msiende mbali sana na mji, lakini kaeni tayari nyote;Juges 20.29 1 Samuel 15.5 Josué 8.16 Juges 20.33 Actes 23.21
5 na mimi, na watu wote walio pamoja nami, tutaukaribia mji; kisha itakuwa, hapo watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo kwanza, sisi tutakimbia mbele yao;Josué 7.5 Matthieu 10.16 Juges 20.31-20.33
6 nao watatoka nje watufuate, hata tuwavute waende mbali na mji wao; kwa kuwa watasema, Wakimbia mbele yetu, kama walivyofanya kwanza; nasi tutakimbia mbele yao;Juges 20.32 Ecclésiaste 9.12 Exode 14.3 Ecclésiaste 8.11 Exode 15.9
7 basi ninyi mtainuka mtoke hapo mwoteapo, na kuushika mji; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, atautia mikononi mwenu.Josué 8.1 2 Rois 5.1 Proverbes 21.30-21.31
8 Kisha itakuwa, mtakapoushika mji, ndipo mtauteketeza mji kwa moto; sawasawa na hilo neno la Bwana; angalieni, nimewaagiza.Josué 1.16 2 Samuel 13.28 Josué 1.9 Josué 6.24 Josué 8.28
9 Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hata hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.Esdras 2.28 Néhémie 7.32 Josué 7.2 Genèse 12.8 Josué 8.12
10 Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli.Josué 7.16 Josué 6.12 Genèse 22.3 Psaumes 119.60 Josué 3.1
11 Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufikilia mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati ya yeye na Ai. 12 Kisha akatwaa watu kama elfu tano, akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa huo mji.Josué 8.2-8.3
13 Basi wakawaweka hao watu, jeshi zima lililokuwa upande wa kaskazini wa mji, na wale waliokuwa waotea upande wa magharibi wa mji; naye Yoshua akaenda usiku huo katikati ya hilo bonde.Josué 8.12 Josué 8.8
14 Kisha ikawa hapo huyo mfalme wa Ai alipoona jambo hilo, ndipo walipofanya haraka, na wakaamka asubuhi na mapema, na watu waume wa mji wakatoka nje waende kupigana na Israeli, yeye na watu wake wote, kwa wakati ulioamriwa, kuikabili Araba; lakini hakujua ya kwamba walikuwako waviziao kinyume chake kwa upande wa nyuma wa mji.Josué 8.16 Deutéronome 1.1 Ecclésiaste 9.12 Josué 8.5 Juges 20.34-20.36
15 Kisha Yoshua na watu wa Israeli wote walifanya kana kwamba wameshindwa mbele yao, wakakimbia kwa njia ya nyika.Josué 18.12 Josué 15.61 Josué 16.1 Juges 20.36
16 Watu wote waliokuwa ndani ya mji waliitwa wakusanyike pamoja ili kuwafuatia; nao wakamfuatia Yoshua, wakasongea mbele na kuuacha mji.Juges 20.31 Josué 8.5-8.6 Psaumes 9.16 Ezéchiel 38.11-38.22 Apocalypse 16.14
17 Hakusalia mtu ye yote ndani ya Ai, au katika Betheli, asiyetoka nje kuwafuatia Israeli; wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli.Josué 11.20 Deutéronome 2.30 Josué 8.24-8.25 Job 5.13 Esaïe 19.11-19.13
18 Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Haya, unyoshe huo mkuki ulio nao mkononi mwako, uuelekeze upande wa Ai; kwa kuwa nitautia mkononi mwako. Basi Yoshua akaunyosha huo mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea huo mji.Josué 8.26 Exode 17.9-17.12 1 Samuel 17.45 Exode 8.5 Josué 8.7
19 Wale watu waliovizia wakainuka kwa upesi kutoka mahali pao, nao wakapiga mbio mara hapo alipokuwa amekwisha unyosha mkono wake, wakaingia ndani ya mji, na kuushika; nao wakafanya haraka kuuteketeza kwa moto huo mji. 20 Kisha hapo hao watu wa Ai walipotazama nyuma yao, wakaona, na tazama, moshi wa huo mji ulikuwa unapaa juu kwenda mawinguni, nao hawakuwa na nguvu za kukimbia huku wala huku; na wale watu waliokuwa wamekimbia kuenenda nyikani wakageuka na kuwarudia hao waliokuwa wakiwafuatia.Amos 2.14-2.16 Psaumes 48.5-48.6 Genèse 19.28 Job 11.20 Apocalypse 6.15-6.17
21 Basi hapo Yoshua na Israeli wote walipoona ya kwamba hao waliovizia wamekwisha kuushika huo mji, na ya kwamba moshi wa mji umepaa juu, ndipo wakageuka tena, na kuwaua watu wa Ai. 22 Tena hao; wengine wakatoka nje kuutoka huo mji kinyume chao; basi hivyo walikuwa wa katikati ya Israeli, wengine upande huu na wengine upande huu; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona.Deutéronome 7.2 Luc 17.26-17.30 Josué 6.21 1 Thessaloniciens 5.3 Job 20.5
23 Kisha wakamshika mfalme wa Ai ali hai, nao wakamleta kwa Yoshua.1 Samuel 15.8 Josué 10.17 Apocalypse 19.20 Josué 8.29
24 Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamekwisha kuwaua wenyeji wote wa Ai katika bara, hapo katika nyika walipokuwamo wakiwafuatia, nao walikuwa wamekwisha anguka wote kwa makali ya upanga, hata walipokuwa wameangamizwa wote, ndipo Israeli wakarejea Ai, na kuupiga huo mji kwa makali ya upanga.Nombres 21.24 Josué 11.10-11.14 Josué 10.30-10.41
25 Wote walioanguka siku hiyo waume kwa wake, walikuwa ni kumi na mbili elfu, yaani, watu wote wa mji wa Ai.Deutéronome 20.16-20.18
26 Kwani huyo Yoshua hakuuzuia mkono wake, huo ulionyosha huo mkuki, hata hapo alipokuwa amewaangamiza kabisa wenyeji wote wa Ai.Josué 8.18 Exode 17.11-17.12
27 Isipokuwa wanyama wa mji na nyara za mji Israeli wakatwaa wenyewe kuwa ni mapato yao, sawasawa na hilo neno la Bwana alilomwamuru Yoshua.Josué 8.2 Josué 11.4 Psaumes 50.10 Matthieu 20.15 Nombres 31.22
28 Basi Yoshua akaupiga moto mji wa Ai, na kuufanya kuwa ni chungu ya magofu hata milele, kuwa ni ukiwa hata siku hii ya leo.Deutéronome 13.16 Esaïe 25.2 Jérémie 50.26 Jérémie 9.11 Michée 3.12
29 Na huyo mfalme wa Ai akamtundika katika mti hata wakati wa jioni; kisha hapo jua lilipokuchwa Yoshua akaagiza, nao wakauondoa mzoga wake katika huo mti, na kuutupa hapo penye maingilio ya lango la mji, kisha wakaweka pale juu yake chungu kubwa ya mawe, hata hivi leo.2 Samuel 18.17 Josué 7.26 Deutéronome 21.22-21.23 Psaumes 110.5 Actes 12.23
30 Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali.Exode 20.24 Deutéronome 27.4-27.6 Genèse 12.7-12.8 Genèse 8.20
31 Kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa Bwana, na kuchinja sadaka za amani.Deutéronome 27.5-27.7 Exode 20.24-20.25 Esdras 6.18 Josué 1.8 2 Chroniques 35.12
32 Akaandika huko juu ya mawe hayo nakala ya torati ya Musa, aliyoiandika mbele ya wana wa Israeli.Deutéronome 27.8 Deutéronome 27.2-27.3
33 Na Israeli wote, na wazee wao, na maakida yao, na makadhi yao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyoamuru, ili wawabarikie watu wa Israeli kwanza.Deutéronome 11.29 Deutéronome 31.12 Deutéronome 31.9 Josué 3.3 Josué 24.1
34 Na baadaye alisoma maneno yote ya torati, baraka na laana, sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati.Néhémie 8.2-8.3 Josué 1.8 Lévitique 26.1-26.46 Deutéronome 31.10-31.12 Néhémie 9.3
35 Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Israeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.Deutéronome 31.12 Néhémie 8.2 Jérémie 26.2 Deutéronome 29.11 Marc 10.14

Cette Bible est dans le domaine public.