Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Juges 1 Bible en Swahili de l’est
1 Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao? Nombres 27.21 Juges 20.18 Juges 1.27 Juges 20.28 Josué 24.29-24.30 2 Bwana akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake. Psaumes 78.68-78.70 Genèse 49.8-49.10 Nombres 2.3 Nombres 7.12 Hébreux 7.14 3 Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika kura yangu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika kura yako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye. Juges 1.17 Josué 19.1 2 Samuel 10.11 Genèse 29.33 4 Yuda akakwea; naye Bwana akawatia Wakanaani na Waperizi mkononi mwao; nao wakawapiga huko Bezeki watu elfu kumi. 1 Samuel 11.8 1 Rois 22.6 1 Rois 22.15 Josué 10.8-10.10 Exode 23.28-23.29 5 Wakampata huyo Adoni-bezeki huko Bezeki; wakapigana naye, nao wakawapiga Wakanaani na Waperizi. 6 Lakini Adoni-bezeki akakimbia; nao wakamwandamia na kumshika, wakamkata vyanda vyake vya gumba vya mikono na vya miguu. 7 Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vyanda vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko. 1 Samuel 15.33 Luc 6.37-6.38 Romains 2.15 Jacques 2.13 Apocalypse 13.10 8 Kisha wana wa Yuda wakapigana na Yerusalemu, wakautwaa, wakaupiga kwa makali ya upanga, na kuupiga moto huo mji. Josué 15.63 Juges 1.21 9 Baadaye wana wa Yuda wakatelemka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi ya milimani, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela. Josué 11.21 Josué 10.36 Josué 15.13-15.20 10 Kisha Yuda akawafuatia hao Wakanaani waliokaa katika Hebroni; (jina la Hebroni hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-arba;) nao wakamwua Sheshai, na Ahimani, na Talmai. Nombres 13.22 Josué 14.15 Josué 15.13-15.19 Psaumes 33.16-33.17 Jérémie 9.23 11 Kisha kutoka hapo akawafuatia wale wenye kukaa Debiri. (Jina la Debiri hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Kiriath-seferi.) Josué 15.15 Josué 10.38-10.39 12 Huyo Kalebu alisema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, nitamwoza mwanangu Aksa awe mkewe. 1 Samuel 17.25 Josué 15.16-15.17 1 Samuel 18.23 13 Naye Othnieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa huyo Kalebu, aliutwaa; basi akamwoza mwanawe Aksa. Juges 3.9 14 Ikawa hapo alipokwenda kukaa naye, huyo mwanamke akamtaka ili aombe shamba kwa baba yake; na huyo mwanamke akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Una haja gani utakayo? Josué 15.18-15.19 15 Mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa wewe umeniweka katika nchi ya Negebu, basi unipe na vijito vya maji pia. Kalebu akampa vile vijito vya maji vya juu na vijito vya chini. Hébreux 6.7 1 Samuel 25.27 2 Corinthiens 9.5 1 Samuel 25.18 Genèse 33.11 16 Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao. Nombres 10.29-10.32 1 Samuel 15.6 Deutéronome 34.3 Juges 4.11 Nombres 21.1 17 Kisha Yuda akaenda pamoja na nduguye Simeoni, na wakawapiga Wakanaani waliokaa katika Sefathi, na kuuharibu mji kabisa. Na jina la mji huo ulikuwa ukiitwa Horma. Nombres 21.3 2 Chroniques 14.10 Josué 19.4 Juges 1.3 Nombres 14.45 18 Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake. Josué 11.22 Juges 3.3 Juges 16.1-16.2 Josué 15.45-15.47 1 Samuel 6.17 19 Bwana alikuwa pamoja na Yuda; naye akawafukuza watu waliokaa katika nchi ya milimani; asiweze kuwafukuza hao waliokaa katika hilo bonde, kwa kuwa wao walikuwa na magari ya chuma. Juges 1.2 Esaïe 41.14-41.15 Josué 7.12 Genèse 39.2 2 Rois 18.7 20 Kisha wakampa huyo Kalebu Hebroni, kama alivyonena Musa naye akawafukuza wale wana watatu wa Anaki. Juges 1.10 Josué 15.13-15.14 Nombres 14.24 Deutéronome 1.36 Josué 21.11-21.12 21 Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo. Josué 15.63 2 Samuel 5.6-5.9 Juges 19.10-19.12 Josué 18.11-18.28 Juges 1.8 22 Nyumba ya Yusufu nayo, wao nao walikwea kwenda juu ya Betheli; naye Bwana alikuwa pamoja nao. Juges 1.19 Nombres 1.32 Josué 16.1-16.4 Genèse 49.24 Josué 14.4 23 Kisha mbari ya Yusufu wakatuma watu waende kuupeleleza Betheli. (Jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Luzu.) Genèse 28.19 Genèse 48.3 Genèse 35.6 Josué 2.1 Josué 7.2 24 Hao wapelelezi walimwona mtu atoka katika huo mji, wakamwambia, Tafadhali, utuonyeshe maingilio ya mji huu, nasi tutakutendea mema. Josué 2.12-2.14 1 Samuel 30.15 25 Basi akawaonyesha maingilio ya mji, nao wakaupiga huo mji kwa makali ya upanga; lakini huyo mtu walimwacha aende zake, na watu wote wa jamaa yake. Josué 6.22-6.25 26 Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo. 2 Rois 7.6 2 Chroniques 1.17 27 Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Bethsheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo. Josué 17.11-17.13 Psaumes 106.34-106.35 Jérémie 48.10 1 Samuel 15.9 Deutéronome 7.2 28 Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepata nguvu, ndipo walipowatia hao Wakanaani katika kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa. 29 Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao. Josué 16.10 1 Rois 9.16 30 Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa. Josué 19.15 31 Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu; Josué 19.24-19.30 32 lakini Waasheri wakakaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; kwa kuwa hawakuwafukuza. Psaumes 106.34-106.35 33 Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Bethshemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya hao wenyeji wa Bethshemeshi, na wenyeji wa Bethanathi, wakawatumikia kazi ya shokoa. Josué 19.32-19.38 Juges 1.30 Psaumes 18.24 Juges 1.35 34 Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kutelemkia bondeni; Josué 19.47 Juges 18.1 35 lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa. Josué 19.42 Juges 12.12 1 Rois 4.9 Josué 10.12 36 Mpaka wa Waamori ulikuwa tangu huko kupandia Akrabimu, tangu hilo jabali, na juu yake. Nombres 34.4 Josué 15.2-15.3