21 Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo. Josué 15.63 Juges 1.8 2 Samuel 5.6-5.9 Juges 19.10-19.12 Josué 18.11-18.28 22 Nyumba ya Yusufu nayo, wao nao walikwea kwenda juu ya Betheli; naye Bwana alikuwa pamoja nao. Juges 1.19 Nombres 1.10 Nombres 1.32 Josué 16.1-16.4 Genèse 49.24 23 Kisha mbari ya Yusufu wakatuma watu waende kuupeleleza Betheli. (Jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Luzu.) Genèse 28.19 Genèse 35.6 Genèse 48.3 Josué 2.1 Josué 7.2 24 Hao wapelelezi walimwona mtu atoka katika huo mji, wakamwambia, Tafadhali, utuonyeshe maingilio ya mji huu, nasi tutakutendea mema. 1 Samuel 30.15 Josué 2.12-2.14 25 Basi akawaonyesha maingilio ya mji, nao wakaupiga huo mji kwa makali ya upanga; lakini huyo mtu walimwacha aende zake, na watu wote wa jamaa yake. Josué 6.22-6.25 26 Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo. 2 Chroniques 1.17 2 Rois 7.6 27 Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Bethsheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo. Josué 17.11-17.13 1 Samuel 15.9 Psaumes 106.34-106.35 Jérémie 48.10 Deutéronome 7.2 28 Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepata nguvu, ndipo walipowatia hao Wakanaani katika kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa. 29 Efraimu naye hakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa katika Gezeri; lakini Wakanaani walikaa ndani ya Gezeri kati yao. Josué 16.10 1 Rois 9.16 30 Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa. Josué 19.15 31 Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu; Josué 19.24-19.30 32 lakini Waasheri wakakaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; kwa kuwa hawakuwafukuza. Psaumes 106.34-106.35 33 Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Bethshemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya hao wenyeji wa Bethshemeshi, na wenyeji wa Bethanathi, wakawatumikia kazi ya shokoa. Josué 19.32-19.38 Juges 1.30 Psaumes 18.24 Juges 1.35 34 Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kutelemkia bondeni; Josué 19.47 Juges 18.1 35 lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa. Josué 19.42 Juges 12.12 1 Rois 4.9 Josué 10.12 36 Mpaka wa Waamori ulikuwa tangu huko kupandia Akrabimu, tangu hilo jabali, na juu yake. Nombres 34.4 Josué 15.2-15.3