Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Matthieu 9
Bible en Swahili de l’est


1 Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. Matthieu 4.13 Marc 5.21 Luc 8.37 Matthieu 8.23 Apocalypse 22.11
2 Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Matthieu 9.22 Matthieu 4.24 Jean 21.5 Colossiens 1.12-1.14 Actes 19.12
3 Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. Matthieu 26.65 Marc 14.64 Actes 6.11-6.13 Luc 5.21 Jean 10.33-10.36
4 Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? Matthieu 12.25 Luc 6.8 Luc 11.17 Jean 2.24-2.25 Luc 9.46-9.47
5 Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? Jean 5.8-5.14 Marc 2.9-2.12 Esaïe 35.5-35.6 Actes 3.16 Luc 5.23-5.25
6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. Esaïe 43.25 Colossiens 3.13 Michée 7.18 2 Corinthiens 5.20 Actes 5.31
7 Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. 8 Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii. Matthieu 15.31 Luc 7.16 Actes 4.21 Luc 17.15 Luc 23.47
9 Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata. Luc 5.27-5.38 Marc 2.14-2.22 Luc 15.1-15.2 Galates 1.16 Luc 6.15
10 Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. 1 Timothée 1.13-1.16 Marc 2.15-2.17 Luc 5.29-5.32 Jean 9.31 Matthieu 5.46-5.47
11 Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Luc 5.30 Matthieu 11.19 Marc 2.16 Galates 2.15 1 Corinthiens 5.9-5.11
12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Apocalypse 3.17-3.18 Luc 5.31 Marc 2.17 Jérémie 33.6 Psaumes 147.3
13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. Matthieu 12.7 Osée 6.6 Marc 2.17 Proverbes 21.3 Luc 19.10
14 Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Marc 2.18-2.22 Luc 18.9-18.12 Matthieu 6.16 Matthieu 11.18-11.19 Luc 5.33-5.39
15 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga. Jean 3.29 Actes 14.23 Esaïe 22.12 Juges 14.11-14.20 Actes 13.1-13.3
16 Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. Psaumes 125.3 Genèse 33.14 Jean 16.12 1 Corinthiens 3.1-3.2 Esaïe 40.11
17 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote. Josué 9.4 Psaumes 119.83 Job 32.19
18 Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. Luc 8.41-8.56 Marc 5.22-5.43 Matthieu 8.2 Matthieu 9.24 Luc 13.14
19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake. Actes 10.38 Matthieu 8.7 Jean 4.34 Galates 6.9-6.10
20 Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Matthieu 14.36 Matthieu 23.5 Marc 5.25-5.43 Luc 8.43-8.56 Actes 19.12
21 Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Luc 8.45-8.47 Marc 5.26-5.33 Actes 19.12
22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. Luc 7.50 Matthieu 15.28 Luc 17.19 Matthieu 9.2 Luc 18.42
23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, 2 Chroniques 35.25 Luc 8.49-8.51 Marc 5.35-5.40 Matthieu 9.18-9.19 Matthieu 11.17
24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. Actes 20.10 Jean 11.11-11.13 Jean 11.4 Psaumes 22.6-22.7 Actes 9.40
25 Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama. Marc 9.27 Actes 9.40-9.41 Marc 8.23 Marc 5.41 Marc 1.31
26 Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote. Matthieu 4.24 Marc 1.45 Matthieu 14.1-14.2 Actes 26.26 Marc 6.14
27 Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi. Matthieu 15.22 Matthieu 20.30-20.31 Luc 18.38-18.39 Marc 10.46-10.48 Matthieu 11.5
28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. Matthieu 8.2 Marc 9.23-9.24 Matthieu 13.36 Jean 4.48-4.50 Matthieu 13.58
29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. Matthieu 8.13 Marc 10.52 Jean 9.6-9.7 Matthieu 9.22 Matthieu 8.6-8.7
30 Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue. Matthieu 8.4 Luc 5.14 Jean 9.7-9.26 Esaïe 42.7 Marc 5.43
31 Lakini wakatoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote. Marc 7.36 Marc 1.44-1.45 Matthieu 9.26
32 Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. Matthieu 12.22-12.24 Luc 11.14 Matthieu 4.24 Marc 9.17-9.27
33 Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote. Marc 7.32-7.37 Esaïe 35.6 Luc 11.14 Luc 7.9 Psaumes 76.1
34 Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo. Luc 11.15 Marc 3.22 Jean 3.20 Matthieu 12.23-12.24
35 Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Matthieu 4.23-4.24 Actes 10.38 Actes 2.22 Luc 4.43-4.44 Marc 1.32-1.39
36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. Marc 6.34 Nombres 27.17 Matthieu 14.14 Zacharie 10.2 Matthieu 15.32
37 Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Luc 10.2 Jean 4.35-4.36 1 Corinthiens 3.9 Marc 16.15 Actes 16.9
38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Michée 5.7 Luc 10.1-10.2 1 Corinthiens 12.28 Jérémie 3.15 2 Thessaloniciens 3.1

Cette Bible est dans le domaine public.