Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jean 9.23
Bible en Swahili de l’est


1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?Luc 13.2 Jean 9.34 Actes 28.4
3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.Jean 11.4 Job 22.5-22.30 Job 42.7 Job 1.8-1.12 Job 21.27
4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.Jean 12.35 Ephésiens 5.16 Ecclésiaste 9.10 Galates 6.10 Jean 4.34
5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.Jean 8.12 Jean 12.46 Jean 1.4-1.9 Esaïe 60.1-60.3 Jean 3.19-3.21
6 Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho,Marc 8.23 Marc 7.33 Apocalypse 3.18
7 akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.Esaïe 35.5 Jean 11.37 Jean 9.11 Néhémie 3.15 Esaïe 8.6
8 Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba?1 Samuel 2.8 Luc 18.35 1 Samuel 21.11 Luc 16.20-16.22 Marc 10.46
9 Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. 10 Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje?1 Corinthiens 15.35 Jean 3.9 Jean 9.26 Ecclésiaste 11.5 Jean 9.15
11 Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.Jean 9.6-9.7 Jean 9.27 Jérémie 36.17
12 Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui.Jean 7.11 Exode 2.18-2.20 Jean 5.11-5.13
13 Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani.Jean 8.3-8.8 Jean 11.57 Jean 12.42 Jean 11.46-11.47 Jean 12.19
14 Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho.Jean 5.9 Matthieu 12.1-12.14 Jean 7.21-7.23 Luc 6.1-6.11 Marc 2.23-3.6
15 Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.Jean 9.26-9.27 Jean 9.10-9.11
16 Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao.Jean 7.43 Jean 10.19 Jean 3.2 Matthieu 12.2 Jean 7.12
17 Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.Jean 6.14 Jean 4.19 Actes 2.22 Matthieu 21.11 Actes 10.38
18 Basi Wayahudi hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona.Jean 5.44 Hébreux 4.11 Jean 12.37-12.40 Jean 1.19 Esaïe 26.11
19 Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa?Actes 4.14 Actes 3.10 Jean 9.8-9.9
20 Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu; 21 lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. 22 Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.Jean 7.13 Jean 16.2 Luc 6.22 Jean 9.34 Jean 12.42-12.43
23 Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.Jean 9.21
24 Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi.Josué 7.19 Jean 9.16 Romains 10.2-10.4 Jean 14.30 Jean 16.2
25 Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona.1 Jean 5.10 Jean 5.11 Jean 9.30
26 Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani? 27 Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?Luc 22.67 Jean 9.10-9.15
28 Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa.Romains 2.17 Jean 7.19 Matthieu 27.39 1 Corinthiens 4.12 Jean 9.34
29 Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako.Jean 8.14 Psaumes 105.26 Jean 7.27 Actes 22.22 Psaumes 103.7
30 Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho!Jean 12.37 Jean 3.10 Matthieu 11.5 Esaïe 29.18 Esaïe 29.14
31 Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.Proverbes 15.29 Proverbes 28.9 Esaïe 1.15 Psaumes 145.19 Zacharie 7.13
32 Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo.Esaïe 64.4 Apocalypse 16.18 Luc 1.70 Job 20.4
33 Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote.Jean 9.16 Jean 3.2 Actes 5.38-5.39
34 Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.Jean 9.22 Jean 9.2 Esaïe 66.5 Psaumes 51.5 Luc 18.17
35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?1 Jean 5.13 Jean 10.36 Hébreux 1.2-1.9 Jean 20.31 Psaumes 2.7
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?Romains 10.14 Cantique 5.9 Jean 1.38 Proverbes 30.3-30.4 Matthieu 11.3
37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.Jean 4.26 Matthieu 13.11-13.12 Matthieu 11.25 Jean 7.17 Psaumes 25.14
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.Matthieu 14.33 Matthieu 28.9 Psaumes 45.11 Matthieu 28.17 Jean 20.28
39 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.Jean 3.19 Jean 12.46 Luc 4.18 Jean 8.12 Actes 26.18
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?Matthieu 15.12-15.14 Apocalypse 3.17 Romains 2.19-2.22 Luc 11.39-11.54 Jean 7.47-7.52
41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.Esaïe 5.21 Jean 15.22-15.24 1 Jean 1.8-1.10 Proverbes 26.12 Hébreux 10.26

Cette Bible est dans le domaine public.