Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 37.27
Bible en Swahili de l’est


1 Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.Proverbes 23.17 Psaumes 37.7 Proverbes 24.19 Psaumes 73.3 Proverbes 3.31
2 Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka.Psaumes 37.35-37.36 Jacques 1.10-1.11 Psaumes 73.17-73.20 Psaumes 92.7 Job 20.5-20.9
3 Umtumaini Bwana ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.Jérémie 17.7-17.8 1 Corinthiens 15.57-15.58 Psaumes 62.8 Matthieu 6.31-6.33 Esaïe 1.16-1.19
4 Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako.Jean 15.7 Psaumes 145.19 Esaïe 58.14 Jean 15.16 1 Jean 5.14-5.15
5 Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.Proverbes 16.3 1 Pierre 5.7 Psaumes 55.22 Philippiens 4.6-4.7 Matthieu 6.25
6 Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri.Job 11.17 Esaïe 58.8 Esaïe 54.17 Michée 7.8-7.9 Esaïe 58.10
7 Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.Psaumes 27.14 Psaumes 40.1 Jérémie 12.1 Psaumes 62.5 Psaumes 62.1
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.Proverbes 14.29 Ephésiens 4.31 Ephésiens 4.26 Proverbes 16.32 Jacques 3.14-3.18
9 Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi.Esaïe 60.21 Psaumes 25.13 Psaumes 55.23 Psaumes 37.29 Job 27.13-27.23
10 Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.Job 24.24 Job 7.10 Psaumes 52.5 Psaumes 37.35-37.36 Apocalypse 6.10-6.11
11 Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.Matthieu 5.5 Psaumes 119.165 Psaumes 72.7 Galates 5.22-5.23 1 Timothée 6.11
12 Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.Psaumes 35.16 Daniel 8.12 Michée 2.1 Psaumes 31.13 2 Samuel 15.10-15.12
13 Bwana atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.Psaumes 2.4 Proverbes 1.26 1 Samuel 26.10 Daniel 5.26 Job 18.20
14 Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta, Wamwangushe chini maskini na mhitaji, Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.Proverbes 29.27 Psaumes 11.2 Psaumes 35.10 Matthieu 23.30-23.34 Proverbes 29.10
15 Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe, Na nyuta zao zitavunjika.Psaumes 46.9 Psaumes 35.8 Psaumes 7.14-7.15 Esther 7.9-7.10 Matthieu 27.4-27.5
16 Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.Proverbes 16.8 Proverbes 15.16-15.17 Proverbes 13.25 1 Timothée 6.6 Ecclésiaste 4.6
17 Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali Bwana huwategemeza wenye haki.Psaumes 145.14 Psaumes 63.8 Esaïe 42.1 Esaïe 41.10 Psaumes 10.15
18 Bwana anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.Psaumes 1.6 Psaumes 103.17 Psaumes 73.24 Psaumes 31.7 1 Jean 2.25
19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.Psaumes 33.19 Proverbes 10.3 Job 5.20-5.22 Amos 5.13 Ephésiens 5.16
20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.Psaumes 102.3 Psaumes 68.2 Psaumes 92.9 Luc 13.3 Juges 5.31
21 Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.Psaumes 112.5 Proverbes 22.7 Hébreux 13.16 2 Corinthiens 8.9 Deutéronome 28.12
22 Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi, Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa.Proverbes 3.33 Psaumes 37.9 Psaumes 128.1 Psaumes 32.1 1 Corinthiens 16.22
23 Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake.1 Samuel 2.9 Proverbes 4.26 Jérémie 10.23 Proverbes 16.9 Psaumes 121.8
24 Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza.Psaumes 145.14 Proverbes 24.16 Jean 10.27-10.30 Psaumes 94.18 Luc 22.31-22.32
25 Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.Hébreux 13.5 Psaumes 25.13 1 Samuel 12.22 Psaumes 37.28 Hébreux 12.5-12.6
26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.Psaumes 112.5 Psaumes 37.21 Psaumes 112.9 Luc 6.35-6.38 Psaumes 147.13
27 Jiepue na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele.Psaumes 34.14 Tite 3.8 Psaumes 102.28 Hébreux 13.16 2 Timothée 2.19
28 Kwa kuwa Bwana hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.Psaumes 21.10 Proverbes 2.22 Psaumes 11.7 Esaïe 59.21 Jean 6.39-6.40
29 Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.Proverbes 2.21 Psaumes 37.9 Psaumes 37.11 Psaumes 37.18 Apocalypse 21.3-21.4
30 Kinywa chake mwenye haki hunena hekima, Na ulimi wake husema hukumu.Proverbes 25.11-25.13 Psaumes 71.15 Deutéronome 6.7-6.9 Proverbes 27.9 Proverbes 10.21
31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi.Deutéronome 6.6 Psaumes 40.8 Psaumes 37.23 Esaïe 51.7 Jérémie 31.33
32 Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumfisha.Psaumes 10.8-10.10 Luc 11.54 Psaumes 37.12 Jérémie 20.10 Luc 20.20
33 Bwana hatamwacha mkononi mwake, Wala hatamlaumu atakapohukumiwa.Psaumes 109.31 2 Pierre 2.9 Romains 8.1 Psaumes 31.7-31.8 1 Samuel 23.26-23.28
34 Wewe umngoje Bwana, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona.Psaumes 27.14 Psaumes 37.9 Psaumes 52.5-52.6 Psaumes 91.8 Psaumes 37.7
35 Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.Job 5.3 Job 8.13-8.19 Psaumes 73.3-73.11 Daniel 4.20-4.33 Esaïe 14.14-14.19
36 Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana.Psaumes 37.10 Esaïe 10.16-10.19 Exode 15.9-15.10 Exode 15.19 Esaïe 10.33-10.34
37 Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.Esaïe 32.17 Esaïe 57.1-57.2 Job 42.12-42.17 Actes 7.59-7.60 Job 1.1
38 Wakosaji wataangamizwa pamoja, Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.Psaumes 52.5 Psaumes 1.4-1.6 Proverbes 14.32 Matthieu 13.49-13.50 Matthieu 25.46
39 Na wokovu wa wenye haki una Bwana; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.Psaumes 9.9 Psaumes 3.8 Psaumes 91.15 Psaumes 46.1 Esaïe 12.2
40 Naye Bwana huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.Esaïe 31.5 1 Chroniques 5.20 Daniel 3.17 Daniel 6.23 Esaïe 46.4

Cette Bible est dans le domaine public.