Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 8
Bible en Swahili de l’est


1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. Actes 7.58 Actes 22.20 Actes 5.40 Actes 5.33 Actes 8.4
2 Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. 2 Chroniques 35.25 Actes 2.5 Jérémie 22.18 2 Chroniques 32.33 Deutéronome 34.8
3 Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. 1 Corinthiens 15.9 Philippiens 3.6 1 Timothée 1.13 Galates 1.13 Actes 7.58
4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. Actes 8.1 Actes 11.19 Actes 14.2-14.7 Actes 15.35 Matthieu 10.23
5 Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Actes 6.5 Actes 8.40 Actes 8.35-8.36 Actes 21.8 Jean 4.25-4.26
6 Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Matthieu 20.15-20.16 Actes 13.44 Jean 4.41-4.42 2 Chroniques 30.12
7 Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Matthieu 10.1 Marc 16.17-16.18 Actes 5.16 Matthieu 4.24 Actes 14.8-14.10
8 Ikawa furaha kubwa katika mji ule. Psaumes 96.10-96.12 Actes 13.48 Esaïe 42.10-42.12 Actes 8.39 Psaumes 98.2-98.6
9 Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. Actes 5.36 Actes 13.6 Jean 7.18 2 Pierre 2.18 2 Thessaloniciens 2.4
10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. Actes 28.6 Actes 14.11 Jonas 3.5 Jérémie 31.34 Jérémie 6.13
11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. Galates 3.1 Actes 8.9 Esaïe 47.9-47.13 Esaïe 8.19 Esaïe 44.25
12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Actes 1.3 Actes 2.38 Actes 2.41 1 Pierre 3.21 Matthieu 28.19
13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. Actes 19.11 Actes 8.6-8.7 Jean 5.20 Actes 13.44 Psaumes 106.12-106.13
14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; Actes 8.1 Galates 2.9 1 Thessaloniciens 2.13 1 Thessaloniciens 3.2 Actes 2.41
15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; Actes 2.38 Jean 14.13-14.14 Philippiens 1.19 Jean 16.23-16.24 Matthieu 18.19
16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Matthieu 28.19 Actes 2.38 Actes 19.2 1 Corinthiens 1.13-1.15 Actes 19.5-19.6
17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Actes 6.6 Actes 19.6 Hébreux 6.2 Actes 9.17 Actes 2.4
18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, 2 Rois 5.15-5.16 1 Timothée 6.5 Matthieu 10.8 2 Rois 8.9 Ezéchiel 13.19
19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Luc 14.7-14.11 1 Corinthiens 15.8-15.9 Jean 5.44 Actes 8.17 3 Jean 1.9
20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Actes 2.38 Daniel 5.17 Matthieu 10.8 Apocalypse 18.15 Deutéronome 7.26
21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Habakuk 2.4 2 Chroniques 25.2 Jean 21.17 Psaumes 36.1 Matthieu 6.22-6.24
22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. Daniel 4.27 1 Rois 8.47-8.48 Actes 9.11 Amos 5.15 Actes 8.20
23 Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. Proverbes 5.22 Esaïe 58.6 Hébreux 12.15 Jean 8.34 Lamentations 3.19
24 Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja. Exode 8.8 Nombres 21.7 1 Rois 13.6 Exode 12.32 Genèse 20.7
25 Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria. Actes 8.40 Jean 15.27 Luc 9.52-9.56 Actes 1.8 Actes 28.31
26 Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Actes 5.19 Actes 27.23 Hébreux 1.14 Actes 12.23 Actes 10.7
27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, Psaumes 68.31 Jean 12.20 Psaumes 87.4 Sophonie 3.10 1 Rois 8.41-8.43
28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Josué 1.8 Luc 4.17 Deutéronome 6.6-6.7 Jean 5.39-5.40 Actes 28.25
29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. Actes 10.19 Actes 11.12 Actes 16.6-16.7 1 Corinthiens 12.11 Actes 13.2-13.4
30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? Luc 24.44-24.45 Matthieu 13.23 Ecclésiaste 9.10 Matthieu 13.51 Ephésiens 5.17
31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. Romains 10.14 Matthieu 18.3-18.4 2 Rois 5.26 Psaumes 25.8-25.9 Jacques 1.21
32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. Esaïe 53.7-53.8 1 Pierre 2.21-2.24 Jérémie 51.40 Jean 1.29 Psaumes 39.2
33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. Esaïe 53.8 Esaïe 53.12 Job 34.5 Philippiens 2.8-2.9 Zacharie 13.7
34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? Matthieu 13.36 Matthieu 15.15 Matthieu 2.2-2.4
35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. Luc 24.27 Actes 18.28 Actes 28.23 Matthieu 5.2 Actes 10.34
36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? Actes 10.47 Jean 3.23 Jean 3.5 1 Jean 5.6 Ezéchiel 36.25
37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Jean 4.1 Jean 3.22-3.23
39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 1 Rois 18.12 Ezéchiel 11.24 2 Rois 2.16 Ezéchiel 8.3 Ezéchiel 43.5
40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria. Actes 23.33 Actes 10.1 Actes 23.23 Actes 21.8 Actes 25.4

Cette Bible est dans le domaine public.