25 Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu. Genèse 24.54 Genèse 24.56 Genèse 28.15 Genèse 24.6-24.7 Genèse 31.13 26 Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia. Genèse 29.30 Osée 12.12 Genèse 31.6 Genèse 29.19-29.20 Genèse 30.29-30.30 27 Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako. Genèse 26.24 Esaïe 61.9 Genèse 39.21-39.23 Actes 7.10 Exode 3.21 28 Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa. Genèse 29.15 Genèse 29.19 29 Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu. Genèse 31.6 Genèse 31.38-31.40 1 Pierre 2.18 Genèse 30.5 Colossiens 3.22-3.25 30 Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe? 1 Timothée 5.8 2 Corinthiens 12.14 Deutéronome 11.10 31 Akamwuliza, Nikupe nini? Yakobo akasema, Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda. 2 Samuel 21.4-21.6 Hébreux 13.5 Psaumes 118.8 32 Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu. Genèse 31.8 Genèse 30.35 Genèse 31.10 33 Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa. 2 Samuel 22.21 Psaumes 37.6 1 Samuel 26.23 Esaïe 59.12 Genèse 31.37 34 Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo. Galates 5.12 1 Corinthiens 14.5 1 Corinthiens 7.7 Nombres 22.29 35 Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe. Genèse 31.9 36 Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia. 37 Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito. Genèse 31.9-31.13 Ezéchiel 31.8 38 Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa. 39 Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka. Exode 12.35-12.36 Genèse 31.9-31.12 Genèse 31.40 Genèse 31.42 Genèse 31.38 40 Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani. 41 Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito, 42 lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo. 43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda. Genèse 30.30 Genèse 26.13-26.14 Genèse 24.35 Genèse 13.2 Genèse 28.15