Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 29
Bible en Swahili de l’est


1 Nawe uwafanyie jambo hili, ili kuwatakasa, wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani; twaa ng’ombe mmoja mume kijana, na kondoo waume wawili walio wakamilifu, 1 Pierre 1.19 Exode 12.5 Matthieu 6.9 Exode 20.11 Lévitique 9.2
2 na mkate usiotiwa chachu, na maandazi yasiyotiwa chachu yaliyokandwa kwa mafuta, na kaki zisizotiwa chachu zilizotiwa mafuta; utazifanya za unga mzuri mwembamba wa ngano. Nombres 6.15 Nombres 6.19 Lévitique 2.15 Lévitique 7.12 Lévitique 8.26
3 Nawe vitie vyote katika kikapu, uvilete ndani ya kikapu, pamoja na huyo ng’ombe, na hao kondoo waume wawili. Lévitique 8.31 Nombres 6.17 Lévitique 8.26 Lévitique 8.2
4 Kisha mlete Haruni na wanawe hata mlangoni pa hema ya kukutania, ukawaoshe kwa maji. Exode 40.12 Hébreux 10.22 Jean 13.8-13.10 Lévitique 8.3-8.6 Exode 30.18-30.21
5 Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho ya naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi; Exode 28.2-28.8 Lévitique 8.7-8.8
6 nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba. Lévitique 8.9 Exode 28.36-28.39
7 Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta. Nombres 35.25 Lévitique 21.10 Exode 28.41 Psaumes 133.2 Lévitique 10.7
8 Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu. Lévitique 8.13 Exode 28.40
9 Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu. Nombres 18.7 Lévitique 8.22-8.28 Nombres 16.40 Nombres 16.10 Exode 28.1
10 Kisha utamleta huyo ng’ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng’ombe. Lévitique 8.14 Lévitique 1.4 Exode 29.15 Exode 29.19 2 Corinthiens 5.21
11 Kisha utamchinja huyo ng’ombe mbele ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania. Lévitique 9.12 Lévitique 9.8 Exode 29.4 Lévitique 1.3-1.5 Lévitique 8.15
12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ng’ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu. Exode 27.2 Lévitique 8.15 Lévitique 9.9 Exode 30.2 Lévitique 4.30
13 Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu. Lévitique 3.3-3.4 1 Samuel 2.16 Lévitique 9.10 Exode 29.18 Lévitique 3.14-3.16
14 Lakini nyama yake huyo ng’ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marago; ni sadaka kwa ajili ya dhambi. Lévitique 4.21 Lévitique 4.11-4.12 Exode 30.10 Lévitique 5.6 Lévitique 4.29
15 Pia mtwae kondoo mume mmoja; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo mume. Exode 29.19 Exode 29.3 Lévitique 1.4-1.9 Exode 29.10 Lévitique 8.18-8.21
16 Kisha utamchinja huyo kondoo mume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kando-kando. Exode 29.11-29.12
17 Kisha utamkata-kata kondoo vipande vyake, na kuyaosha matumbo yake na miguu yake, na kuiweka pamoja na vipande vyake na kichwa chake. Matthieu 23.26 Lévitique 8.21 Jérémie 4.14 Lévitique 1.13 Lévitique 9.14
18 Nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Bwana; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Genèse 8.21 Exode 29.25 Philippiens 4.18 Jérémie 7.21-7.22 Lévitique 9.24
19 Kisha mtwae huyo kondoo wa pili; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo. Exode 29.3 Lévitique 8.22-8.29
20 Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kuume, na katika ncha za masikio ya kuume ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kuume, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kando-kando. Esaïe 50.5 Lévitique 14.7 Hébreux 10.22 1 Pierre 1.2 Lévitique 16.19
21 Kisha twaa katika hiyo damu iliyo juu ya madhabahu, na katika hayo mafuta ya kutiwa, na kumnyunyizia Haruni, juu ya mavazi yake, na wanawe, na mavazi yao pia, pamoja naye; naye atatakaswa, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye. Hébreux 9.22 Exode 29.7 Lévitique 8.30 Exode 29.1 Lévitique 14.15-14.18
22 Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu; Exode 29.13 Lévitique 9.21 Lévitique 9.19 Lévitique 8.25-8.27 Lévitique 7.32-7.33
23 utwae na mkate mmoja wa unga, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na kaki moja katika kile kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichowekwa mbele ya Bwana; Exode 29.2-29.3 Lévitique 8.26
24 nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisa-tikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana. Lévitique 7.30 Lévitique 8.27 Lévitique 10.14 Exode 29.26-29.27 Lévitique 9.21
25 Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, viwe harufu nzuri mbele ya Bwana; ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Lévitique 8.28 Exode 29.41 Lévitique 2.9 Psaumes 99.6 Lévitique 2.16
26 Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; nacho kitakuwa ni sehemu yako. Lévitique 8.29 Psaumes 99.6 Lévitique 7.31 Lévitique 7.34
27 Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe; Nombres 18.11 Lévitique 10.15 Deutéronome 18.3 Hébreux 7.28 Lévitique 7.37
28 navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya Bwana. Exode 29.27 Lévitique 3.1 Nombres 31.29 Nombres 31.41 Nombres 15.19-15.20
29 Na hayo mavazi matakatifu ya Haruni yatakuwa ya wanawe baada yake, wayavae watakapotiwa mafuta, na watakapowekwa kwa kazi takatifu. Nombres 18.8 Exode 40.15 Nombres 20.26-20.28 Exode 30.30 Lévitique 8.7-8.12
30 Huyo mwanawe atakayekuwa kuhani badala yake atayavaa muda wa siku saba, hapo atakapoingia ndani ya hiyo hema ya kukutania, ili atumike ndani ya mahali patakatifu. Nombres 20.28 Exode 29.35 Lévitique 9.1 Lévitique 12.2-12.3 Exode 12.15
31 Nawe twaa huyo kondoo mume aliyekuwa wa kuwekwa kwa kazi takatifu, na kuitokosa nyama yake katika mahali patakatifu. Lévitique 8.31 1 Samuel 2.15 1 Samuel 2.13 Ezéchiel 46.20-46.24
32 Na Haruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Matthieu 12.4 Exode 29.2-29.3 Exode 29.23 Exode 24.9-24.11 Lévitique 10.12-10.14
33 Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu. Nombres 18.4 Nombres 16.40 Nombres 1.51 Jean 6.53-6.55 Psaumes 22.26
34 Na kwamba kitu cho chote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au cho chote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu. Exode 12.10 Lévitique 8.32 Lévitique 10.16 Exode 16.19 Lévitique 7.18-7.19
35 Ni hivyo utakavyowatendea Haruni na wanawe, sawasawa na hayo yote niliyokuagiza; utawaweka kwa kazi takatifu siku saba. Exode 29.37 Lévitique 14.8-14.11 Exode 39.42-39.43 Jean 16.14 Lévitique 8.4-8.36
36 Kila siku utamtoa ng’ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa. Hébreux 10.11 Exode 30.28-30.29 Exode 30.26 Ezéchiel 48.18-48.20 Ezéchiel 43.27
37 Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu. Exode 40.10 Matthieu 23.19 Matthieu 23.17 Exode 30.28-30.29 Daniel 9.24
38 Basi sadaka utakazozitoa juu ya madhabahu ni hizi; wana-kondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku daima. Nombres 28.3-28.8 1 Chroniques 16.40 Daniel 12.11 Daniel 9.27 2 Chroniques 31.3
39 Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni; Ezéchiel 46.13-46.15 2 Rois 16.15 Actes 26.7 Psaumes 55.16-55.17 Luc 1.10
40 tena, pamoja na mwana-kondoo mmoja utatoa vibaba vitatu vya unga mzuri uliochanganyika na mafuta yenye kupondwa, kiasi cha kibaba na robo kibaba; na divai kiasi cha kibaba na robo kibaba, iwe sadaka ya kinywaji. Lévitique 23.13 Esaïe 57.6 Joël 2.14 Ezéchiel 46.14 Philippiens 2.17
41 Na huyo mwana-kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni, nawe utamfanyia vivyo kama ile sadaka ya unga ya asubuhi, na kama ile sadaka yake ya kinywaji, iwe harufu nzuri, ni dhabihu ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Ezéchiel 46.13-46.15 Daniel 9.21 1 Rois 18.29 Esdras 9.4-9.5 1 Rois 18.36
42 Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya Bwana; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo. Exode 25.22
43 Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo, na hiyo Hema itafanywa takatifu na utukufu wangu. 1 Rois 8.11 Exode 40.34 Ezéchiel 43.5 2 Chroniques 5.14 Malachie 3.1
44 Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu; pia Haruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Lévitique 21.15 Lévitique 22.16 Lévitique 22.9 Jean 10.36 Apocalypse 1.5-1.6
45 Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao. 2 Corinthiens 6.16 Zacharie 2.10 Lévitique 26.12 Exode 25.8 Apocalypse 21.3
46 Nao watanijua kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao; ni mimi Bwana Mungu wao. Exode 20.2 Ezéchiel 20.5 Lévitique 19.2 Jérémie 31.33 Lévitique 18.30

Cette Bible est dans le domaine public.