Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 22.32
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng’ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko.Josué 3.16 Nombres 34.15 Deutéronome 34.1 Nombres 21.20 Deutéronome 34.8
2 Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori.Juges 11.25 Nombres 21.3 Nombres 21.20-21.35
3 Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli.Exode 15.15 Josué 2.24 Esaïe 23.5 Josué 9.24 Josué 2.10-2.11
4 Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng’ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.Nombres 31.8 Nombres 25.15-25.18 Juges 11.25 Nombres 24.17 Josué 13.21-13.22
5 Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.Deutéronome 23.4 Josué 24.9 Michée 6.5 Jude 1.11 Josué 13.22
6 Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.Nombres 24.9 Nombres 23.7-23.8 Genèse 27.29 Genèse 12.3 1 Rois 22.6
7 Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.Michée 3.11 1 Samuel 9.7-9.8 Esaïe 56.11 Nombres 23.23 Romains 16.18
8 Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama Bwana atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu.Ezéchiel 33.31 Jérémie 12.2 Nombres 12.6 Nombres 23.12 Nombres 22.19-22.20
9 Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?Genèse 20.3 Nombres 22.20 Genèse 41.25 Exode 4.2 Matthieu 24.24
10 Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema, 11 Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza. 12 Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.Genèse 12.2 Nombres 23.3 Genèse 22.16-22.18 Nombres 23.13-23.15 Psaumes 146.5
13 Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana Bwana amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi.Nombres 22.14 Deutéronome 23.5
14 Wakuu wakaondoka wakaenda kwa Balaki, wakasema, Balaamu, anakataa kuja pamoja nasi.Nombres 22.13 Nombres 22.37
15 Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza.Actes 10.7-10.8 Nombres 22.7-22.8
16 Wakamfikilia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lo lote lisikuzuie usinijie; 17 maana nitakufanyizia heshima nyingi sana, na neno lo lote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa.Nombres 24.11 Matthieu 14.7 Deutéronome 16.9 Esther 7.9 Nombres 23.2-23.3
18 Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.Nombres 24.13 2 Chroniques 18.13 1 Rois 22.14 Nombres 23.26 Nombres 22.38
19 Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua Bwana atakaloniambia zaidi.Nombres 22.7-22.8 Jude 1.11 2 Pierre 2.15 2 Pierre 2.3 1 Timothée 6.9-6.10
20 Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.Nombres 23.26 Nombres 24.13 Nombres 23.12 Nombres 22.35 Esaïe 37.29
21 Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.Proverbes 1.15-1.16
22 Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.Nombres 22.32 Exode 4.24 Exode 23.20 Nombres 22.35 Osée 12.4-12.5
23 Na yule punda akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejeza njiani.Daniel 10.7 Actes 22.9 Jude 1.11 2 Rois 6.17 2 Pierre 2.16
24 Kisha malaika wa Bwana akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu. 25 Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili.Esaïe 47.12 Job 5.13-5.15
26 Malaika wa Bwana akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto.Esaïe 26.11 Osée 2.6
27 Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.Jacques 1.19 Proverbes 14.16 Proverbes 27.3-27.4
28 Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?2 Pierre 2.16 1 Corinthiens 1.19 Exode 4.11 Luc 1.37 Romains 8.22
29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.Proverbes 12.10 Matthieu 15.19 Proverbes 12.16 Ecclésiaste 9.3
30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!2 Pierre 2.16 1 Corinthiens 1.27-1.28
31 Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.Genèse 21.19 Luc 24.31 Luc 24.16 Psaumes 9.20 Exode 34.8
32 Malaika wa Bwana akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,Nombres 22.22 Psaumes 36.6 Michée 6.5 Exode 3.2-3.6 Actes 13.10
33 punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.Nombres 14.37 1 Rois 13.24-13.28 Nombres 16.33-16.35
34 Balaamu akamwambia malaika wa Bwana, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.Job 34.31-34.32 1 Samuel 15.24 2 Samuel 12.13 1 Samuel 15.30 1 Samuel 26.21
35 Malaika wa Bwana akamwambia Balaamu Enenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki.Nombres 22.20-22.21 Esaïe 37.26-37.29 2 Thessaloniciens 2.9-2.12 Psaumes 81.12
36 Balaki aliposikia ya kuwa Balaamu amefika, akatoka kwenda kumlaki, mpaka Mji wa Moabu, ulioko katika mpaka wa Arnoni, ulioko katika upande wa mwisho wa mpaka huo.Genèse 14.17 Deutéronome 2.24 Esaïe 16.2 1 Samuel 13.10 Juges 11.18
37 Balaki akamwambia Balaamu, Je! Mimi sikutuma watu kwako kwa bidii ili kukuita? Mbona hukunijia? Je! Siwezi mimi kukufanyizia heshima nyingi?Nombres 24.11 Jean 5.44 Nombres 22.16-22.17 Matthieu 4.8-4.9 Luc 4.6
38 Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wo wote kusema neno lo lote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema.Nombres 22.18 Nombres 23.26 Nombres 23.16 Esaïe 44.25 Proverbes 19.21
39 Balaamu akaenda pamoja na Balaki wakafika Kiriath-husothi. 40 Balaki akachinja ng’ombe, na kondoo, akampelekea Balaamu na wale wakuu waliokuwa pamoja naye.Nombres 23.14 Proverbes 1.16 Nombres 23.30 Nombres 23.2 Genèse 31.54
41 Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hata mahali pa juu pa Baali; na kutoka huko akawaona watu, hata pande zao za mwisho.Nombres 23.13 Nombres 21.28 Jérémie 48.35 Deutéronome 12.2 Nombres 25.2-25.3

Cette Bible est dans le domaine public.