Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 3
Bible en Swahili de l’est


1 Basi vizazi vya Haruni na Musa, siku hiyo Bwana aliyosema na Musa katika mlima wa Sinai, ni hivi. Exode 6.20 Genèse 2.4 Genèse 10.1 Exode 6.27 Matthieu 1.1
2 Tena majina ya hao wana wa Haruni ni haya; Nadabu mzaliwa wa kwanza, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. Exode 6.23 Nombres 26.60 Exode 28.1 1 Chroniques 24.1 1 Chroniques 6.3
3 Hayo ndiyo majina ya wana wa Haruni, hao makuhani waliotiwa mafuta, ambao aliwaweka wakfu ili wafanye kazi ya ukuhani. Exode 28.41 Lévitique 8.12 Lévitique 8.30 Lévitique 8.1-8.9 Exode 29.1-29.37
4 Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana, waliposongeza moto wa kigeni mbele za Bwana, katika bara ya Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani mbele ya uso wa Haruni baba yao. Lévitique 10.1-10.2 Nombres 26.61
5 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 6 Ilete karibu kabila ya Lawi, ukawaweke mbele ya Haruni kuhani, ili wapate kumtumikia. Deutéronome 33.8-33.9 Nombres 1.49-1.53 Deutéronome 10.8 Malachie 2.4 Nombres 8.6-8.26
7 Nao wataulinda ulinzi wake, na ulinzi wa mkutano wote mbele ya hema ya kukutania, ili watumike utumishi wa maskani. Nombres 1.50 Nombres 8.15 Nombres 8.11 1 Chroniques 26.20 Nombres 31.30
8 Nao watavitunza vyombo vyote vya hema ya kukutania, na kulinda ulinzi wa wana wa Israeli, ili watumike utumishi wa maskani. 1 Chroniques 26.20-26.28 Nombres 10.17 Nombres 10.21 Esaïe 52.11 Nombres 4.15
9 Nawe utawapa Haruni na wanawe hao Walawi wawe nao; amepewa watu hao kabisa kwa ajili ya wana wa Israeli. Nombres 8.19 Ephésiens 4.8 Nombres 18.6-18.7 Ephésiens 4.11
10 Nawe utawaweka Haruni na wanawe, nao wataushika ukuhani wao, na mgeni atakayekaribia atauawa. Nombres 1.51 Nombres 18.7 Nombres 3.38 Romains 12.7 1 Chroniques 6.32
11 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 12 Mimi, tazama, nimewatwaa Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu; Nombres 3.41 Nombres 8.16 Nombres 8.18 Nombres 3.45 Nombres 18.6
13 kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi Bwana. Exode 13.2 Exode 13.12 Lévitique 27.26 Exode 13.15 Nombres 18.15
14 Kisha Bwana akanena na Musa huko katika bara ya Sinai, na kumwambia, 15 Uwahesabu wana wa Lawi kwa kuandama nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mtu mume tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu. Nombres 26.62 Proverbes 8.17 Nombres 3.28 Nombres 3.39-3.40 Marc 10.14
16 Basi Musa akawahesabu kama neno la Bwana kama alivyoagizwa. Nombres 4.37 Nombres 3.39 Nombres 4.41 Nombres 4.27 Genèse 45.21
17 Na wana wa Lawi walikuwa ni hawa kwa majina yao; Gershoni, na Kohathi, na Merari. Genèse 46.11 Exode 6.16-6.19 Nombres 24.1-24.25 Josué 21.1-21.45 1 Chroniques 6.1-6.2
18 Na majina ya wana wa Gershoni kwa jamaa zao ni Libni na Shimei. 1 Chroniques 6.17 1 Chroniques 6.20-6.21 Nombres 3.21 1 Chroniques 26.1-26.32 Néhémie 12.1-12.26
19 Na wana wa Kohathi kwa jamaa zao ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. Exode 6.18 1 Chroniques 6.18 1 Chroniques 15.5 1 Chroniques 25.4 1 Chroniques 26.1-26.32
20 Na wana wa Merari kwa jamaa zao ni Mahli, na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kwa nyumba za baba zao. Exode 6.19 1 Chroniques 6.19 Nombres 3.33 1 Chroniques 6.44-6.47 1 Chroniques 23.21-23.23
21 Katika Gershoni walikuwa jamaa ya Walibni, na jamaa ya Washimei, hawa ndio jamaa za Wagershoni. 22 Hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya waume wote, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, hao waliohesabiwa kwao walikuwa saba elfu na mia tano. Nombres 4.38-4.40
23 Jamaa za Wagershoni watapanga rago nyuma ya maskani, upande wa magharibi. Nombres 1.53 Nombres 2.17
24 Na mkuu wa nyumba ya baba zao Wagershoni atakuwa Eliasafu mwana wa Laeli. 25 Na ulinzi wa Wagershoni katika hema ya kukutania ni hiyo maskani, na Hema, na kifuniko chake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania, Exode 25.9 Esdras 8.28-8.30 Exode 40.28 Colossiens 4.17 2 Chroniques 31.2
26 na kuta za nguo za ua, na sitara ya mlango wa ua, iliyo karibu na maskani, na karibu na madhabahu pande zote, na kamba zake zitumiwazo kwa matumizi yake yote. Exode 35.18 Exode 27.9-27.16 Exode 38.9-38.16
27 Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi. 1 Chroniques 26.23 Nombres 3.19 1 Chroniques 23.12
28 Kama hesabu ya waume wote, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa elfu nane na mia sita, wenye kuulinda ulinzi wa mahali patakatifu. Nombres 4.35-4.36 Nombres 3.31 Nombres 3.7
29 Jamaa za wana wa Kohathi watapanga rago upande wa kusini wa maskani. Nombres 1.53 Nombres 3.23 Nombres 2.10
30 Na mkuu wa nyumba ya baba za jamaa za Wakohathi atakuwa Elisafani mwana wa Uzieli. 31 Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika kutumika kwao, na pazia, na utumishi wake wote. Exode 36.35-36.36 Nombres 4.4-4.16 Exode 40.30 Exode 40.2-40.16 Exode 31.1-31.18
32 Na Eleazari mwana wa Haruni kuhani atakuwa mkuu wa hao wakuu wa Walawi, naye atawasimamia hao walindao ulinzi wa mahali patakatifu. Nombres 4.16 1 Chroniques 9.14-9.20 2 Rois 25.18 Nombres 20.25-20.28 1 Chroniques 26.20-26.24
33 Katika Merari ni jamaa ya hao Wamahli, na jamaa ya Wamushi; hizo ni jamaa za Merari. 1 Chroniques 6.19 Nombres 3.20 1 Chroniques 23.21
34 Na hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya waume wote, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa sita elfu na mia mbili. Nombres 2.9 Nombres 2.11 Nombres 1.21
35 Na mkuu wa nyumba ya baba za jamaa za Merari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hao watapanga rago upande wa maskani, wa kaskazini. Nombres 2.25 Nombres 1.53 Nombres 3.28-3.29
36 Na usimamizi walioamriwa wana wa Merari ulikuwa ni kutunza mbao za maskani, na mataruma yake, na nguzo zake, na matako yake, na vyombo vyake vyote, na utumishi wake wote; Exode 26.32 Exode 26.37 Exode 26.15-26.29 Exode 35.11 Exode 39.33
37 na nguzo za ua zilizouzunguka, na matako yake, na vigingi vyake, na kamba zake. 38 Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa. Nombres 3.10 Nombres 1.53 Nombres 2.3 Nombres 18.1-18.5 1 Chroniques 6.48-6.49
39 Hao wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya Bwana, kwa jamaa zao, waume wote tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa ishirini na mbili elfu. Nombres 26.62 Nombres 4.47-4.48 Matthieu 7.14
40 Kisha Bwana akamwambia Musa, Uwahesabu waume wote wazaliwa wa kwanza katika wana wa Israeli tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi uyahesabu majina yao. Nombres 3.15 Apocalypse 3.5 Nombres 3.12 Exode 32.26-32.29 Nombres 3.45
41 Nawe utawatwaa Walawi kwa ajili yangu mimi (Mimi ndimi Bwana) badala ya hao wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli; na wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa wana wa Israeli. Nombres 3.12 Nombres 3.45 Exode 32.26-32.29 Nombres 18.15 Exode 24.5-24.6
42 Musa akahesabu, kama Bwana alivyomwagiza, wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli. 43 Wazaliwa wa kwanza wote walio waume kwa hesabu ya majina, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, katika hao waliohesabiwa kwao, walikuwa ishirini na mbili elfu na mia mbili na sabini na watatu. Nombres 3.39
44 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 45 Uwatwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza katika wana wa Israeli, na wanyama wa Walawi badala ya wanyama wao; na hao Walawi watakuwa wangu mimi; mimi ndimi Bwana. Nombres 3.12 Nombres 3.40-3.41
46 Tena kwa kuwakomboa hao watu mia mbili na sabini na watatu, wa hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli, ambao wamezidi ile hesabu ya Walawi, Exode 13.13 Nombres 18.15-18.16
47 utatwaa shekeli tano kwa kichwa cha kila mtu kwa hiyo shekeli ya mahali patakatifu (shekeli ni gera ishirini); Lévitique 27.6 Exode 30.13 Lévitique 27.25 Nombres 18.16 Ezéchiel 45.12
48 na hizo fedha ambazo waliosalia wamekombolewa kwazo utampa Haruni na wanawe. 49 Basi Musa akawatoza fedha za ukombozi, hao waliozidi hesabu ya wale waliokombolewa na Walawi; 50 akatwaa hizo fedha kwa wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli; shekeli elfu moja na mia tatu na sitini na tano kwa shekeli ya mahali patakatifu; Nombres 3.46-3.47 Hébreux 9.12 1 Timothée 2.5-2.6 1 Pierre 1.18 Matthieu 20.28
51 kisha hizo fedha za ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Musa. Nombres 3.48 Nombres 16.15 1 Pierre 5.2 1 Corinthiens 9.12 1 Samuel 12.3-12.4

Cette Bible est dans le domaine public.