Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 4.10
Bible en Swahili de l’est


1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,Matthieu 4.1-4.11 Marc 1.12-1.13 1 Rois 19.4 Luc 3.3 Luc 4.18
2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.1 Rois 19.8 Exode 34.28 Hébreux 2.18 Hébreux 4.15 Deutéronome 9.9
3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.Matthieu 4.3 Luc 3.22
4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.Deutéronome 8.3 Ephésiens 6.17 Luc 4.10 Luc 4.8 Jean 10.34-10.35
5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.Job 20.5 Matthieu 4.8 Ephésiens 6.12 1 Corinthiens 15.52 Marc 4.8-4.9
6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.Jean 12.31 Jean 14.30 Ephésiens 2.2 1 Jean 5.19 Apocalypse 13.2
7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.Psaumes 72.11 Matthieu 2.11 Luc 17.16 Apocalypse 22.8 Esaïe 46.6
8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.Deutéronome 6.13 Matthieu 4.10 Deutéronome 10.20 Luc 4.4 Jacques 4.7
9 Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini;Luc 4.3 Matthieu 4.5-4.6 Matthieu 8.29 Job 2.6 Romains 1.4
10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde;Psaumes 91.11-91.12 Luc 4.8 Hébreux 1.14 2 Corinthiens 11.14 Luc 4.3
11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.Psaumes 91.12
12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.Deutéronome 6.16 Psaumes 95.9 Matthieu 4.7 Psaumes 106.14 1 Corinthiens 10.9
13 Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.Jean 14.30 Hébreux 4.15 Jacques 4.7 Matthieu 4.11
14 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.Matthieu 4.12 Marc 1.14 Matthieu 9.26 Marc 1.28 Jean 4.43
15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.Matthieu 4.23 Matthieu 9.8 Luc 4.16 Matthieu 9.35 Marc 1.45
16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.Luc 2.39 Luc 2.51 Matthieu 2.23 Actes 13.14-13.16 Actes 17.2
17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,Esaïe 61.1-61.3 Actes 13.15 Luc 20.42 Actes 7.42
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,Esaïe 61.1 Matthieu 11.5 Psaumes 146.7-146.8 Actes 10.38 Luc 7.22
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.Esaïe 61.2 Esaïe 63.4 Luc 19.42 Lévitique 25.50-25.54 Lévitique 25.8-25.13
20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.Luc 4.17 Luc 19.48 Jean 8.2 Matthieu 26.55 Actes 16.13
21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.Jean 4.25-4.26 Actes 2.16-2.18 Actes 3.18 Luc 10.23-10.24 Jean 5.39
22 Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?Jean 6.42 Psaumes 45.2 Matthieu 13.54-13.56 Proverbes 16.21 Cantique 5.16
23 Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.Marc 6.1 Matthieu 4.13 Jean 2.3-2.4 Matthieu 11.23-11.24 Romains 2.21-2.22
24 Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe.Matthieu 13.57 Jean 4.44 Marc 6.4-6.5 Actes 22.3
25 Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima;1 Rois 17.1 Jacques 5.17 Matthieu 20.15 Marc 7.26-7.29 Romains 9.15
26 wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni.1 Rois 17.9-17.24 Matthieu 11.21
27 Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.2 Rois 5.1-5.27 Job 21.22 Job 33.13 Daniel 4.35 Jean 17.12
28 Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo.Jérémie 37.15-37.16 2 Chroniques 16.10 Actes 7.54 Luc 11.53-11.54 Actes 22.21-22.23
29 Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini;Jean 8.59 Psaumes 37.32-37.33 Actes 7.57-7.58 Nombres 15.35 Jean 8.37
30 lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake.Jean 10.39 Jean 8.59 Actes 12.18 Jean 18.6-18.7
31 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;Matthieu 4.13 Matthieu 10.23 Actes 13.50-14.2 Luc 4.23 Actes 14.6-14.7
32 wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.Luc 4.36 Matthieu 7.28-7.29 1 Corinthiens 14.24-14.25 Marc 1.22 Jérémie 23.28-23.29
33 Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu,Marc 1.23
34 akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu.Marc 1.24 Matthieu 8.29 Jacques 2.19 Apocalypse 3.7 Actes 3.14
35 Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno.Luc 4.41 Luc 4.39 Matthieu 8.26 Luc 11.22 Psaumes 50.16
36 Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.Luc 4.32 1 Pierre 3.22 Luc 10.17-10.20 Matthieu 9.33 Matthieu 12.22-12.23
37 Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.Luc 4.14 Matthieu 9.26 Marc 1.28 Marc 1.45 Esaïe 52.13
38 Akatoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake.Matthieu 8.14-8.15 Marc 1.29-1.31 1 Corinthiens 9.5 Jacques 5.14-5.15 Matthieu 15.23
39 Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia.Luc 4.35 Luc 8.24 Luc 8.2-8.3 Luc 4.41 2 Corinthiens 5.14-5.15
40 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.Matthieu 8.16-8.17 Marc 1.32-1.34 Marc 5.23 Matthieu 14.13 Matthieu 11.5
41 Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.Marc 1.34 Marc 3.11 Actes 16.17-16.18 Matthieu 4.3 Luc 4.34-4.35
42 Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafuta-tafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao.Matthieu 14.13-14.14 Luc 8.37-8.38 Luc 6.12 Marc 6.33-6.34 Jean 4.34
43 Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa.Marc 1.38-1.39 2 Timothée 4.2 Jean 6.38-6.40 Jean 9.4 Esaïe 48.16
44 Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.Matthieu 4.23 Marc 1.39 Luc 4.15

Cette Bible est dans le domaine public.