Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 106.21
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.Psaumes 105.1 Psaumes 107.1 1 Chroniques 16.34 Psaumes 105.45 Esdras 3.11
2 Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya Bwana, Kuzihubiri sifa zake zote?Job 26.14 Psaumes 145.3-145.12 Romains 11.33 Psaumes 40.5 Psaumes 139.17-139.18
3 Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.Psaumes 15.2 Apocalypse 22.14 Jacques 1.25 Galates 6.9 Luc 11.28
4 Ee Bwana, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako,Psaumes 119.132 Luc 23.42 Actes 15.14 Néhémie 13.14 Luc 1.68-1.69
5 Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.Psaumes 105.6 Psaumes 105.43 Esaïe 12.6 Jacques 2.5 Psaumes 118.15
6 Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu, Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.1 Rois 8.47 Néhémie 9.16 Lévitique 26.40 Psaumes 78.8 Esdras 9.6-9.7
7 Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.Exode 14.11-14.12 Psaumes 78.42 Proverbes 1.22 Deutéronome 15.15 Psaumes 5.7
8 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu.Exode 9.16 Ezéchiel 20.9 Ezéchiel 20.14 Romains 9.17 Ezéchiel 20.22
9 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.Psaumes 18.15 Nahum 1.4 Psaumes 78.13 Esaïe 63.11-63.14 Esaïe 51.10
10 Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.Psaumes 107.2 Exode 14.30 Michée 6.4 Exode 15.9-15.10 Exode 15.13
11 Maji yakawafunika watesi wao, Hakusalia hata mmoja wao.Exode 15.5 Exode 14.27-14.28 Psaumes 78.53 Exode 15.10 Exode 15.19
12 Ndipo walipoyaamini maneno yake, Waliziimba sifa zake.Exode 14.31-15.21 Luc 8.13 Jean 8.30-8.31
13 Wakayasahau matendo yake kwa haraka, Hawakulingojea shauri lake.Exode 15.24 Exode 16.2 Psaumes 78.11 Exode 17.2 Proverbes 1.30
14 Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani.1 Corinthiens 10.9 Exode 17.2 Nombres 11.4 1 Corinthiens 10.6 Nombres 11.33-11.34
15 Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao.Esaïe 10.16 Esaïe 24.16 Psaumes 78.29-78.31 Nombres 11.31-11.34
16 Wakamhusudu Musa matuoni, Na Haruni, mtakatifu wa Bwana.Lévitique 21.10-21.12 Nombres 16.1-16.50 Exode 28.36 Lévitique 21.6-21.8
17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu.Deutéronome 11.6 Nombres 26.10 Nombres 16.29-16.33
18 Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza wabaya.Nombres 16.46 Hébreux 12.29 Nombres 16.35-16.40
19 Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.Exode 32.4-32.8 Néhémie 9.18 Exode 32.35 Deutéronome 9.8 Actes 7.41
20 Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng’ombe mla majani.Jérémie 2.11 Exode 20.4-20.5 Psaumes 89.17 Romains 1.22-1.23 Esaïe 40.18-40.25
21 Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.Psaumes 106.13 Deutéronome 7.18-7.19 Esaïe 12.2 Luc 1.47 Deutéronome 32.17-32.18
22 Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.Psaumes 105.23 Exode 14.25-14.28 Psaumes 78.51 Psaumes 105.27-105.36 Exode 15.10
23 Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.Ezéchiel 22.30 Deutéronome 9.25 Psaumes 105.6 Matthieu 12.18 Psaumes 105.26
24 Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake.Deutéronome 1.32 Nombres 14.31 Ezéchiel 20.6 Jérémie 3.19 Hébreux 3.18-3.19
25 Bali wakanung’unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana.Hébreux 3.15 Nombres 14.22 Deutéronome 1.26-1.27 Hébreux 3.7-3.8 Nombres 14.1-14.4
26 Ndipo alipowainulia mkono wake, Ya kuwa atawaangamiza jangwani,Ezéchiel 20.15 Hébreux 3.11 Psaumes 95.11 Nombres 14.28-14.35 Exode 6.8
27 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali.Psaumes 44.11 Lévitique 26.33 Deutéronome 32.26-32.27 Ezéchiel 20.23 Deutéronome 4.26-4.27
28 Wakajiambatiza na Baal-Peori, Wakazila dhabihu za wafu.Osée 9.10 Deutéronome 4.3 1 Corinthiens 10.19-10.20 Jérémie 10.8-10.10 Nombres 31.16
29 Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.Nombres 25.9 Deutéronome 32.16-32.21 1 Corinthiens 10.8 Romains 1.21-1.24 Psaumes 106.39
30 Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa.Josué 7.12 Nombres 25.6-25.8 Deutéronome 13.15-13.17 Jonas 1.12-1.15 1 Rois 18.40-18.41
31 Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele.Nombres 25.11-25.13 Genèse 15.6 Marc 14.3-14.9 Deutéronome 24.13
32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,Psaumes 81.7 Deutéronome 1.37 Nombres 20.2-20.13 Deutéronome 4.21 Deutéronome 3.26
33 Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.Nombres 20.10-20.11 Job 38.2 Jacques 3.2 Genèse 30.1 Genèse 35.16-35.18
34 Hawakuwaharibu watu wa nchi Kama Bwana alivyowaambia;Juges 1.21 Deutéronome 7.16 Deutéronome 7.2 Juges 1.19 1 Samuel 15.3
35 Bali walijichanganya na mataifa, Wakajifunza matendo yao.Juges 3.5-3.6 Juges 2.2-2.3 Esaïe 2.6 Josué 15.63 1 Corinthiens 5.6
36 Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao.Deutéronome 7.16 Exode 23.33 Juges 2.3 Juges 3.5-3.7 Ezéchiel 20.28-20.32
37 Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.2 Rois 16.3 1 Corinthiens 10.20 2 Rois 17.17 Deutéronome 32.17 Ezéchiel 20.26
38 Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.Nombres 35.33 Esaïe 1.15 Esaïe 26.21 Deutéronome 21.9 Ezéchiel 22.3
39 Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, Wakafanya uasherati kwa matendo yao.Ezéchiel 20.18 Nombres 15.39 Lévitique 17.7 Osée 9.1 Ezéchiel 20.30-20.31
40 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya watu wake, Akauchukia urithi wake.Juges 2.14 Deutéronome 9.29 Deutéronome 32.19 Juges 2.20 Lévitique 20.23
41 Akawatia mikononi mwa mataifa, Nao waliowachukia wakawatawala.Juges 2.14 Deutéronome 32.30 Juges 3.8 Juges 3.12 Néhémie 9.27-9.38
42 Adui zao wakawaonea, Wakatiishwa chini ya mkono wao.Juges 4.3 Juges 10.12
43 Mara nyingi aliwaponya, Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao, Wakadhilika katika uovu wao.Juges 2.16-2.18 Psaumes 81.12 1 Samuel 12.9-12.11 Juges 6.5 Psaumes 106.29
44 Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao.Juges 3.9 Juges 4.3 Juges 6.6-6.10 Juges 2.18 Néhémie 9.27-9.38
45 Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;Psaumes 105.8 Psaumes 69.16 Juges 2.18 Psaumes 90.13 Lamentations 3.32
46 Akawajalia kuhurumiwa Na watu wote waliowateka.Esdras 9.9 Jérémie 42.12 1 Rois 8.50 Néhémie 1.11 2 Chroniques 30.9
47 Ee Bwana, Mungu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.Apocalypse 7.10-7.12 Ezéchiel 36.24-36.28 Ezéchiel 37.21-37.28 1 Chroniques 16.35-16.36 Psaumes 126.1
48 Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Watu wote na waseme, Amina. Haleluya.Psaumes 41.13 Psaumes 89.52 Psaumes 72.18-72.19 Psaumes 105.45-106.1 1 Chroniques 29.10

Cette Bible est dans le domaine public.