Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 18
Bible en Swahili de l’est


1 Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana; 2 Samuel 22.1-22.51 1 Jean 4.19 Colossiens 1.11 Philippiens 4.13 Esaïe 12.1-12.6
2 Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. Psaumes 144.2 Psaumes 28.1 Jérémie 16.19 Proverbes 18.10 Esaïe 32.2
3 Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu. Psaumes 55.16 Psaumes 28.1-28.2 Psaumes 96.4 Psaumes 91.15 2 Samuel 22.4
4 Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Psaumes 116.3 Matthieu 27.24-27.25 2 Corinthiens 1.9 Matthieu 27.39-27.44 Psaumes 22.16
5 Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Psaumes 88.15-88.17 Ecclésiaste 9.12 Actes 2.24 Psaumes 116.3 Psaumes 88.3-88.8
6 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. Psaumes 50.15 Psaumes 34.15 2 Samuel 22.7 Psaumes 130.1-130.2 Actes 12.5
7 Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Juges 5.4 Actes 4.31 Habakuk 3.6 Ezéchiel 38.19-38.20 Psaumes 114.4-114.7
8 Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao. Psaumes 21.9 Nombres 11.1 Psaumes 50.3 Psaumes 104.32 Genèse 19.28
9 Aliziinamisha mbingu akashuka, Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Psaumes 68.4 Esaïe 51.6 Hébreux 12.26 Deutéronome 5.22-5.23 Deutéronome 33.26
10 Akapanda juu ya kerubi akaruka, Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo. Psaumes 104.3 Psaumes 99.1 Psaumes 80.1 Ezéchiel 1.5-1.14 2 Samuel 22.11-22.12
11 Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni. Psaumes 97.2 Deutéronome 4.11 Psaumes 91.1 Psaumes 81.7 Psaumes 27.5
12 Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Kukapita mawingu yake makuu. Mvua ya mawe na makaa ya moto. Josué 10.11 Matthieu 17.2 Psaumes 97.3-97.4 2 Samuel 22.13-22.15 Apocalypse 16.21
13 Bwana alipiga radi mbinguni, Yeye Aliye juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto. Psaumes 104.7 1 Samuel 7.10 Psaumes 29.3-29.4 Psaumes 140.10 Habakuk 3.5
14 Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya. Psaumes 144.6 Habakuk 3.11 Psaumes 77.17 Deutéronome 32.23 Josué 10.10
15 Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee Bwana, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako. Psaumes 106.9 Exode 15.8 Jérémie 31.37 Esaïe 11.4 2 Samuel 22.16
16 Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi. Psaumes 144.7 Exode 2.10 Jonas 2.5-2.6 2 Samuel 22.17 Psaumes 57.3
17 Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. Psaumes 35.10 Hébreux 2.14-2.15 Psaumes 142.6 2 Samuel 22.1 Job 16.9
18 Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu. Deutéronome 32.35 1 Samuel 30.6 Psaumes 46.1-46.2 Zacharie 1.15 Jérémie 18.17
19 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. Psaumes 118.5 Psaumes 31.8 Psaumes 37.23 Job 36.16 Psaumes 40.2
20 Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. Psaumes 24.4 1 Samuel 24.17 1 Samuel 24.11-24.13 Psaumes 26.6 Psaumes 7.8
21 Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu. Psaumes 119.102 Actes 24.16 Proverbes 8.32 1 Samuel 15.11 Psaumes 26.1
22 Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikujiepusha nazo. Psaumes 119.30 Jean 5.14 Psaumes 119.117 Psaumes 119.13 Psaumes 119.128
23 Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu. Matthieu 5.29-5.30 Psaumes 7.1-7.8 Matthieu 18.8-18.9 Psaumes 37.27 Psaumes 17.3
24 Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake. Ruth 2.12 1 Samuel 26.23 Matthieu 10.41-10.42 2 Thessaloniciens 1.6-1.7 Hébreux 6.16
25 Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; Matthieu 5.7 Matthieu 18.33-18.35 Psaumes 112.4-112.6 Néhémie 9.17 Luc 6.35-6.38
26 Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi. Proverbes 3.34 Lévitique 26.23-26.24 Lévitique 26.27-26.28 Jacques 2.13 Romains 2.4-2.6
27 Maana Wewe utawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. Psaumes 101.5 Luc 18.14 Psaumes 40.17 2 Corinthiens 8.9 Esaïe 3.9
28 Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; Bwana Mungu wangu aniangazia giza langu. Job 18.6 Psaumes 132.17 1 Rois 11.36 Job 29.3 Matthieu 4.16
29 Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. Ephésiens 6.10-6.13 2 Corinthiens 12.9-12.10 2 Samuel 22.30 1 Samuel 17.49 1 Corinthiens 15.10
30 Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia. Apocalypse 15.3 Psaumes 12.6 Deutéronome 32.4 Psaumes 17.7 Psaumes 19.7-19.10
31 Maana ni nani aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu? Psaumes 86.8 Esaïe 45.5 Deutéronome 32.31 Deutéronome 32.39 1 Samuel 2.2
32 Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Esaïe 45.5 2 Corinthiens 3.5 Psaumes 91.2 Psaumes 28.7 Psaumes 93.1
33 Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Habakuk 3.19 Deutéronome 32.13 2 Samuel 22.14 Deutéronome 33.29 2 Samuel 2.18
34 Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba. Psaumes 144.1 Jérémie 49.35 Esaïe 45.1 Osée 1.5 2 Samuel 22.36
35 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. 2 Samuel 22.36 Galates 5.22-5.23 Psaumes 28.7 Esaïe 22.3 Psaumes 45.3-45.4
36 Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza. Proverbes 4.12 2 Samuel 22.37 Luc 24.46-24.48 Job 18.7 Psaumes 4.1
37 Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe. Psaumes 44.5 Psaumes 9.3 Esaïe 53.10-53.12 Psaumes 35.2 Psaumes 35.5
38 Nitawapiga-piga wasiweze kusimama, Wataanguka chini ya miguu yangu. Psaumes 36.12 2 Samuel 5.1-5.25 1 Samuel 17.49-17.51 1 Samuel 30.17 2 Samuel 8.1-8.18
39 Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia chini yangu walioniondokea. Psaumes 18.32 Ephésiens 1.22 Philippiens 3.21 Jean 15.23 Psaumes 66.3
40 Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Nao walionichukia nimewakatilia mbali. Psaumes 21.12 Psaumes 94.23
41 Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita Bwana lakini hakuwajibu, Proverbes 1.28 Job 27.9 Esaïe 1.15 Zacharie 7.13 Osée 7.14
42 Nikawaponda kama mavumbi mbele ya upepo, Nikawatupa nje kama matope ya njiani. Zacharie 10.5 Esaïe 10.6 2 Rois 13.7 Esaïe 41.2 Esaïe 25.10
43 Umeniokoa na mashindano ya watu, Umenifanya niwe kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua walinitumikia. 2 Samuel 3.1 Esaïe 55.5 Romains 16.26 Ephésiens 1.22 2 Samuel 22.44-22.46
44 Kwa kusikia tu habari zangu, Mara wakanitii. Wageni walinijia wakinyenyekea. Psaumes 81.15 Psaumes 66.3 Deutéronome 33.29 Esaïe 62.8 2 Samuel 1.13
45 Wageni nao walitepetea, Walitoka katika ngome zao wakitetemeka. Michée 7.17 Esaïe 24.4 Apocalypse 6.16 Jacques 1.11
46 Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu; Psaumes 18.2 Psaumes 21.13 Psaumes 79.9 Psaumes 68.20 Jérémie 10.10
47 Ndiye Mungu anipatiaye kisasi; Na kuwatiisha watu chini yangu. Psaumes 47.3 Nahum 1.2 Romains 12.19 2 Samuel 22.48 Psaumes 144.2
48 Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu wa jeuri. Psaumes 140.1 Psaumes 59.1-59.2 Psaumes 140.4 Psaumes 7.16 Psaumes 22.27-22.30
49 Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako. Romains 15.9 Psaumes 138.4 Psaumes 72.18-72.19 Psaumes 14.7 2 Samuel 22.50-22.51
50 Ampa mfalme wake wokovu mkuu, Amfanyia fadhili masihi wake,Daudi na mzao wake hata milele. Psaumes 144.10 2 Samuel 7.13 Psaumes 132.10 Psaumes 78.71-78.72 Luc 1.31-1.33

Cette Bible est dans le domaine public.