Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 18.41
Bible en Swahili de l’est


1 Wewe, Bwana, nguvu zangu, nakupenda sana;2 Samuel 22.1-22.51 Colossiens 1.11 1 Jean 4.19 Esaïe 12.1-12.6 Psaumes 34.19
2 Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.Psaumes 144.2 Proverbes 18.10 Psaumes 28.1 Jérémie 16.19 Psaumes 132.17
3 Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.Psaumes 50.15 Luc 1.71 Psaumes 145.3 Psaumes 5.2-5.3 Psaumes 55.16
4 Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.Psaumes 116.3 2 Corinthiens 1.9 Matthieu 27.24-27.25 Psaumes 22.12-22.13 Esaïe 53.3-53.4
5 Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili.Psaumes 86.13 Psaumes 88.15-88.17 Ecclésiaste 9.12 Actes 2.24 Psaumes 116.3
6 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.Psaumes 50.15 2 Samuel 22.7 Psaumes 34.15 2 Chroniques 30.27 Psaumes 11.4
7 Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.Actes 4.31 Juges 5.4 Psaumes 46.2 Jérémie 4.24 Matthieu 28.2
8 Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao.Psaumes 21.9 Deutéronome 29.20 Daniel 7.10 Deutéronome 29.23-29.24 Nahum 1.5-1.6
9 Aliziinamisha mbingu akashuka, Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.2 Pierre 3.10 Joël 3.16 Matthieu 24.29 Marc 15.33 Psaumes 68.4
10 Akapanda juu ya kerubi akaruka, Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo.Psaumes 104.3 Psaumes 99.1 Ezéchiel 10.20-10.22 Psaumes 80.1 Ezéchiel 1.5-1.14
11 Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni.Psaumes 97.2 Deutéronome 4.11 Joël 2.2 Psaumes 91.1 Psaumes 81.7
12 Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Kukapita mawingu yake makuu. Mvua ya mawe na makaa ya moto.Josué 10.11 Habakuk 3.4-3.5 Matthieu 17.2 Psaumes 97.3-97.4 2 Samuel 22.13-22.15
13 Bwana alipiga radi mbinguni, Yeye Aliye juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto.Psaumes 104.7 1 Samuel 7.10 Psaumes 29.3-29.4 Exode 20.18 Apocalypse 8.5
14 Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya.Psaumes 144.6 Habakuk 3.11 Deutéronome 32.42 Psaumes 77.17 Deutéronome 32.23
15 Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee Bwana, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.Psaumes 106.9 Exode 15.8 Josué 3.13-3.16 Jonas 2.6 Esaïe 30.27-30.28
16 Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi.Psaumes 144.7 Exode 2.10 Jonas 2.5-2.6 2 Samuel 22.17 Psaumes 40.1-40.3
17 Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.Psaumes 35.10 Psaumes 142.6 Hébreux 2.14-2.15 Psaumes 9.13 Luc 19.14
18 Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu.Deutéronome 32.35 Psaumes 46.11 1 Samuel 30.6 Psaumes 46.1-46.2 Zacharie 1.15
19 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.Psaumes 118.5 Psaumes 31.8 Psaumes 37.23 Job 36.16 Psaumes 40.2
20 Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.Psaumes 24.4 Hébreux 7.26 Esaïe 62.11 1 Corinthiens 3.8 Psaumes 18.24
21 Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu.Psaumes 119.102 2 Chroniques 34.33 Actes 24.16 Proverbes 8.32 1 Samuel 15.11
22 Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikujiepusha nazo.Psaumes 119.30 Psaumes 119.112 Jean 5.14 Psaumes 119.117 Psaumes 119.13
23 Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu.1 Samuel 26.23 Matthieu 5.29-5.30 Psaumes 7.1-7.8 Matthieu 18.8-18.9 Psaumes 37.27
24 Mradi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.Matthieu 10.41-10.42 Ruth 2.12 1 Samuel 26.23 2 Thessaloniciens 1.6-1.7 Hébreux 6.16
25 Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;Matthieu 5.7 Matthieu 18.33-18.35 Ezéchiel 18.25-18.30 Esaïe 26.7 Psaumes 112.4-112.6
26 Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.Proverbes 3.34 Lévitique 26.23-26.24 Lévitique 26.27-26.28 Psaumes 109.17-109.19 Jacques 2.13
27 Maana Wewe utawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili.Psaumes 101.5 2 Samuel 22.28 Esaïe 10.12 Esaïe 57.15 Luc 1.52-1.53
28 Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; Bwana Mungu wangu aniangazia giza langu.Job 18.6 Psaumes 132.17 1 Rois 11.36 Job 29.3 Proverbes 20.27
29 Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.Ephésiens 6.10-6.13 2 Corinthiens 12.9-12.10 2 Samuel 22.30 Psaumes 44.6-44.7 Apocalypse 3.21
30 Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.Deutéronome 32.4 Apocalypse 15.3 Psaumes 12.6 Psaumes 17.7 Psaumes 84.11-84.12
31 Maana ni nani aliye Mungu ila Bwana? Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?Psaumes 86.8 1 Samuel 2.2 Esaïe 45.5 Deutéronome 32.31 Deutéronome 32.39
32 Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.Esaïe 45.5 2 Corinthiens 3.5 2 Samuel 22.33 Psaumes 91.2 Psaumes 28.7
33 Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.Habakuk 3.19 Deutéronome 32.13 2 Samuel 2.18 2 Samuel 22.14 Deutéronome 33.29
34 Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.Psaumes 144.1 Jérémie 49.35 Esaïe 45.1 Osée 1.5 2 Samuel 22.36
35 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza.2 Samuel 22.36 Esaïe 40.11 Galates 5.22-5.23 Psaumes 28.7 Esaïe 22.3
36 Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Na miguu yangu haikuteleza.Proverbes 4.12 2 Samuel 22.37 Luc 24.46-24.48 Job 18.7 Psaumes 4.1
37 Nitawafuatia adui zangu na kuwapata, Wala sitarudi nyuma hata wakomeshwe.Apocalypse 19.19-19.20 Psaumes 37.20 Esaïe 63.1-63.6 Psaumes 44.5 Psaumes 9.3
38 Nitawapiga-piga wasiweze kusimama, Wataanguka chini ya miguu yangu.2 Samuel 21.15-21.22 2 Samuel 10.1-10.19 Psaumes 36.12 2 Samuel 5.1-5.25 1 Samuel 17.49-17.51
39 Nawe hunifunga mshipi wa nguvu kwa vita, Hunitiishia chini yangu walioniondokea.Psaumes 18.32 Ezéchiel 30.24-30.25 1 Chroniques 22.18 Esaïe 45.14 Ephésiens 1.22
40 Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Nao walionichukia nimewakatilia mbali.Psaumes 21.12 Psaumes 94.23
41 Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita Bwana lakini hakuwajibu,Proverbes 1.28 Job 27.9 Ezéchiel 8.18 Job 35.12-35.13 Michée 3.4
42 Nikawaponda kama mavumbi mbele ya upepo, Nikawatupa nje kama matope ya njiani.Zacharie 10.5 Esaïe 10.6 2 Rois 13.7 Psaumes 50.22 Esaïe 41.2
43 Umeniokoa na mashindano ya watu, Umenifanya niwe kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua walinitumikia.2 Samuel 3.1 Esaïe 55.5 Apocalypse 11.15 Romains 15.18 2 Samuel 19.9
44 Kwa kusikia tu habari zangu, Mara wakanitii. Wageni walinijia wakinyenyekea.Psaumes 81.15 Psaumes 66.3 Deutéronome 33.29 Esaïe 62.8 2 Samuel 1.13
45 Wageni nao walitepetea, Walitoka katika ngome zao wakitetemeka.Michée 7.17 Jacques 1.11 Esaïe 24.4 Apocalypse 6.16
46 Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu;Psaumes 18.2 Psaumes 42.9 Psaumes 57.5 Esaïe 12.2 Exode 15.2
47 Ndiye Mungu anipatiaye kisasi; Na kuwatiisha watu chini yangu.Psaumes 47.3 Deutéronome 32.35 Nahum 1.2 Romains 12.19 2 Samuel 22.48
48 Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu wa jeuri.Psaumes 140.1 Psaumes 86.14 Psaumes 59.1-59.2 Psaumes 140.4 Psaumes 7.16
49 Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.Romains 15.9 Psaumes 108.3 Psaumes 138.4 Psaumes 72.18-72.19 Psaumes 14.7
50 Ampa mfalme wake wokovu mkuu, Amfanyia fadhili masihi wake,Daudi na mzao wake hata milele.Psaumes 144.10 2 Samuel 7.13 Psaumes 2.6 1 Chroniques 17.11-17.14 1 Samuel 2.10

Cette Bible est dans le domaine public.