Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 2.25
Bible en Swahili de l’est


1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.1 Corinthiens 16.8 Actes 20.16 Romains 15.6 Philippiens 1.27 Actes 4.32
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.Actes 4.31 Esaïe 65.24 1 Rois 19.11 Psaumes 18.10 Cantique 4.16
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.Matthieu 3.11 Jean 1.32-1.33 Actes 2.4 Jérémie 23.29 1 Corinthiens 12.10
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.Actes 13.52 Actes 4.31 Marc 16.17 Actes 9.17 Ephésiens 5.18
5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.Luc 2.25 Actes 8.2 Luc 17.24 Matthieu 24.14 Actes 10.7
6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.1 Corinthiens 16.9 2 Corinthiens 2.12 Matthieu 2.3 Actes 3.11 Actes 2.2
7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?Actes 2.12 Actes 1.11 Marc 1.27 Matthieu 21.11 Actes 3.10
8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia,1 Pierre 1.1 Actes 16.6 Actes 18.2 Genèse 14.1 Actes 19.10
10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,Actes 16.6 Actes 13.13 Actes 18.23 Actes 15.38 Actes 11.20
11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.1 Corinthiens 12.10 Exode 15.11 Psaumes 71.17 Psaumes 96.3 Actes 27.12
12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?Actes 2.7 Actes 17.20 Luc 18.36 Luc 15.26 Actes 10.17
13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.1 Corinthiens 14.23 Esaïe 25.6 Actes 2.15 1 Samuel 1.14 Zacharie 10.7
14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.Actes 7.2 Actes 5.35 Actes 1.26 Actes 2.22 Actes 21.28
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;1 Samuel 1.15 1 Thessaloniciens 5.5-5.8 Matthieu 20.3
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,Joël 2.28-2.32
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.Esaïe 44.3 Actes 10.45 Jean 7.39 Actes 21.9 Tite 3.4-3.6
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.Galates 3.28 Colossiens 3.11 Actes 21.10 1 Corinthiens 7.21-7.22
19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.Joël 2.30-2.31 Malachie 4.1-4.6 Sophonie 1.14-1.18
20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.2 Pierre 3.10 Matthieu 24.29 1 Thessaloniciens 5.2 Amos 8.9 Joël 2.1
21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.Romains 10.12-10.13 Actes 22.16 Joël 2.32 Matthieu 28.19 Psaumes 86.5
22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;Jean 3.2 Jean 14.10-14.11 Matthieu 12.28 Luc 11.20 Actes 4.10
23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;Luc 22.22 Actes 3.18 Actes 4.28 Esaïe 46.10-46.11 1 Pierre 1.20
24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.Colossiens 2.12 Hébreux 13.20 Ephésiens 1.20 Actes 2.32 1 Pierre 1.21
25 Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.Psaumes 16.8-16.11 Esaïe 50.7-50.9 Psaumes 62.6 Psaumes 109.31 Esaïe 41.13
26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.Psaumes 71.23 Psaumes 16.9 Psaumes 30.11 Psaumes 63.5 Psaumes 22.22-22.24
27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.Actes 2.31 Psaumes 86.13 Psaumes 49.15 Luc 1.35 Psaumes 89.19
28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.Psaumes 16.11 Psaumes 21.6 Proverbes 8.20 Psaumes 21.4 Psaumes 25.4
29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.Actes 13.36 1 Rois 2.10 Hébreux 7.4 Actes 7.8-7.9 Néhémie 3.16
30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;2 Samuel 23.2 Psaumes 132.11-132.18 2 Pierre 1.21 Psaumes 89.3-89.4 2 Samuel 7.11-7.16
31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.Psaumes 16.10 Actes 2.27 Actes 13.35 1 Pierre 1.11-1.12
32 Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.Actes 3.15 Actes 2.24 Actes 1.8 Actes 1.22 Actes 4.33
33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.Actes 1.4 Actes 10.45 Actes 5.31 Actes 2.17 Marc 16.19
34 Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa kuume.Psaumes 110.1 Matthieu 22.42-22.45 1 Corinthiens 15.25 Hébreux 1.13 Ephésiens 1.22
35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.Esaïe 60.14 Psaumes 72.9 Luc 20.16-20.18 Psaumes 21.8-21.12 Romains 16.20
36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.2 Corinthiens 5.10 2 Thessaloniciens 1.7-1.10 Jérémie 33.14 Jean 5.22-5.29 Romains 9.3-9.6
37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?Luc 3.10 Actes 5.33 Actes 7.54 Jean 16.8-16.11 Zacharie 12.10
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.Luc 24.47 Actes 8.12 Actes 22.16 Actes 10.48 1 Pierre 3.21
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.Joël 2.32 Actes 15.8 1 Corinthiens 7.14 Romains 8.30 Ephésiens 4.4
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.Matthieu 17.17 Deutéronome 32.5 Galates 5.3 Matthieu 23.33 2 Corinthiens 6.17
41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.Actes 4.4 Actes 2.47 Actes 2.37 Actes 1.15 Actes 13.48
42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.Hébreux 10.25 Actes 1.14 Actes 20.7 Actes 2.46 Hébreux 10.39
43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume.Actes 9.34 Actes 4.33 Actes 5.11-5.13 Jean 14.12 Marc 16.17
44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika,Actes 4.32 1 Jean 3.16-3.18 Actes 6.1-6.3 2 Corinthiens 9.6-9.15 2 Corinthiens 8.14-8.15
45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja.1 Jean 3.17 Actes 11.29 Actes 4.34-5.2 1 Timothée 6.18-6.19 Proverbes 19.17
46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,Actes 5.42 Actes 20.7 Luc 24.53 Actes 2.42 Actes 16.34
47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.Actes 11.24 Actes 2.41 Actes 16.5 Romains 14.18 Actes 5.13-5.14

Cette Bible est dans le domaine public.