Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Samuel 25.4
Bible en Swahili de l’est


1 Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama.Deutéronome 34.8 1 Samuel 28.3 Nombres 20.29 2 Chroniques 33.20 Genèse 21.21
2 Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa mkuu sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo zake huko Karmeli.Josué 15.55 Genèse 38.13 1 Samuel 23.24 Psaumes 73.3-73.7 Luc 16.19-16.25
3 Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake; naye alikuwa wa mbari ya Kalebu.Proverbes 31.26 Psaumes 10.3 Proverbes 31.10 1 Samuel 25.10-25.11 Josué 15.13
4 Basi Daudi akasikia huko nyikani ya kuwa Nabali alikuwa katika kuwakata manyoya kondoo zake.2 Samuel 13.23 Genèse 38.13
5 Daudi akatuma vijana kumi, Daudi naye akawaambia hao vijana, Kweeni mwende Karmeli, na kumwendea huyu Nabali ili mnisalimie;1 Samuel 17.22 Genèse 43.23
6 na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani na iwe kwako, na amani nyumbani mwako, na amani kwao wote ulio nao.1 Chroniques 12.18 Luc 10.5 Psaumes 122.7 1 Timothée 5.6 Matthieu 10.12-10.13
7 Nami sasa nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo zako; haya! Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli.1 Samuel 25.21 1 Samuel 25.15-25.16 1 Samuel 22.2 Esaïe 11.6-11.9 Philippiens 4.8
8 Waulize vijana wako, nao watakuambia; basi na wakubaliwe vijana hawa machoni pako; maana tumekujia katika siku ya heri; uwape, nakusihi, cho chote kitakachokujia mkononi, uwape watumwa wako na mwanao Daudi.Esther 9.19 Néhémie 8.10-8.12 1 Samuel 24.11 1 Samuel 3.6 Luc 14.12-14.14
9 Basi walipofika vijana wake Daudi, wakamwambia Nabali sawasawa na maneno hayo yote kwa jina la Daudi, kisha wakanyamaza.Genèse 8.4 2 Chroniques 14.7 2 Rois 2.15
10 Naye Nabali akawajibu wale watumishi wa Daudi, akasema, Huyu Daudi ni nani? Na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi kuna watumwa wengi wanaomtoroka kila mtu bwana wake!Juges 9.28 1 Samuel 22.2 Psaumes 73.7-73.8 Psaumes 123.3-123.4 Exode 5.2
11 Basi mimi je! Nitwae mkate wangu, na maji yangu, na machinjo yangu niliyowachinjia hao watu wangu wakatao manyoya kondoo zangu, na kuwapa watu ambao siwajui wametoka wapi?Juges 8.6 1 Samuel 25.3 Ecclésiaste 11.1-11.2 Jean 9.29-9.30 1 Samuel 24.13
12 Basi vijana wake Daudi wakageuka, wakaenda zao, wakarudi, nao wakaja wakamwambia sawasawa na maneno hayo yote.Hébreux 13.17 Esaïe 36.21-36.22 2 Samuel 24.13
13 Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao wakapanda nyuma yake Daudi, wapata kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa na vyombo vyao.1 Samuel 23.13 Proverbes 19.2 1 Samuel 24.5-24.6 Proverbes 25.8 Proverbes 14.29
14 Lakini kijana mmojawapo alimpasha habari Abigaili, mkewe Nabali, kasema, Tazama, Daudi alituma wajumbe kutoka nyikani waje ili kumsalimu bwana wetu, naye akawatukana.Marc 15.29 1 Samuel 13.10
15 Walakini watu hawa walitutendea mema sana, wala hatukupata dhara, wala sisi hatukupotewa na kitu cho chote, wakati wote tulipofuatana nao, tulipokuwako mavueni;1 Samuel 25.21 1 Samuel 25.7 Philippiens 2.15
16 watu hao walikuwa boma kwetu usiku na mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoo.Job 1.10 Exode 14.22 Jérémie 15.20 Zacharie 2.5
17 Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.1 Samuel 20.7 Deutéronome 13.13 1 Rois 21.13 1 Samuel 20.9 2 Samuel 23.6-23.7
18 Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.2 Samuel 16.1 1 Chroniques 12.40 Proverbes 6.4-6.5 Genèse 32.13-32.20 2 Samuel 17.28-17.29
19 Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.Genèse 32.20 Genèse 32.16 Proverbes 31.27 Proverbes 31.11-31.12
20 Ikawa, alipokuwa amepanda punda wake, na kutelemka penye sitara ya mlima, tazama, Daudi na watu wake walikuwa wakishuka kumkabili; naye akawakuta.2 Rois 4.24
21 Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema.Proverbes 17.13 1 Pierre 3.9 1 Pierre 2.20-2.23 1 Samuel 25.13 1 Pierre 3.17
22 Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.1 Samuel 3.17 1 Rois 14.10 1 Samuel 20.13 Ruth 1.17 2 Rois 9.8
23 Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi.1 Samuel 20.41 Juges 1.14 Josué 15.18 1 Samuel 24.8
24 Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako.2 Samuel 14.9 Genèse 44.33-44.34 2 Samuel 14.12 Genèse 44.18 Esther 8.3
25 Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.1 Samuel 25.17 Malachie 2.2 2 Samuel 13.33 1 Samuel 25.26 Esaïe 42.25
26 Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.2 Samuel 18.32 Hébreux 10.30 Genèse 20.6 Psaumes 44.3 1 Samuel 1.26
27 Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu.Genèse 33.11 1 Samuel 30.26 2 Rois 5.15 Juges 4.10 2 Samuel 16.2
28 Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.2 Samuel 7.11 1 Samuel 18.17 1 Samuel 24.11 2 Samuel 7.27 2 Samuel 7.16
29 Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.Jérémie 10.18 Psaumes 116.15 1 Samuel 2.9 Deutéronome 33.29 Psaumes 66.9
30 Tena itakuwa, hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli;1 Samuel 13.14 Psaumes 89.20 1 Samuel 23.17 1 Samuel 15.28
31 hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.Genèse 40.14 Proverbes 5.12-5.13 Romains 12.19 2 Corinthiens 1.12 1 Samuel 24.15
32 Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki;Luc 1.68 Genèse 24.27 Exode 18.10 Psaumes 72.18 2 Corinthiens 8.16
33 na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.1 Samuel 25.26 Proverbes 17.10 Proverbes 27.21 1 Samuel 26.9-26.10 Proverbes 25.12
34 Kwa kuwa ni kweli, aishivyo Bwana, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.Josué 10.6 Josué 10.9 1 Samuel 11.11 1 Samuel 25.18 1 Samuel 25.26
35 Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako.2 Rois 5.19 1 Samuel 20.42 Genèse 19.21 Luc 8.48 2 Samuel 15.9
36 Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hata kulipopambazuka.1 Samuel 25.19 2 Samuel 13.23 2 Samuel 13.28 Proverbes 20.1 Esther 1.3-1.7
37 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe.Proverbes 23.29-23.35 Job 15.21-15.22 1 Samuel 25.34 1 Samuel 25.22 Deutéronome 28.28
38 Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, Bwana alimpiga huyo Nabali, hata akafa.1 Samuel 26.10 2 Rois 19.35 Exode 12.29 2 Samuel 6.7 1 Samuel 6.9
39 Naye aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, Daudi alisema, Na ahimidiwe Bwana ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumwa wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali Bwana amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe.1 Samuel 25.26 1 Samuel 25.34 Psaumes 7.16 1 Rois 2.44 1 Samuel 25.32
40 Na hao watumishi wa Daudi walipomjia huyo Abigaili huko Karmeli, walimwambia, wakasema, Daudi ametutuma kwako ili tukutwae uwe mkewe.Genèse 24.51 Genèse 24.37-24.38
41 Naye akainuka na kujiinamisha kifulifuli mpaka nchi, akasema, Tazama, mjakazi wako ni mtumwa wa kuwaosha miguu watumishi wa bwana wangu.1 Timothée 5.10 Ruth 2.10 Proverbes 18.12 Proverbes 15.33 Ruth 2.13
42 Abigaili akafanya haraka, akainuka, akapanda punda, pamoja na vijakazi watano wake waliofuatana naye, akawafuata hao wajumbe wa Daudi, akawa mkewe.Genèse 24.61-24.67 Psaumes 45.10-45.11
43 Tena Daudi akamwoa Ahinoamu wa Yezreeli; wakawa wote wawili wakeze.Josué 15.56 1 Samuel 27.3 1 Samuel 30.5 2 Samuel 3.2 Genèse 2.24
44 Walakini Sauli alikuwa amempa Palti, mwana wa Laishi, aliyekuwa mtu wa Galimu, Mikali binti yake, aliyekuwa mkewe Daudi.1 Samuel 18.27 2 Samuel 3.14 1 Samuel 18.20 Esaïe 10.30

Cette Bible est dans le domaine public.