Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 27.32
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.1 Samuel 3.2 Genèse 48.10 Jean 9.3 Genèse 25.23-25.25 Ecclésiaste 12.3
2 Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.Ecclésiaste 9.10 1 Samuel 20.3 Genèse 47.29 Jacques 4.14 Marc 13.35
3 Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;Genèse 25.27-25.28 Genèse 10.9 1 Corinthiens 6.12
4 ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.Genèse 27.25 Hébreux 11.20 Genèse 49.28 Genèse 48.9 Genèse 14.19
5 Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete. 6 Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena,Genèse 25.28
7 Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za Bwana kabla ya kufa kwangu.Josué 6.26 1 Samuel 24.19 Deutéronome 33.1
8 Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza.Genèse 27.13 Actes 5.29 Ephésiens 6.1 Genèse 25.23 Genèse 27.43
9 Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo.1 Samuel 16.20 Juges 13.15
10 Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake. 11 Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini.Genèse 25.25
12 Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka.Deutéronome 27.18 Malachie 1.14 Genèse 27.36 Genèse 27.21-27.22 Genèse 9.25
13 Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee wana-mbuzi.Matthieu 27.25 2 Samuel 14.9 1 Samuel 25.24 1 Samuel 14.36-14.45 Genèse 25.33
14 Akaenda, akawatwaa, akamletea mamaye. Mamaye akafanya chakula kitamu namna ile aliyopenda babaye.Genèse 27.17 Genèse 27.4 Luc 21.34 Genèse 27.31 Proverbes 23.2-23.3
15 Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo.Genèse 27.27 Luc 20.46 Luc 15.22
16 Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake. 17 Naye akampa Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu, na mkate alioufanya. 18 Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu? 19 Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondoka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki.Esaïe 28.15 Genèse 27.21 Genèse 29.23-29.25 1 Rois 14.2 Genèse 25.25
20 Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu Bwana, Mungu wako, amenifanikisha.Job 13.7 Genèse 24.12 Exode 20.7
21 Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo.Genèse 27.12 Esaïe 57.19 Jacques 4.8 Psaumes 73.28
22 Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau. 23 Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki.Hébreux 11.20 Genèse 27.16 Romains 9.11-9.12
24 Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi.Job 13.7-13.8 Zacharie 8.16 1 Samuel 27.10 Proverbes 12.22 Colossiens 3.9
25 Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa.Genèse 27.4
26 Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. 27 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.Hébreux 11.20 Hébreux 6.7 Genèse 26.12 Cantique 4.11-4.14 Osée 14.6-14.7
28 Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo.Deutéronome 33.28 Deutéronome 33.13 Genèse 27.39 Deutéronome 7.13 2 Samuel 1.21
29 Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.Genèse 12.3 Nombres 24.9 Genèse 9.25-9.26 Romains 9.12 Genèse 27.37
30 Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake. 31 Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki.Genèse 27.4
32 Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.Genèse 27.18
33 Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.Genèse 28.3-28.4 Romains 11.29 Romains 5.20-5.21 Jean 10.28-10.29 Ephésiens 1.3
34 Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.Hébreux 12.17 Proverbes 1.31 Luc 13.24-13.28 Proverbes 19.3 Proverbes 1.24-1.28
35 Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.Malachie 2.10 2 Rois 10.19 Genèse 27.19-27.23 Job 13.7 2 Corinthiens 4.7
36 Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?Genèse 25.26 Genèse 25.31-25.34 Jean 1.47 Genèse 32.28
37 Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu?Genèse 27.28-27.29 2 Samuel 8.14 Romains 9.10-9.12 Genèse 25.23
38 Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.Hébreux 12.17 Genèse 27.34 Genèse 49.28 Esaïe 65.14 Genèse 27.36
39 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia,penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.Genèse 27.28 Hébreux 11.20 Josué 24.4 Genèse 36.6-36.8
40 Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.2 Rois 8.20-8.22 Genèse 25.23 2 Samuel 8.14 2 Rois 14.7 1 Rois 11.15-11.17
41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.Genèse 37.4 1 Jean 3.12-3.15 Genèse 50.3-50.4 Genèse 32.6 Genèse 37.8
42 Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua.Genèse 42.21-42.22 Psaumes 64.5 Job 20.12-20.14 Proverbes 4.16-4.17 1 Samuel 30.5
43 Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani;Genèse 11.31 Genèse 27.8 Genèse 27.13 Jérémie 35.14 Genèse 12.4-12.5
44 ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke;Genèse 31.38 Genèse 31.41
45 hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?2 Samuel 14.6-14.7 Lamentations 3.37 Genèse 4.8-4.16 Jacques 4.13-4.15 Proverbes 19.21
46 Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?Genèse 24.3 Genèse 26.34-26.35 Genèse 28.8 1 Rois 19.4 Nombres 11.15

Cette Bible est dans le domaine public.