Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 38
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Job 40.6 Exode 19.16-19.19 Job 37.14 2 Rois 2.1 Deutéronome 4.11-4.12
2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Job 35.16 Job 42.3 1 Timothée 1.7 Job 34.35 Job 27.11
3 Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Job 40.7 1 Pierre 1.13 Exode 12.11 Jérémie 1.17 1 Rois 18.46
4 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Psaumes 104.5 Proverbes 30.4 Hébreux 1.10 Hébreux 1.2 Proverbes 8.22
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Esaïe 40.12 Job 11.9 Psaumes 78.55 Esaïe 34.11 Proverbes 8.27
6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Job 26.7 Psaumes 104.5 Esaïe 28.16 Psaumes 118.22 2 Pierre 3.5
7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? Job 1.6 Job 2.1 Apocalypse 2.28 Psaumes 104.4 Apocalypse 22.16
8 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni. Genèse 1.9 Jérémie 5.22 Proverbes 8.29 Psaumes 104.8-104.9 Psaumes 33.7
9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Genèse 1.2
10 Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango, Psaumes 104.9 Job 26.10 Jérémie 5.22 Genèse 1.9-1.10 Psaumes 33.7
11 Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa? Psaumes 89.9 Apocalypse 20.2-20.3 Proverbes 8.29 Apocalypse 20.7-20.8 Luc 8.32-8.33
12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? Psaumes 74.16 Luc 1.78 Psaumes 136.7-136.8 Job 8.9 Psaumes 148.3-148.5
13 Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo? Job 37.3 Psaumes 104.35 Psaumes 104.21-104.22 Psaumes 19.4-19.6 Psaumes 139.9-139.12
14 Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi. Psaumes 104.6 Psaumes 104.2
15 Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika. Psaumes 10.15 Psaumes 37.17 Job 18.5 Ezéchiel 30.22 Job 5.14
16 Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi? Psaumes 77.19 Proverbes 8.24 Job 26.5-26.6 Jérémie 51.36
17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu? Psaumes 9.13 Psaumes 107.18 Job 3.5 Psaumes 107.10 Psaumes 23.4
18 Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote. Psaumes 89.11-89.12 Psaumes 74.17 Jérémie 31.37 Apocalypse 20.9 Esaïe 40.28
19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? Jean 1.9 Esaïe 45.7 Jérémie 13.16 Psaumes 105.28 Psaumes 104.20
20 Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake? Genèse 23.17 Job 26.10 Genèse 10.19
21 Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa! Job 15.7 Job 38.12 Job 38.4
22 Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, Job 37.6 Psaumes 135.7 Psaumes 33.7 Job 6.16
23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita? Josué 10.11 Esaïe 30.30 Apocalypse 16.21 Exode 9.18 Job 36.31
24 Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi? Matthieu 24.27 Job 38.12-38.13 Jonas 4.8
25 Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi; Job 28.26 Job 37.3-37.6 Job 36.27-36.28 Psaumes 29.3-29.10
26 Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu; Psaumes 107.35 Hébreux 6.7-6.8 Jérémie 14.22 Esaïe 35.1-35.2 Job 36.27
27 Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo? Psaumes 107.35 Psaumes 104.14
28 Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande? Jérémie 14.22 Psaumes 147.8 Job 38.8 Joël 2.23 Deutéronome 33.28
29 Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa? Psaumes 147.16-147.17 Job 37.10 Job 38.8 Job 6.16
30 Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi. Job 37.10
31 Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni? Amos 5.8 Job 9.9
32 Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake? Job 9.9 Job 38.31 2 Rois 23.5
33 Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia? Jérémie 31.35-31.36 Job 38.12-38.13 Genèse 8.22 Psaumes 148.6 Genèse 1.16
34 Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize? Job 22.11 1 Samuel 12.18 Zacharie 10.1 Job 36.27-36.28 Jacques 5.18
35 Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa? 2 Rois 1.14 Apocalypse 11.5-11.6 Nombres 16.35 2 Rois 1.10 Lévitique 10.2
36 Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni? Job 32.8 Psaumes 51.6 Ecclésiaste 2.26 Exode 36.1-36.2 Job 9.4
37 Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni? Genèse 9.15 Psaumes 147.4 Genèse 15.5 Genèse 8.1
38 Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja? 39 Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga, Psaumes 104.21 Psaumes 145.15-145.16 Job 4.10-4.11 Psaumes 34.10
40 Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia? Job 37.8 Nombres 24.9 Nombres 23.24 Genèse 49.9
41 Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula? Psaumes 147.9 Matthieu 6.26 Luc 12.24 Psaumes 104.27-104.28

Cette Bible est dans le domaine public.