6 Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawi, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi. Exode 39.2-39.7 Exode 26.1 7 Itakuwa na vipande viwili vya mabegani, vilivyoungana kwenye ncha zake mbili; ili ipate kuunganywa. Exode 39.4 8 Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa. Exode 29.5 Exode 28.27-28.28 Lévitique 8.7 Esaïe 11.5 Exode 39.20-39.21 9 Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu, ya rangi ya chani-kiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli; Ezéchiel 28.13 Exode 28.36 2 Chroniques 2.7 Exode 39.6 Cantique 8.6 10 majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao. Genèse 43.33 Exode 1.1-1.4 11 Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu. Exode 28.25 Exode 39.13 Exode 28.21 Apocalypse 7.2 2 Timothée 2.19 12 Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli; naye Haruni atayachukua majina yao mbele za Bwana juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho. Josué 4.7 Exode 28.29 Lévitique 24.7 Exode 39.6-39.7 Nombres 31.54 13 Nawe fanya vijalizo viwili vya dhahabu; 14 na mikufu miwili ya dhahabu safi; utaifanya iwe mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa; nawe uitie ile mikufu ya kazi ya kusokotwa katika vile vijalizo. 1 Rois 7.17 2 Chroniques 4.12-4.13 2 Rois 25.17 Exode 39.15 Exode 28.22-28.25
Le pectoral
15 Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya. Exode 39.8-39.21 Exode 28.30 Exode 28.4 Exode 28.6 Exode 26.1 16 Kitakuwa mraba, tena cha kukunjwa; urefu wake utakuwa shibiri moja, na upana wake shibiri moja. 17 Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza; Ezéchiel 28.13 Esaïe 54.11-54.12 Proverbes 3.15 Lamentations 4.7 Apocalypse 21.19-21.21 18 na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi; Ezéchiel 10.1 Jérémie 17.1 Ezéchiel 1.26 Exode 39.11 Apocalypse 4.3 19 na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto; Exode 39.12 Esaïe 54.12 20 na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake. Daniel 10.6 Ezéchiel 1.16 Apocalypse 21.11 Apocalypse 4.3 Ezéchiel 10.9 21 Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili. Apocalypse 21.12 Apocalypse 7.4-7.8 Jacques 1.1 Luc 22.30 1 Rois 18.31 22 Nawe utie katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa, ya dhahabu safi. 23 Nawe utie pete mbili za dhahabu katika kile kifuko cha kifuani, na kuzitia hizo pete mbili katika ncha mbili za kifuko cha kifuani. Exode 25.11-25.15 24 Nawe utie hiyo mikufu miwili ya dhahabu iliyosokotwa katika zile pete mbili zilizo katika ncha za kifuko cha kifuani. 25 Na ncha zile nyingine za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa utazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera upande wa mbele. Exode 39.4 Exode 28.14 Exode 39.15 26 Nawe utafanya pete mbili za dhahabu, uzitie katika hizo ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake, ulio upande wa naivera ulio ndani. 27 Nawe fanya pete mbili za dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi. 28 Nao watakikaza kile kileso kwa zile pete zake kwenye pete za naivera kwa ukanda wa rangi ya samawi, ili kwamba kikae pale juu ya ule mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, ili kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera. Nombres 15.38 Exode 28.37 Exode 39.30-39.31 Exode 28.31 29 Na Haruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya Bwana daima. Exode 28.12 Exode 28.30 Exode 28.15 Jérémie 30.21 Romains 10.1 30 Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Bwana; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Bwana daima. Deutéronome 33.8 Esdras 2.63 Lévitique 8.8 Nombres 27.21 Néhémie 7.65