Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 20.46
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa katika mwaka wa saba, mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, baadhi ya wazee wa Israeli walikuja ili kuuliza kwa Bwana, wakaketi mbele yangu.Ezéchiel 8.1 Ezéchiel 26.1 Ezéchiel 29.1 Ezéchiel 30.20 Ezéchiel 24.1
2 Neno la Bwana likanijia, kusema, 3 Mwanadamu, sema na wazee wa Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mmekuja kuniuliza neno? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.Michée 3.7 Proverbes 28.9 Jean 4.24 Ezéchiel 14.7-14.8 1 Samuel 28.6
4 Je! Utawahukumu, mwanadamu, utawahukumu? Uwajulishe machukizo ya baba zao;Ezéchiel 22.2 Ezéchiel 23.36 Luc 11.47-11.51 Jérémie 14.11-14.14 1 Corinthiens 6.2
5 uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile nilipochagua Israeli, na kuwainulia wazao wa nyumba ya Yakobo mkono wangu, na kujidhihirisha kwao katika nchi ya Misri, hapo nilipowainulia mkono wangu, nikisema, Mimi ni Bwana, Mungu wenu;Genèse 14.22 Deutéronome 7.6 Ezéchiel 47.14 Ezéchiel 20.15 Exode 3.8
6 katika siku ile naliwainulia mkono wangu, kuwatoa katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyowapelelezea, ijaayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote;Ezéchiel 20.15 Psaumes 48.2 Exode 3.8 Jérémie 32.22 Exode 33.3
7 nikawaambia, Kila mtu kwenu na atupilie mbali machukizo ya macho yake, wala msijitie unajisi kwa vinyago vya Misri, Mimi ni Bwana, Mungu wenu.Lévitique 18.3 Ezéchiel 18.31 Exode 20.2 Ezéchiel 20.8 Deutéronome 29.16-29.18
8 Lakini waliniasi, wala hawakutaka kunisikiliza; hawakutupilia mbali kila mtu machukizo ya macho yake, wala hawakuviacha vinyago vya Misri; ndipo nikasema kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao, katikati ya nchi ya Misri.Ezéchiel 20.21 Ezéchiel 7.8 Ezéchiel 5.13 Esaïe 63.10 Ezéchiel 20.7
9 Lakini nalitenda kwa ajili ya jina langu, ili lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao walikaa pamoja nao, ambao machoni pao nalijidhihirisha kwao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.Ezéchiel 20.14 Ezéchiel 39.7 Ezéchiel 20.22 Ezéchiel 36.21-36.22 Exode 32.12
10 Basi nikawatoa katika nchi ya Misri, nikawaleta jangwani.Exode 15.22 Exode 13.17-13.18 Exode 20.2 Exode 14.17-14.22
11 Nikawapa amri zangu, na kuwaonyesha hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda.Lévitique 18.5 Romains 10.5 Deutéronome 4.8 Néhémie 9.13-9.14 Psaumes 147.19-147.20
12 Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.Ezéchiel 20.20 Deutéronome 5.12-5.15 Exode 20.8-20.11 Lévitique 21.23 Ezéchiel 37.28
13 Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, wakazikataa hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda; na sabato zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize.Ezéchiel 20.21 Ezéchiel 20.8 Deutéronome 9.8 Ezéchiel 20.24 Esaïe 56.6
14 Lakini nalitenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi machoni pa mataifa, ambao naliwatoa mbele ya macho yao.Ezéchiel 20.9 Ephésiens 1.12 Ephésiens 1.6 Ezéchiel 20.22 Ezéchiel 36.22-36.23
15 Tena naliwainulia mkono wangu jangwani, ya kwamba sitawaingiza katika nchi ile niliyokuwa nimewapa, ijaayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote;Psaumes 95.11 Psaumes 106.26 Hébreux 3.11 Deutéronome 1.34-1.35 Hébreux 3.18
16 kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao.Nombres 15.39 Ezéchiel 20.8 Ezéchiel 14.3-14.4 Exode 32.1-32.8 Nombres 25.2
17 Walakini jicho langu likawahurumia nisiwaangamize kabisa, wala sikuwakomesha kabisa jangwani.Ezéchiel 11.13 Jérémie 5.18 Jérémie 4.27 Ezéchiel 8.18 Ezéchiel 9.10
18 Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao.1 Pierre 1.18 Deutéronome 4.3-4.6 Ezéchiel 20.7 Jérémie 2.7 Actes 7.51
19 Mimi ni Bwana, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda;Ezéchiel 11.20 Deutéronome 11.1 Ezéchiel 36.27 Deutéronome 5.6-5.7 Ezéchiel 37.24
20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.Jérémie 17.22 Ezéchiel 20.12 Esaïe 58.13 Exode 20.11 Néhémie 13.15-13.22
21 Lakini watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu, wala hawakuzishika hukumu zangu kuzitenda, ambazo mwanadamu ataishi kwazo kama akizitenda; walizitia unajisi sabato zangu, ndipo nikasema, kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao jangwani.Ezéchiel 20.13 Ezéchiel 20.8 Nombres 21.5 Deutéronome 31.27 Daniel 11.36
22 Lakini naliuzuia mkono wangu, nikatenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao mbele ya macho yao naliwatoa.Ezéchiel 20.14 Ezéchiel 20.9 Jérémie 14.21 Psaumes 78.38 Esaïe 48.9-48.11
23 Tena naliwainulia mkono wangu jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya mataifa, na kuwatapanya katika nchi mbalimbali;Lévitique 26.33 Ezéchiel 20.15 Apocalypse 10.5-10.6 Deutéronome 32.26-32.27 Jérémie 15.4
24 kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walizitia unajisi sabato zangu, na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao.Ezéchiel 6.9 Ezéchiel 20.16 Ezéchiel 20.13 Amos 2.4 Ezéchiel 18.15
25 Tena naliwapa amri zisizokuwa njema, na hukumu ambazo hawakuweza kuishi kwazo;Psaumes 81.12 Ezéchiel 20.39 Esaïe 66.4 Deutéronome 28.36 Ezéchiel 20.26
26 nami nikawatia unajisi kwa matoleo yao wenyewe, kwa kuwa walipitisha motoni wote waliofungua tumbo; ili kuwafanya kuwa ukiwa, wakapate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Lévitique 18.21 Ezéchiel 6.7 Ezéchiel 16.20-16.21 Ezéchiel 20.31 Esaïe 63.17
27 Basi, mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Baba zenu wamenitukana kwa jambo hili, kwa kuwa wamekosa kosa juu yangu.Romains 2.24 Ezéchiel 3.11 Ezéchiel 2.7 Ezéchiel 3.27 Ezéchiel 3.4
28 Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifanya nukato la kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.Ezéchiel 6.13 Josué 23.14 Esaïe 57.5-57.7 Jérémie 3.6 Jérémie 2.7
29 Ndipo nikawauliza, Nini maana yake mahali palipoinuka mnapopaendea? Basi, jina lake mahali pale ni Bama hata leo.Ezéchiel 16.31 Ezéchiel 16.24-16.25
30 Basi, uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mnajitia unajisi kwa kuzifuata njia za baba zenu? Mnakwenda kufanya uasherati kwa kuyafuata machukizo yao?Jérémie 16.12 Jérémie 7.26 Juges 2.19 Matthieu 23.32 Jérémie 9.14
31 Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi.Ezéchiel 20.26 Psaumes 106.37-106.39 Jérémie 7.31 Ezéchiel 20.3 Proverbes 1.27-1.28
32 Na haya yote yaingiayo katika nia zenu hayatakuwa kamwe; ikiwa mmesema, Sisi tutakuwa sawasawa na mataifa, sawasawa na jamaa za nchi nyingine, kutumikia miti na mawe.Ezéchiel 11.5 Jérémie 44.17 Apocalypse 9.20 Deutéronome 4.28 Daniel 5.4
33 Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika, nitakuwa mfalme juu yenu;Jérémie 21.5 Jérémie 42.18 Daniel 9.11-9.12 Jérémie 44.6 Ezéchiel 8.18
34 nami nitawatoa katika mataifa, na kuwakusanya, na kuwatoa katika nchi mlizotawanyika ndani yake, kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika;Ezéchiel 20.38 Ezéchiel 34.16 Amos 9.9-9.10 Jérémie 44.6 Lamentations 2.4
35 nami nitawaingiza katika jangwa la mataifa, na huko ndiko nitakakoteta nanyi uso kwa uso.Osée 2.14 Ezéchiel 17.20 Ezéchiel 20.36 Ezéchiel 19.13 Jérémie 2.35
36 Kama nilivyoteta na baba zenu katika jangwa la Misri, ndivyo nitakavyoteta nanyi, asema Bwana MUNGU.Nombres 11.1-11.35 1 Corinthiens 10.5-10.10 Ezéchiel 20.13 Ezéchiel 20.21 Nombres 25.1-25.18
37 Nami nitawapitisha chini ya fimbo, nami nitawaingiza katika mafungo ya agano.Jérémie 33.13 Lévitique 27.32 Matthieu 25.32-25.33 Ezéchiel 16.59-16.60 Amos 3.2
38 Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Ezéchiel 13.9 Amos 9.9-9.10 Zacharie 13.8-13.9 Psaumes 95.11 Malachie 3.3
39 Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Enendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago wenu.Ezéchiel 20.25-20.26 Ezéchiel 43.7 Esaïe 1.13-1.15 Juges 10.14 2 Rois 3.13
40 Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote.Esaïe 56.7 Esaïe 60.7 Malachie 3.4 Ezéchiel 17.23 Esaïe 66.23
41 Nitawatakabali kama harufu ipendezayo, nitakapowatoa katika mataifa, na kuwakusanya toka nchi zile mlizotawanyika; nami nitatakaswa kwenu machoni pa mataifa.Ezéchiel 28.25 Ezéchiel 11.17 Ezéchiel 28.22 Esaïe 5.16 Ezéchiel 38.23
42 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapowaingiza katika nchi ya Israeli, katika nchi ile ambayo niliuinua mkono wangu kwamba nitawapa baba zenu.Ezéchiel 38.23 Ezéchiel 34.13 Ezéchiel 36.23-36.24 Jean 17.3 Ezéchiel 24.24
43 Na huko mtazikumbuka njia zenu, na matendo yenu yote, ambayo mmejitia unajisi kwayo; nanyi mtajichukia katika macho yenu wenyewe, kwa sababu ya maovu yenu yote mliyoyatenda.Ezéchiel 6.9 Osée 5.15 Ezéchiel 36.31 Jérémie 31.18 Ezéchiel 16.61-16.63
44 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimetenda nanyi kwa ajili ya jina langu, si sawasawa na njia zenu mbaya, wala si sawasawa na matendo yenu mabovu, enyi nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.Ezéchiel 24.24 Ezéchiel 20.22 Ezéchiel 20.14 Ezéchiel 20.9 Ezéchiel 36.21-36.22
45 Neno la Bwana likanijia, kusema, 46 Mwanadamu, uelekeze uso wako kusini, ukadondoze neno lako upande wa kusini, ukatabiri juu ya msitu wa uwanda wa Negebu,Amos 7.16 Ezéchiel 21.2 Jérémie 13.19 Esaïe 30.6 Deutéronome 32.2
47 ukauambie msitu wa Negebu, Lisikie neno la Bwana; Bwana MUNGU asema hivi; Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hata kaskazini zitateketezwa kwa moto huo.Jérémie 21.14 Esaïe 9.18-9.19 Ezéchiel 17.24 Luc 23.31 Esaïe 24.1-24.6
48 Na watu wote wenye mwili wataona ya kuwa mimi, Bwana, nimeuwasha; hautazimika.Jérémie 40.2-40.3 Esaïe 26.11 Lamentations 2.16-2.17 2 Chroniques 7.20-7.22 Deutéronome 29.24-29.28
49 Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, wao hunisema; Je! Mtu huyu si mtu mwenye kupiga mithali?Jean 16.25 Ezéchiel 17.2 Actes 17.18 Matthieu 13.13-13.14

Cette Bible est dans le domaine public.