Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 24.3
Bible en Swahili de l’est


1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.Jean 20.1-20.2 Luc 24.10 Matthieu 27.55-27.56 Marc 16.1-16.8 Marc 15.40
2 Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,Jean 20.1-20.2 Matthieu 28.2 Marc 15.46-15.47 Marc 16.3-16.4 Matthieu 27.60-27.66
3 Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.Luc 24.23 Jean 20.6-20.7 Matthieu 16.5
4 Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;Marc 16.5 Actes 1.10 Genèse 18.2 Jean 20.11-20.12 Matthieu 28.2-28.6
5 nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?Apocalypse 1.18 Apocalypse 2.8 Luc 1.12-1.13 Actes 10.3-10.4 Luc 1.29
6 Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya,Luc 9.22 Matthieu 17.22-17.23 Luc 18.31-18.33 Matthieu 28.6 Marc 10.33-10.34
7 akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu.Matthieu 16.21
8 Wakayakumbuka maneno yake.Jean 12.16 Jean 14.26 Jean 2.19-2.22
9 Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote.Luc 24.22-24.24 Matthieu 28.7-28.8 Marc 16.10 Marc 16.7-16.8
10 Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao;Luc 8.2-8.3 Marc 15.40-15.41 Marc 6.30 Marc 16.9-16.11 Jean 20.11-20.18
11 hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo.Marc 16.11 Job 9.16 Actes 12.9 Luc 24.25 Genèse 19.14
12 Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hata kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.Jean 20.3-20.10
13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.Marc 16.12-16.13 Luc 24.18
14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.Luc 6.45 Malachie 3.6 Deutéronome 6.7
15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao.Luc 24.36 Jean 14.18-14.19 Matthieu 18.20
16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.Jean 21.4 Jean 20.14 Luc 24.31 2 Rois 6.18-6.20 Marc 16.12
17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.Ezéchiel 9.4-9.6 Jean 16.20-16.22 Jean 16.6
18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?Jean 19.25
19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;Matthieu 21.11 Actes 2.22 Actes 7.22 Jean 4.19 Marc 1.24
20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.Luc 23.13 Luc 22.66-23.5 Actes 13.27-13.29 Actes 4.27-4.28 Actes 4.8-4.10
21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;Luc 1.68 Luc 2.38 Psaumes 130.8 Esaïe 59.20 Apocalypse 5.9
22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,Jean 20.1-20.2 Luc 24.1-24.11 Jean 20.18 Marc 16.9-16.10 Matthieu 28.7-28.8
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. 24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.Luc 24.12 Jean 20.1-20.10
25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!Marc 8.17-8.18 Marc 9.19 Marc 16.14 Hébreux 5.11-5.12 Marc 7.18
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?1 Pierre 1.11 Hébreux 9.22-9.23 Actes 17.3 Luc 24.46 Esaïe 53.1-53.12
27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.Zacharie 9.9 Deutéronome 18.15 Jean 1.45 Esaïe 7.14 Esaïe 53.1-53.12
28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele.Marc 6.48 Genèse 32.26 Genèse 42.7 Genèse 19.2
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.Luc 14.23 2 Rois 4.8 Actes 16.14 Genèse 19.3
30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.Matthieu 14.19 Luc 24.35 Actes 27.35 Marc 14.22 Marc 6.41
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao.Luc 24.16 Luc 4.30 Jean 8.59 Jean 20.13-20.16
32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?Luc 24.45 Psaumes 39.3 Jean 6.63 Actes 17.2-17.3 Hébreux 4.12
33 Wakaondoka saa ile ile, wakarejea Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa pamoja nao,Marc 16.13 Jean 20.19-20.26 Actes 1.14
34 wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni.1 Corinthiens 15.5 Luc 22.54-22.62 Marc 16.7
35 Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao katika kuumega mkate.Marc 16.12-16.13 Luc 24.30-24.31 Actes 2.42
36 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.Marc 16.14 Jean 20.26 Jean 14.27 Jean 20.19-20.23 1 Corinthiens 15.5
37 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.Job 4.14-4.16 1 Samuel 28.13 Luc 16.30 Matthieu 14.26-14.27 Marc 6.49-6.50
38 Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?Hébreux 4.13 Jérémie 4.14 Daniel 4.19 Matthieu 16.8 Daniel 4.5
39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.Jean 20.27 1 Jean 1.1 Jean 20.20 Nombres 16.22 Jean 20.25
40 Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?Jean 21.5 Psaumes 126.1-126.2 Genèse 45.26-45.28 Jean 16.22 Jean 21.10-21.13
42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. 43 Akakitwaa, akala mbele yao.Actes 10.41
44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.Psaumes 72.1-72.20 Actes 13.33 Psaumes 118.22 Psaumes 110.1-110.7 Luc 9.22
45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.Actes 16.14 Psaumes 119.18 Job 33.16 Luc 24.32 1 Jean 5.20
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;Esaïe 53.2-53.12 Esaïe 50.6 Luc 24.44 Actes 17.3 Luc 24.26-24.27
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.Actes 5.31 Matthieu 28.19 Actes 2.38 Actes 13.46 Actes 11.18
48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.Actes 13.31 Actes 5.32 Actes 2.32 Actes 1.8 Actes 3.15
49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.Actes 1.4 Actes 1.8 Jean 14.26 Esaïe 44.3-44.4 Esaïe 59.20-59.21
50 Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki.Actes 1.12 Matthieu 21.17 Nombres 6.23-6.27 Hébreux 7.5-7.7 Genèse 27.4
51 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.Jean 20.17 Marc 16.19 2 Rois 2.11 Hébreux 1.3 Actes 1.9
52 Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu.Jean 16.22 Matthieu 28.9 Jean 14.28 Matthieu 28.17 1 Pierre 1.8
53 Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.Marc 16.20 Matthieu 28.20 Actes 2.46-2.47 Apocalypse 22.21 Actes 5.41-5.42

Cette Bible est dans le domaine public.