Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jean 11
Bible en Swahili de l’est


1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. Matthieu 21.17 Jean 12.17 Marc 11.1 Luc 10.38-10.42 Jean 11.3
2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. Jean 12.3 Marc 14.3 Luc 7.37-7.38 Matthieu 26.6-26.7
3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. Jean 11.5 Jean 11.36 Jean 11.11 Jean 13.23 2 Timothée 4.20
4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Jean 11.40 Jean 9.3 Jean 13.31-13.32 Jean 8.54 Jean 17.5
5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. Jean 11.36 Jean 15.9-15.13 Jean 16.27 Jean 17.26 Jean 11.8
6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. Esaïe 30.18 Esaïe 55.8-55.9 Genèse 42.24 Genèse 45.1-45.5 Genèse 44.1-44.5
7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. Actes 20.22-20.24 Luc 9.51 Actes 15.36 Jean 10.40-10.42
8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? Jean 10.31 Jean 8.59 Matthieu 16.21-16.23 Psaumes 11.1-11.3 Jean 10.39
9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. Jean 9.4 Jean 12.35 Jérémie 31.9 Proverbes 3.23 Luc 13.31-13.33
10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. 1 Jean 2.10-2.11 Jérémie 20.11 Jérémie 13.16 Ecclésiaste 2.14 Psaumes 27.2
11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Daniel 12.2 Marc 5.39 Actes 7.60 Jean 11.13 Matthieu 27.52
12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. Matthieu 9.24
14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. Jean 10.24 Jean 16.25 Jean 16.29
15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake. 2 Timothée 2.10 Jean 11.4 Esaïe 65.8 Jean 11.35-11.36 1 Jean 5.13
16 Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye. Matthieu 10.3 Jean 21.2 Jean 13.37 Luc 6.15 Marc 3.18
17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Jean 11.39 Actes 2.27-2.31 Osée 6.2 Jean 2.19
18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; Jean 11.1 Apocalypse 21.16 Jean 6.19 Apocalypse 14.20 Luc 24.13
19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. Job 2.11 Jean 11.31 1 Thessaloniciens 5.11 Lamentations 1.9 Lamentations 1.2
20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Luc 10.38-10.42 Actes 28.15 Jean 11.30 Matthieu 25.1 Matthieu 25.6
21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Jean 11.37 Jean 11.32 Jean 4.47-4.49 1 Rois 17.18 Luc 7.13-7.15
22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Jean 9.31 Jean 11.41-11.42 Marc 9.23 Matthieu 28.18 Psaumes 2.8
23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Jean 11.43-11.44
24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Actes 24.15 Jean 5.28-5.29 Esaïe 26.19 Luc 14.14 Psaumes 17.15
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 1 Thessaloniciens 4.14 Jean 1.4 Jean 3.36 Jean 6.39-6.40 Jean 6.44
26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? Jean 10.28 Jean 14.10 Jean 4.14 Jean 9.35 Jean 5.24
27 Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni. Matthieu 16.16 Jean 6.14 Malachie 3.1 Jean 6.69 1 Jean 5.1
28 Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. Jean 13.13 Marc 14.14 Jean 20.16 1 Thessaloniciens 4.17-4.18 Luc 22.11
29 Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea. Proverbes 15.23 Psaumes 27.8 Cantique 3.1-3.4 Psaumes 119.59-119.60 Proverbes 27.17
30 Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. Jean 11.20
31 Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko. Jean 11.19 Genèse 37.35 1 Corinthiens 2.15 2 Samuel 12.16-12.18
32 Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Jean 11.21 Jean 4.49 Luc 17.16 Luc 5.8 Apocalypse 5.8
33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, Jean 12.27 Jean 11.38 Genèse 43.30-43.31 Marc 3.5 Hébreux 4.15
34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Marc 16.6 Jean 20.2 Jean 1.39 Marc 15.47 Matthieu 28.6
35 Yesu akalia machozi. Luc 19.41 Jean 11.33 Hébreux 4.15 Jérémie 13.17 Esaïe 63.9
36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. Jean 11.3 Jean 14.21-14.23 Ephésiens 5.25 Ephésiens 5.2 Apocalypse 1.5
37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? Jean 9.6-9.7 Jean 11.21 Marc 15.32 Matthieu 27.40-27.42 Psaumes 78.19-78.20
38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. Matthieu 27.60 Jean 11.33 Luc 24.2 Esaïe 22.16 Jean 20.1
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Jean 11.17 Marc 16.3 Philippiens 3.21 Psaumes 49.9 Actes 13.36
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Jean 11.4 Jean 11.23-11.26 Romains 4.17-4.25 Jean 1.14 Psaumes 63.2
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Jean 17.1 Matthieu 11.25 Psaumes 123.1 Philippiens 4.6 Luc 10.21
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. Jean 3.17 Jean 17.21 Jean 17.8 Matthieu 26.53 Jean 11.22
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Actes 9.40 1 Rois 17.21-17.22 Luc 7.14-7.15 2 Rois 4.33-4.36 Actes 9.34
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake. Jean 20.7 Jean 19.40 Osée 13.14 Jean 20.5 Actes 20.9-20.12
45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. Jean 2.23 Jean 11.19 Jean 12.42 Jean 10.41 Jean 7.31
46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. Jean 9.13 Actes 5.25 Luc 16.30-16.31 Jean 5.15-5.16 Jean 12.37
47 Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. Matthieu 26.3 Matthieu 5.22 Jean 12.19 Actes 5.24 Psaumes 2.2-2.4
48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. Luc 21.20-21.24 Luc 8.12 Actes 5.38-5.40 Luc 19.41-19.44 Daniel 9.26-9.27
49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; Proverbes 26.12 Jean 18.13-18.14 Matthieu 26.3 Jean 11.51 Luc 3.2
50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. Jean 18.14 Luc 24.46 Jean 19.12 Romains 3.8 Jean 11.48
51 Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. Exode 28.30 1 Samuel 23.9 Galates 4.4-4.5 Matthieu 7.22-7.23 Nombres 22.28
52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja. Jean 10.16 Esaïe 49.6 1 Jean 2.2 Romains 3.29 Actes 18.10
53 Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua. Psaumes 109.4-109.5 Actes 5.33 Matthieu 22.46 Matthieu 16.21 Psaumes 71.10
54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. Jean 7.1 2 Chroniques 13.19 Jean 7.4 Jean 7.13 2 Samuel 13.23
55 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase. Jean 6.4 Jean 2.13 Exode 19.10 Jean 12.1 2 Chroniques 30.17-30.20
56 Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii? Jean 7.11 Jean 11.7-11.8
57 Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata. Jean 10.39 Psaumes 109.4 Jean 8.59 Jean 9.22 Jean 5.16-5.18

Cette Bible est dans le domaine public.