Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 2.48
Bible en Swahili de l’est


1 Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.Luc 3.1 Matthieu 24.14 Actes 11.28 Marc 14.9 Actes 25.21
2 Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.Luc 3.1 Actes 26.30 Matthieu 4.24 Actes 5.37 Actes 18.12
3 Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. 4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;Michée 5.2 Jean 7.42 1 Samuel 16.1 Matthieu 2.23 Luc 1.26-1.27
5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.Matthieu 1.18-1.19 Deutéronome 22.22-22.27
6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,Michée 5.2 Apocalypse 12.1-12.5 Luc 1.57 Psaumes 33.11 Proverbes 19.21
7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.Jean 1.14 Galates 4.4 Esaïe 53.2-53.3 2 Corinthiens 8.9 Matthieu 1.25
8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.Jean 10.8-10.12 Genèse 31.39-31.40 Ezéchiel 34.8 Exode 3.1-3.2 1 Samuel 17.34-17.35
9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.2 Corinthiens 3.18 1 Timothée 3.16 2 Corinthiens 4.6 Luc 24.4 1 Rois 8.11
10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;Esaïe 52.7 Matthieu 28.18 Psaumes 98.2-98.3 Genèse 12.3 Esaïe 40.9
11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.Esaïe 9.6 Matthieu 1.21 Luc 1.43 Actes 2.36 Matthieu 16.16
12 Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.Esaïe 7.14 Esaïe 53.1-53.2 Esaïe 7.11 Psaumes 22.6 1 Samuel 2.34
13 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,1 Rois 22.19 Apocalypse 5.11 Genèse 28.12 Psaumes 103.20-103.21 Psaumes 148.2
14 Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.Luc 1.79 Colossiens 1.20 Luc 19.38 Apocalypse 5.13 Esaïe 9.6-9.7
15 Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.2 Rois 2.11 Jean 20.1-20.10 Psaumes 111.2 Matthieu 2.9-2.11 Matthieu 2.1-2.2
16 Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.Luc 2.7 Luc 19.32 Luc 2.12 Luc 22.13 Luc 1.39
17 Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.Jean 4.28-4.29 Psaumes 16.9-16.10 Luc 2.38 Psaumes 66.16 Psaumes 71.17-71.18
18 Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.Luc 5.9-5.10 Luc 4.36 Esaïe 8.18 Luc 1.65-1.66 Luc 2.47
19 Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.Luc 2.51 Genèse 37.11 Luc 1.66 1 Samuel 21.12 Luc 9.43-9.44
20 Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.Actes 11.18 Matthieu 9.8 1 Chroniques 29.10-29.12 Psaumes 107.21 Luc 18.43
21 Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.Luc 1.31 Luc 1.59 Genèse 17.12 Lévitique 12.3 Matthieu 1.25
22 Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana,Lévitique 12.1-12.8
23 (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana),Exode 13.2 Nombres 3.13 Exode 22.29 Nombres 8.16-8.17 Nombres 18.15
24 wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.Lévitique 12.6-12.8 2 Corinthiens 8.9 Lévitique 12.2
25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.Luc 1.6 Luc 2.38 Marc 15.43 Esaïe 25.9 Esaïe 40.1
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.Jean 8.51 Hébreux 11.5 Luc 9.27 Actes 2.36 Actes 10.38
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,Luc 2.51 Apocalypse 17.3 Luc 2.41 Actes 10.19 Luc 2.48
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,Luc 1.64 Luc 2.20 Marc 10.16 Luc 2.13-2.14 Luc 1.46
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;Genèse 15.15 Luc 2.26 Esaïe 57.1-57.2 Apocalypse 14.13 Philippiens 1.23
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,Luc 3.6 Luc 2.10-2.11 Esaïe 52.10 Esaïe 49.6 Actes 4.10-4.12
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;Psaumes 98.2-98.3 Psaumes 96.1-96.3 Esaïe 42.10-42.12 Psaumes 96.10-96.13 Esaïe 62.1-62.2
32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.Esaïe 49.6 Esaïe 60.1-60.3 Actes 26.23 Esaïe 42.6-42.7 Esaïe 60.19
33 Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake.Luc 1.65-1.66 Luc 2.48 Esaïe 8.18
34 Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.1 Corinthiens 1.23 1 Pierre 2.7-2.8 Matthieu 21.44 Actes 9.1-9.20 Osée 14.9
35 Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.Deutéronome 8.2 Juges 5.15-5.16 Luc 16.14-16.15 Actes 8.21-8.23 Matthieu 12.24-12.35
36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.Actes 21.9 Genèse 30.13 Exode 15.20 Apocalypse 7.6 Job 5.26
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.1 Timothée 5.5 Actes 14.23 Actes 13.3 Actes 26.7 Luc 5.33
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.Luc 2.25 Marc 15.43 Luc 1.68 Luc 24.21 2 Corinthiens 9.15
39 Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.Luc 2.4 Deutéronome 12.32 Galates 4.4-4.5 Matthieu 2.22-2.23 Luc 2.51
40 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.Luc 2.52 Luc 1.80 Psaumes 22.9 Jean 1.14 Luc 2.47
41 Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka.Deutéronome 12.18 Deutéronome 16.1-16.8 Jean 2.13 1 Samuel 1.3 Jean 6.4
42 Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; 43 na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari.Exode 12.15 2 Chroniques 30.21-30.23 2 Chroniques 25.17
44 Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;Psaumes 42.4 Esaïe 2.3 Psaumes 122.1-122.4
45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.1 Rois 12.12 Esaïe 49.1-49.2 Luc 5.17 Esaïe 50.4 Matthieu 16.21
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.Matthieu 7.28 Luc 4.32 Marc 1.22 Jean 7.15 Luc 4.22
48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.Luc 4.22 Luc 2.49 Matthieu 12.46 Luc 3.23
49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?Malachie 3.1 Psaumes 40.8 Jean 4.34 Jean 5.17 Jean 6.38
50 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia.Luc 18.34 Luc 9.45 Marc 9.32
51 Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.Luc 2.19 Genèse 37.11 Marc 6.3 Daniel 7.28 Matthieu 3.15
52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.Luc 2.40 1 Samuel 2.26 Proverbes 3.3-3.4 Luc 1.80 Romains 14.18

Cette Bible est dans le domaine public.